Tanzania; Kinara wa kuuza Ardhi Afrika

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Jarida la The African Report, limefichua dili la serikali la kuimilikisha ardhi yenye ukubwa wa hekari zaidi ya 300,000 kwenye Bonde la Mto Rufiji lililoko mkoani Pwani kwa kampuni ya Muasia wa Bangalore inayojulikana kama Karutari Global.
Jarida hilo limeripoti kuwa mwekezaji huyo anatarajiwa kujipatia hekari hizo iwapo mipango hiyo inayojadiliwa itakwenda vizuri.
Kadhalika jarida linasema Tanzania inaongoza barani Afrika eneo la Kusini mwa Jangwa Sahara kwa kumilikisha kiasi kikubwa cha ardhi yake kwa wawekezaji wa kigeni na kwamba hadi sasa imetoa hekari zaidi ya milioni moja za maeneo yenye rutuba kwa wawekezaji wa nje.
Habari za kuuza ardhi ya Afrika zimechapishwa kwenye jarida hilo toleo namba 41 la Julai 2012, lenye kichwa cha habari toleo maalumu “Namna wanasiasa walivyoachia Dola bilioni 100 za ardhi. Taarifa maalumu ya uchunguzi wa siri ya dili anayotishia mamilioni ya wakulima wa Afrika.”
Ripoti maalumu iliyochapishwa kurasa za 23 na 24 za jarida hilo inaitaja Tanzania kuwa imeuza hekari 1,083,000 za ardhi kuanzia mwaka 2006 na kuanika kuwa watuhumiwa wa ufisadi huo wa ardhi ni wanasiasa na viongozi wa serikali ambao hugawa ardhi ya taifa kwa wageni kwa kuingia ubia na wageni .
“Wakati mwingine wanajichukulia ardhi bila kufuata taratibu na sheria zilizopo. Huwahonga viongozi wa vijiji na kuwashinikiza kuitisha mikutano ya haraka inayowezesha kutimiza azma hizo,” jarida hilo likimkariri Barnaba Baha wa asasi ya kimataifa ya Action Aid.
Ripoti inasema kwenye bonde la Mto Rufiji mpango wa kuuza zaidi ya hekari 300,000 unaendelea na kuitaja kampuni ya India ya Karutari Global iliyowekeza nchini Ethiopia kuwa ndiyo inayokusudiwa kupewa eneo hilo.
Jarida linaeleza kuwa Karutari Global ni kampuni ya Bangalore inayomilikiwa na Muasia Sai Ramakrishna Karutari aliyeelezwa kuwa ni mmiliki wa majumba ya kuendesha kilimo (green house) yanayozalisha miche zaidi ya milioni 650 za maua ya rozi kila mwaka .
Jarida linawakariri wasemaji wa Benki ya Dunia (WB) wakishangaa uuzaji huo wa ardhi kwa kile wanachokiita ni dili dhidi ya maili za mraba milioni 1.5 za ardhi ambazo hazijaguswa lakini sasa zinatolewa kwa wawekezaji wa kigeni na tawala za Kiafrika.
Watafiti wanaeleza kuwa uporaji huu wa ardhi ni aina nyingine ya kugombea Afrika kama ule uliofanyika mwaka 1885 baada ya mkutano wa Berlin ulioigawa Afrika kwa wakoloni ambapo Tanganyika ( sasa Tanzania ) ilichukuliwa na Wajerumani.
Mtafiti kutoka Ethiopia akizungumzia kiama cha wakulima wa Afrika alikaririwa na jarida hilo: “Ninasema kinachotokea barani Afrika ni kuigombea Afrika lakini kwa hili la sasa ni serikali zenyewe kupora ardhi za watu wake na kuwazawadia wawekezaji.”
Kama kawaida jarida hilo linaeleza kuwa viongozi wa Afrika wameendelea kuimbiwa nyimbo za hadaa kuwa uwekezaji utaleta ajira kwa vijana, utaboresha teknolojia ya kilimo na kuongeza uzalishaji utaokaopunguza umaskini.
Habari hizo zinaitaja Tanzania, Kenya, Zambia, Uganda, Kongo , Ethiopia, Mali, Msumbiji na Liberia kuwa zinaonyesha sura ya serikali za Afrika zinavyojizatiti kuvutia mitaji ya nje kwenye sekta ya kilimo.
Hata hivyo jarida linaeleza kuwa cha kushangaza mipango ya kujitwalia ardhi za wakulima pembezoni hufanywa kwenye miji mikuu bila kuwashirikisha wakulima wamiliki ambao ndiyo wahanga wa uporaji huo.
 
