Tanzania Kili music Awards (TKMA) 2011 - In pictures

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
37.jpg

Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo,Dr. Emmanuel Nchimbi akikabidhi tuzo ya heshima kwa Shirika la Utangazaji la Habari Tanzania (TBC) kwa Joe Lugalabamu.

35.jpg

Mwanamitindo Khadija Mwanamboka (kushoto) pamoja na Producer Pancho Latino (wa pili kulia) wakimkabidhi tuzo ya Msanii Mpya anaechipukia Linnah ambaye pia alijinyakulia tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kike.

9.jpg

Wachezaji wa Soka nchini,Juma Kasseja (kushoto) na Shadrack Nsajigwa (kulia) wakimkabidhi tuzo tuzo ya Wimbo Bora wa Taarab Mzee Yussuf.

40.jpg

Mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma, Said Mabele akitoa shukrani kwa wapenzi wa Muziki wa dansi na waandaaji wa Tuzo hizo muda mfupi baada ya kukabidhiwa tuzo ya Heshima.

16.jpg

Mzee Small Ngamba na Bi. Chau wakikabidhi tuzo kwa Producer Man Water mwakilishi wa 20% ambaye alijinyakulia tuzo 5 (tano),katika mchakato huo.

20.jpg

Msanii kutoka THT, Elius Barnaba (kulia), akikabidhiwa tuzo ya Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba.

33.jpg

Joe Makini akijinyakulia tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop.

22.jpg

Cpwaa akitoa shukrani za dhati kwa mashabiki wake walio mpigia kura na kuweza kupata tuzo ya Video Bora ya Muziki.

14.jpg

Mbungu wa Viti Maalum CCM, Mh. Vicky Kamata (kushoto), akimkabidhi tuzo ya Wimbo Bora wa R&B , Ben Poul.

7.jpg

Msanii wa vichekesho toka kundi la Orijinal Komedi, ambaye pia ni Mwanamuziki akitoa shukrani zake kwa mashabiki wake mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya Wimbo Bora wa Asili Tanzania.

13.jpg

Lady Jay Dee akiwa ameshikilia tuzo mbili alizojishindia, za Wimbo Bora wa Afrika Mashariki na Msanii Bora wa Kike.

8.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa Prime Time, Juhayna Kussaga pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja wakimkabidhi tuzo ya Mtunzi Bora Man Water kwa niaba ya 20 %.

3.jpg

Antonio Nugaz,Ruben Ndege pamoja na Dataz katika pozi.

43.jpg

Banana Zorro, Diamond na Ali Kiba wakitoa shoo ya pamoja

13.jpg

Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo,Dr. Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa BASATA,Ghonche Matelego wakifatilia kwa makini shughuli ya utoaji Tuzo.


26.jpg

Rais wa RBP,Mama Rahma Al Kharous pia alikuwepo kushuhudia tuzo hizo.
 
Sasa hivi mpoki ana wimbo gani wa asili hadi apewe tuzo?Yuko wapi mrisho mpoto!Cpwa kwa video sawa!!20% kupata tuzo 5 nooooo!labda 2 tu
 
Sasa hivi mpoki ana wimbo gani wa asili hadi apewe tuzo?Yuko wapi mrisho mpoto!Cpwa kwa video sawa!!20% kupata tuzo 5 nooooo!labda 2 tu
......kijana ukiwa MNAFIKI ukizeeka utakuwa MCHAWI
 
lady jaydee aache ubinafsi. ajiulize wasanii wote waliokuwa ukumbini walipewa mwaliko au yy ni bora zaidi ya wote waliohudhuria TKMA 2011. anachefuaaaaaaaa
 
lady jaydee aache ubinafsi. ajiulize wasanii wote waliokuwa ukumbini walipewa mwaliko au yy ni bora zaidi ya wote waliohudhuria TKMA 2011. anachefuaaaaaaaa

Poeples nyingine bana..sasa unataka JD afanye kama wengine wafanyavyo? she has a right to do as she pleases bila kuwafikiria hao wengine...remember..ni wajibu wa kila mtu kuamua thamani yake. If you sell yourself cheap..its you. ......ndo maana unaweza kunywa ndovu kwa 2000 uswahilini..ukienda holiday inn ukainywa kwa 5000! bia ile ile....
 
huyo nchimbi moustach kama pusi! hivi mkewe hamshauri kuwa style yake ya kilongtime!!!???
 
......kijana ukiwa MNAFIKI ukizeeka utakuwa MCHAWI
.......Ungekuwa sio MNAFIKI ungejibu swali/hoja,kwa mtindo huu bora hata atakayefika uzeeni kuliko asiyefika....kama unawapenda sana,bora upende hata paka!!!!
 
Wasema chochcote wa shughuli ya kili music awards juzi...

TONZO.jpg

Angalau CPWAA anaonekana mtu.Tuzo kam hizi zinatokea mara moja sana.Kwa nini nominee usivae japo suti kwa tukio muhimu kama hili??Unakuja hovyo hovyo tu kama umekurupushwa geto!!Hata kaseja na nsajigwa wanawashinda hawa watu.Hakuna tofauti na chokoraa ukiwaangalia wasanii wengine hapo.Tujirekebishe walau kwa masaa machache hayo.Duu
 
Back
Top Bottom