Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Salaam!
Ninapoangalia kina,uzito na uhatari wa kile kinachoendelea huko Japan kufuatia tetemeko kubwa la ardhi ambalo lilifuatiwa na Tsunami ninajikuta napata pendekezo linalohitaji ujasiri wa kiuongozi, maono ya mbali na kujali utu wa mwanadamu kwa kiwango cha pekee kabisa.
Tanzania imekuwa mpokeaji mkubwa wa misaada kutoka Japan tangu wakati wa Uhuru. Tumepokea kila aina ya misaada na ukiondoa misaada ya kifedha, ufundi na sayansi vijana wetu wengi wamepata nafasi ya kwenda kusoma huko chini ya mipango ya makubaliano kati ya nchi nzetu mbili. Usishangae kukuta kwa mfano madaktari wetu wengi wa wanyama wamesomea huko na wataalam wetu wa mambo mengine mengi pia wamesomea huko. Ni chini ya mwezi mmoja tu uliopita ambapo serikali ya Japan ilitoa msaada ya karibu shilingi bilioni 7.3 kwa ajili ya kusaidia masuala ya chakula kwa nchi yetu. Na ilikuwa mapema mwezi huu ambapo serikali hiyo hiyo ilitoa msaada wa shilingi milioni 462 kwa taasisi kadhaa za elimu nchini. Hata hivyo sitaki kuelezea historia na kina cha misaada kwani mingi inafahamika na inaweza kufahamika kwa mtu kufanya kautafiti kadogo tu.
Hata hivyo katika saa hii ya giza, ambapo wananchi wa Japan wamepatwa na baa kubwa kuliko yote yaliyowahi kutoka katika historia yao ni wazi kuwa mahitaji yao kama binadamu yanazidi sana uwezo wao wa kiteknolojia. Ni mahitaji ya kuonesha watu wanajali, wanawapenda na wanawashukuru kwa mema mengi ambayo wameyafanya kwa mataifa mengine tangu kuisha kwa vita ya pili ya dunia.
Ni kwa sababu hiyo, ninaamini serikali yetu iamue kwa dhati kurudisha wema wa watu wa Japan kwa kurudisha misaada hiyo michache ambayo imetolewa na kusitisha mpango wowote wa mikataba na nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo kama kitu kidogo ambacho wananchi wa Tanzania wanaweza kuwasaidia ndugu zao wa Japan wanapoinuka kutoka katika msiba mkubwa wa kihistoria.
Kwa kufanya hivyo nina uhakika watawala wetu wataweza kubuni njia nyingine za kufidia upungufu wowote utakaojitokeza ikiwemo usimamizi mzuri wa fedha zetu wenyewe, kuchukua mikopo toka taasisi ya ndani na kufanya jitihada ya haraka kurudisha fedha zilizofujwa kifisadi katika sehemu mbalimbali.
Siyo tu turudishe misaada ambayo Wajapan wameitoa kwetu hasa ile iliyokuwa itekelezwe kuanzia mwaka huu bali pia ile ambayo imetolewa kuanzia mwaka jana! Pendekezo hili ni kali lakini linawezekana. Lakini juu ya hilo napendekeza serikali yetu itoe si chini ya shilingi bilioni 20 kusaidia Japan kama fedha kutoka "Kwa watu wa Tanzania" kuonesha imani yetu kuwa taifa hilo rafiki litaweza kupita salama katika saa hii ya giza ambayo inabakia katika historia ikigubikwa na huzuni isiyo kifani.
Nakumbuka wakati wa janga la Haiti nilitoa pendekezo kama hili lakini halikufanyika aidha kwa sababu tumejiaminisha katika ubinafsi wetu kuwa sisi "tutapokea tu na hatutoi kamwe" au ni kwa sababu tumedekezwa mno katika mahitaji yetu kiasi kwamba hatuwezi kuona mahitaji mazito ya watu wengine. Ndugu zangu, Taifa lisilotoa halibarikiwi! - kanuni ya utoaji inayohusu binadamu inahusu vile vile mataifa!
Ninaomba, tufanye kitu ambacho hakitoki katika umaskini wa vitu vyetu au hali zetu kama taifa bali kinatoka katika utajiri wa tunu za wema wetu kama binadamu.
I know... I'm just fantasizing about greatness of our people.... kama tungekuwa na viongozi wenye uwezo wa kuona ukuu huo.
Napendekeza.