Tanzania (Kilimanjaro Stars) vs Zimbabwe

Baada ya hii mechi, wachezaji wote wa Kili Staz na Makocha wao inabidi wastafishwe mechi za kimataifa kwa manufaa ya Umma.

sure mkuu inauma sana watawalaum watu kwa kukosa uzalendo haiwezekani kila mechi ya stars mtu unakwenda uwanjani kupata machungu kamavile umelazimishwa lakini ulikwena kwa kupenda mwenyewe na ukalipa pesa ya mlangoni
 
stars sijui wamekula nini. yaani hawakabi kabisa. inaonesha hawana mazoezi yaani kwa ufupi hawapo fit kimazoezi na kimchezo. wengi wa mashabiki wanashangilia zimbabwe. mia
 
Tanzania tuna mikoa zaidi ya 25 tunashindwa kupata vijana 11 bora wa kutengeneza Timu ya Taifa! inasikitisha kwakweli.
 
nurdin bakar anapasha. ikiingia anaweza badilisha mchezo. said maulid,thomas ulimwengu na mrisho ngasa pale mbele hawaelewani kabisa. refa anatubeba lakini hatubebeki. timu ikitolewa msilalamike. walistahili. mia
 
Very poor football from our very poor national team. No pace, no power and no determination. Kuna mashabiki uwanjani nimeona wanashangilia rangi za jezi za Zimbo, hadi mtangazaji wa SS9 anashangaa. Hii beki nadhani imechaguliwa kiswahiba manake hapa bongo kuna mabeki wazuri tu wangetuondolea hii aibu. Uswahiba kauanzisha JK umeenda hadi kwa makocha. Tuombe Mungu ibakie 2 : 0 hadi mwisho
 
wachezaji wetu wamekuwa kama wa somalia. wana anguka anguka. pengo la samatha linaonekana.
 
Duh! Naamini sasa,nway me nishajitoa huko taifa starz kitambo,nilijua tutatolewa lakini sio mapema hvi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom