Tanzania kuingia gizani yatimia

Ihselegn

Member
Nov 3, 2011
20
1
Lizemwalo lipo kama halipo laja, leo ni siku ya pili mji wa kigamboni upo gizani, maji yawashida, msemaji hamna, Tanzania tutafika?
 
Sijui ni mgao umeanza lakini umeanzia Kigamboni maana naona wanakata zaidi ya 12hrs na hakuna info yoyote..Tanesco wanazima simu au inatoa busy signal. Nilidhani Ngeleja alisema mwisho wa mgao Desemba 2011 maana wameingia mikataba kibao na megawatt za kutosha zitazalishwa?? Did I miss something?
 
since when did politicians start speaking the truth?
 
Na sio siku mbili tu bali ni zaidi na pia si Kigamboni tu bali kuna baadhi ya maeneo mengi hapa Dar ambayo pia yameathirika na hakuna msemaji sijui tuwaeleje na isitoshe wamebebwa sana hawa na serikali kwani bajeti yao iko juu huduma ziro
 
Angalieni Kigamboni, isije kuwa ndio wameamua kuwafukuza kijanja. Kwa kuwa mnapiga kelele sana kupinga Mradi wa mji mpya. Sasa wanaanza na Umeme kuwakatia, kisha Simu, Vivuko vinaondolewa mtaambiwa vyote viwili ni vibovu kwa wakati mmoja, barabara inayoingia kupitia Kibada itafungwa.

Sijui mtafikaje huko au kutoa vipi. Yaani kila nikiangalia sipati :photo:

Miaka 50 ya Uhuru Tanzania

MIZAMBWA
INANIUMA SANA.
 
Mabwepande kuna maeneo ya kumwaga
 
I like science make ukweli wake haufichawagi. TANESCO siku zake zinahesabika hata iajiri information minister wa sadam Hussein hata badili ukweli huo. Yetu macho.
 
Mabwepande kuna maeneo ya kumwaga

Tatizo watu wa Kigamboni hawataki kutoka kule. Wameshajenga mahekalu yao inakuwa shida kuhamia mabwe Pande.

na sisi tukiwa kama viooo ngozi wenu mliotuchagua tule mali za nji hii tumeamua kuuza Kigamboni.

TOKEEEEEEEEEEENI HUKO MTUPISHE TUWAPE WAZUNGU WANAOSTAHILI KUISHI KARIBU NA BAHARI.

VINGINEVYO TUNAWAPIGA MABOMU NA MAJI WASHA!!!!!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kigamboni wamezidi kutukatia umeme, ni kama tupo kwenye mgao. Hakuna tofauti na wakati ule wa mgao. Kila siku lazima umeme ukatike. Hali imeongezeka makali baada tu ya malumbano ya kivuko na Mzee wa Piga Mbizi.
Tuhurumieni jamani, kama ni adhabu imetosha. Wengine huku umeme ndio maisha.
 
Mizambwa umenifurahisha kweli...Kama hizo ndizo hatua za kutuhamisha basi wamefaulu maana wakikata umeme, maji pia hatuna. Kule hatuna maji yenu yenye dawa, ni visima tu ambavyo vinatumia pampu kupandisha maji..so hatuna huduma zote muhimu..umeme na maji..patamu kweli.

On a serious note, nimeongea na officer mmoja wa Tanesco Kigamboni 0788499014-Emergency line amesema tatizo lipo kwenye nyaya zinazotoka Kurasini kuja Kigamboni ambazo amesema zimeungua ZOTE...hazifai tena..thus wanatafuta another route ya kupeleka umeme K'mboni wakati wanashughulikia swala la nyaya.
Kuhusiana na umeme kukatika-katika karibu kila siku anasema kwamba umeme ukiwa mdogo kwenye transformer Ilala basi inajizima yenyewe then baadaye inaboot...?????

Well, mlioko huku ng'ambo mvuke na madumu ya maji otherwise...hakuna matumaini. Mercy!
 
On a serious note, nimeongea na officer mmoja wa Tanesco Kigamboni 0788499014-Emergency line amesema tatizo lipo kwenye nyaya zinazotoka Kurasini kuja Kigamboni ambazo amesema zimeungua ZOTE...hazifai tena..Kuhusiana na umeme kukatika-katika karibu kila siku anasema kwamba umeme ukiwa mdogo kwenye transformer Ilala basi inajizima yenyewe then baadaye inaboot...?????

Inabidi tukupongeze kwa jitihada zako za kufuatilia suala hili la kukatika ovyo umeme Kigamboni. Ingawa Tanesco wenyewe hawatoi Tangazo lolote utashangaa umeme unazima tu.

Kuhusu kuungua kwa nyaya - Ina maana walikueleza kuwa itachukua siku ngapi kurekebisha, kwani wananchi wapo gizani siku mbili ni hatari. na je, ingekuwa ni LINE inayoenda IKULU wangekaa kimya siku mbili bila matengenezo wanatafuta njia nyingine kama wanavyofanya kwa Kigamboni. ISIWE NDIZO AHADI ZA kISIASA ZIMEINGIA HADI TANESCO.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Mizambwa umenifurahisha kweli...Kama hizo ndizo hatua za kutuhamisha basi wamefaulu maana wakikata umeme, maji pia hatuna. Kule hatuna maji yenu yenye dawa, ni visima tu ambavyo vinatumia pampu kupandisha maji..so hatuna huduma zote muhimu..umeme na maji..patamu kweli. On a serious note, nimeongea na officer mmoja wa Tanesco Kigamboni 0788499014-Emergency line amesema tatizo lipo kwenye nyaya zinazotoka Kurasini kuja Kigamboni ambazo amesema zimeungua ZOTE...hazifai tena..thus wanatafuta another route ya kupeleka umeme K'mboni wakati wanashughulikia swala la nyaya. Kuhusiana na umeme kukatika-katika karibu kila siku anasema kwamba umeme ukiwa mdogo kwenye transformer Ilala basi inajizima yenyewe then baadaye inaboot...????? Well, mlioko huku ng'ambo mvuke na madumu ya maji otherwise...hakuna matumaini. Mercy!
Shukrani kwa ufuatiliaji na kutujuza.
 
Kuhusu kuungua kwa nyaya - Ina maana walikueleza kuwa itachukua siku ngapi kurekebisha, kwani wananchi wapo gizani siku mbili ni hatari. na je, ingekuwa ni LINE inayoenda IKULU wangekaa kimya siku mbili bila matengenezo wanatafuta njia nyingine kama wanavyofanya kwa Kigamboni. ISIWE NDIZO AHADI ZA kISIASA ZIMEINGIA HADI TANESCO.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Ndugu yangu Mzw....hawakusema itachukua siku ngapi...japokuwa uzembe unaojidhihirisha ni mkubwa sana. Ingekuwa ni ikulu wangevuta hata kutoka nje ya nchi. Naona jana walivuta kutoka wapi maana ulikuwa unacheza cheza kweli pia mdogo sana..sasa sijui ndio style yenyewe wanatupa wa kuonja au bado mambo hayajatengemaa...dunno...but hawa watu wanatuumiza.

I have a feeling Mizambwa, kuwa watu wanataka kuiua Tanesco ili wachukue tender...nionavyo mimi..yaani wanaitengenezea mazingira magumu sana hadi wananchi wanaikinai na kuichukia kabisa then wanaleta option 2 ambayo obviously itakuwa better machoni kwa watu kulinganisha na option 1...thus shirika linaachia ngazi, wenye akili zao wanachukua tender. Huu ni mtizamo wangu tuu ambao nauona unafanya kazi sana katika system ya kibepari.
 
Na sio siku mbili tu bali ni zaidi na pia si Kigamboni tu bali kuna baadhi ya maeneo mengi hapa Dar ambayo pia yameathirika na hakuna msemaji sijui tuwaeleje na isitoshe wamebebwa sana hawa na serikali kwani bajeti yao iko juu huduma ziro

Serikali ndiyo inaitwisha mzigo mzito Tanesco,nayo in turn inabebesha mzigo wananchi...
 
Back
Top Bottom