Jarida la The African Report, limefichua dili la serikali la kuimilikisha ardhi yenye ukubwa wa hekari zaidi ya 300,000 kwenye Bonde la Mto Rufiji lililoko mkoani Pwani kwa kampuni ya Muasia wa Bangalore inayojulikana kama Karutari Global.
Jarida hilo limeripoti kuwa mwekezaji huyo anatarajiwa kujipatia hekari hizo iwapo mipango hiyo inayojadiliwa itakwenda vizuri.
Kadhalika jarida linasema Tanzania inaongoza barani Afrika eneo la Kusini mwa Jangwa Sahara kwa kumilikisha kiasi kikubwa cha ardhi yake kwa wawekezaji wa kigeni na kwamba hadi sasa imetoa hekari zaidi ya milioni moja za maeneo yenye rutuba kwa wawekezaji wa nje.
Habari za kuuza ardhi ya Afrika zimechapishwa kwenye jarida hilo toleo namba 41 la Julai 2012, lenye kichwa cha habari toleo maalumu "Namna wanasiasa walivyoachia Dola bilioni 100 za ardhi. Taarifa maalumu ya uchunguzi wa siri ya dili anayotishia mamilioni ya wakulima wa Afrika."
Ripoti maalumu iliyochapishwa kurasa za 23 na 24 za jarida hilo inaitaja Tanzania kuwa imeuza hekari 1,083,000 za ardhi kuanzia mwaka 2006 na kuanika kuwa watuhumiwa wa ufisadi huo wa ardhi ni wanasiasa na viongozi wa serikali ambao hugawa ardhi ya taifa kwa wageni kwa kuingia ubia na wageni .
"Wakati mwingine wanajichukulia ardhi bila kufuata taratibu na sheria zilizopo. Huwahonga viongozi wa vijiji na kuwashinikiza kuitisha mikutano ya haraka inayowezesha kutimiza azma hizo," jarida hilo likimkariri Barnaba Baha wa asasi ya kimataifa ya Action Aid.
Ripoti inasema kwenye bonde la Mto Rufiji mpango wa kuuza zaidi ya hekari 300,000 unaendelea na kuitaja kampuni ya India ya Karutari Global iliyowekeza nchini Ethiopia kuwa ndiyo inayokusudiwa kupewa eneo hilo.
Jarida linaeleza kuwa Karutari Global ni kampuni ya Bangalore inayomilikiwa na Muasia Sai Ramakrishna Karutari aliyeelezwa kuwa ni mmiliki wa majumba ya kuendesha kilimo (green house) yanayozalisha miche zaidi ya milioni 650 za maua ya rozi kila mwaka .
Jarida linawakariri wasemaji wa Benki ya Dunia (WB) wakishangaa uuzaji huo wa ardhi kwa kile wanachokiita ni dili dhidi ya maili za mraba milioni 1.5 za ardhi ambazo hazijaguswa lakini sasa zinatolewa kwa wawekezaji wa kigeni na tawala za Kiafrika.
Watafiti wanaeleza kuwa uporaji huu wa ardhi ni aina nyingine ya kugombea Afrika kama ule uliofanyika mwaka 1885 baada ya mkutano wa Berlin ulioigawa Afrika kwa wakoloni ambapo Tanganyika ( sasa Tanzania ) ilichukuliwa na Wajerumani
.
Mtafiti kutoka Ethiopia akizungumzia kiama cha wakulima wa Afrika alikaririwa na jarida hilo: "Ninasema kinachotokea barani Afrika ni kuigombea Afrika lakini kwa hili la sasa ni serikali zenyewe kupora ardhi za watu wake na kuwazawadia wawekezaji."
Kama kawaida jarida hilo linaeleza kuwa viongozi wa Afrika wameendelea kuimbiwa nyimbo za hadaa kuwa uwekezaji utaleta ajira kwa vijana, utaboresha teknolojia ya kilimo na kuongeza uzalishaji utaokaopunguza umaskini.
Habari hizo zinaitaja Tanzania, Kenya, Zambia, Uganda, Kongo , Ethiopia, Mali, Msumbiji na Liberia kuwa zinaonyesha sura ya serikali za Afrika zinavyojizatiti kuvutia mitaji ya nje kwenye sekta ya kilimo.
Hata hivyo jarida linaeleza kuwa cha kushangaza mipango ya kujitwalia ardhi za wakulima pembezoni hufanywa kwenye miji mikuu bila kuwashirikisha wakulima wamiliki ambao ndiyo wahanga wa uporaji huo.

Hivi Mhe.Mdee siyo member humu Jf mwenye ufahamu atujuze!

Hotuba yake 2014/2015 iwe pana zaidi na iguse maeneo mengi ya Nchi hii maana ardhi nyingi iko mikononi mwa Wakoloni Mambo leo/Makampuni Mfu .
Makampuni majina tu! Yamejazana pale Brela na TIC na hayajafanya Biashara hata ya Dola moja lakini yanamiliki maelfu ya Ekari na yanatumia ardhi hiyo hiyo waliyonyang'anywa/porwa watanzania na mbaya wanachukua Mikopo kwenye Benki zetu au hata za Ulaya dhamana ikiwa ni Ardhi ile ile na mara nyingi wengi wao wanapeleka pesa hizo Ulaya au Nchi Nyingi kama Mtaji kwa Shughuli tofauti kabisa!

Nimefurahi sana kusikia kuwa Hotuba ijayo ya Kambi ya Upinzani itarejea na Majina na kiasi cha ardhi iko mikononi mwa Mafisadi wa Ardhi Tanzania.

Na mimi napendekeza Upinzani uwekeze kiasi cha Bajeti yake kufanya Utafiti Nchi Nzima kwenye suala hili la Ardhi ili Bajeti na Uchaguzi wa Serikali ya Mitaa 2015 pamoja na Suala ya Katiba hoja kuu iwe Ufisadi wa Ardhi.
Pamoja na kunufaika kisiasa lakini itatusaidia kuondokana yaliyoikuta Zimbwabwe.

CC Kurugenzi ya Habari

Back
Top Bottom