Tanzania kulipa mishahara bidhaa badala ya pesa?

Netanyahu

Senior Member
Oct 2, 2008
147
22
Kuna mzee mstaafu nilikutana naye alinieleza mambo ya ajabu ya namna ya kuinua mauzo ya bidhaa za Tanzania.

Aliniambia kuwa Kuna kiwanda Tanzania kilikuwa kinajulikana kama LIGHT SOURCE kilikuwa kinatengeneza taa (Bulbs) kikiwa pale kule Pugu ROAD Dar es salaam mkono wa kulia kama unaenda Airport karibu na D.T.DOBIE.Kabla ya kufilisika kilifikia mahali kikawa hakina hela kabisa kiasi cha kushindwa kulipa mishahara na pesa za likizo za wafanyakazi wake.

Uongozi wa kiwanda ukasoma sheria za kazi na kodi wakaona mahali pameandikwa “payments benefits can be in cash or in kind”

Wakati ule bulb zilikuwa zimejazana kwenye bohari ya kiwanda zikiwa haziuziki kutokana na soko huria na ushindani.Basi ikawa mfanyakazi ukiomba likizo ilikuwa hulipwi mshahara hela taslimu bali unapigiwa pesa yako inayolingana na hela ya Likizo halafu unapewa mabox ya balbu zinazolingana na hela ya likizo ukauze uende zako likizo huko kijijini kwenu.

Mzee huyo akashauri kuwa Ili kuongeza soko la bidhaa zetu zinazozalishwa ndani ni vyema wafanyakazi wa serikali Tanzania wawe wapewe vitu vinavyozalishwa Tanzania wakauze ili wapate hiyo mishahara na marurupu yao badala ya kuwapa hela Taslimu.Akasema kitu kama hicho kitakasaidia kupanua soko la bidhaa zetu na watu watapenda kuziuza na kuzitumia maana watu watapigana kufa na kupona ili wauze wapate chao.Pia itasaidia kupata ufumbuzi wa wa wafanyakazi wanaolalamikia serikali kuwa mishahara ni midogo haitoshi kwa kuwa kila mmoja itakuwa ni juhudi yake tu ukiongea vizuri ukapata bei kubwa zaidi unapouza kile cha juu ni halali yako.

Fikiria Raisi Kikwete mwisho wa Mwezi umefika halafu anapewa mananasi yaliyokosa soko Kijijini kwao Msata akayauze huko kwenye safari zake anazoenda nje mara kwa mara ili apate posho za safari na mshahara wake si uchumi ungeinuka?

Habari ndo hiyo.

Wadau mnasemaje?
 
Mkuu
Kuna bidhaa zingine haziwezi kuuzika, chukua mfano askari/polisi je huyu mwajiri wake atampatia nini ili naye aweze kuuza ili apate chochote kitu. Mimi nadhani ni vyema kuzalisha bidhaa bora na kuwaelimisha watanzania kupenda kutumia bidhaa za nyumbani kuliko kupenda vya ughaibuni. Kuna bidhaa ambazo tunaweza zalisha vizuri tu hapa nchini kwa wingi tu bila kutegemea kuagiza nje. vile vile kwa mamlaka husika ni kutoa unafuu wa kodi kwa bidhaa zetu punde pale zinapotumika katika soko la ndani ili bei zake ziweze kushindana na bidhaa tunazoagiza toka nje. Na kwa bidhaa zinazotoka nje ambazo tunaweza kuzizalisha hapa nchini zitozwe kodi zaidi ili kunusuru bidhaa zetu.
 
Viongozi wetu hapa Tanzania ni watu wanaosafiri sana nchi za nje kila kukicha lakini wakiwa huko hawajifunzi wenzetu wanafanya nini kulinda uchumi wao. Leo hii Japan haiwezekani mtu kuimport rice/mchele katika chi ile kutoka nchi za nje, yote hiyo kulinda soko la mchele wao; leo hii sisi hapa mfano mdogo tu ni wa kiwanda cha kutengezea viberiti pale Moshi, kile kiwanda hakiwezi kuuza bidhaa zake kwasababu tumeruhusu viberiti kuingizwa toka nchi za nje!; matokeo yake ni kwamba watu wengi hawawezikuajiliwa, serikali inakosa kodi na uchumi wetu kuathirika; huo ni mfano wa bidhaa moja tu!! Ili kuongeza ajira kwa vijana wetu viwanda vyetu sharti vizalishe na haviwezi kuzalisha kama haviuzi kwa hiyo serikali yetu lazima iweinward looking kulinda maslahi ya nchi!!
 
Back
Top Bottom