Tanzania: Inflation rate hits 19.2%

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,601
8,741
Tanzania's year-on-year inflation rate rose for the 13th straight month to 19.2 per cent in November from 17.9 per cent in October, the National Bureau of Statistics (NBS) said on Friday.

Food and fuel price rises have been driving the year-on-year inflation rate higher in east Africa's second-largest economy, with no sign of respite.

"The annual headline inflation rate for the year ended November 2011 has further increased to 19.2 per cent compared to 17.9 per cent registered in the year ended October 2011," NBS said in a statement.

"Again, the food and non-alcoholic beverages inflation rate has increased to 26.1 per cent in November 2011 from 24 per cent recorded in the year ended October 2011."

Food and non-alcoholic beverages have a 47.8 per cent weighting in the country's basket of goods used to measure inflation.

Among food prices that increased were the national staple maize, rice, bread, wheat flour, cassava, meat, oil, Irish potatoes, sweet potatoes and sugar.

NBS said the year-on-year inflation rate for energy rose to 39.2 per cent in November from 37.4 per cent in October.

Stripping out food and energy prices, the annual inflation rate edged up to 8.8 per cent in November from 8.5 per cent in October.

On a monthly basis, consumer prices rose 1.4 per cent in November from October.
 
WAKATI mwaka 2011 ukielekea ukingoni, hali ya uchumi nchini imezidi kuwa tetereka huku mfumuko wa bei ukipaa na kufikia asilimia 19.2, ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.4 kutoka 17.9 wa Oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NAO kuhusu mwenendo wa bei za bidhaa na huduma mbalimbali nchini, mfumuko huo umepanda ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tu.

Taarifa hiyo imetaja baadhi ya mambo yaliyochangia ongezeko hilo kuwa ni pamoja na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali za vyakula na bidhaa zingine.

“Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kumechangiwa hasa na kuongezeka bei za bidhaa mbalimbali za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo ya NAO iliyosainiwa na Mkurugenzi wake Mkuu, Dk Albina Chuwa.

Baadhi ya bidhaa za vyakula ambavyo kwa mujibu wa taarifa hiyo vimechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la mfumuko wa bei, ni pamoja na mchele ambao katika kipindi cha mwezi mmoja, umeongezeka bei kwa asilimia 8.8, mihogo asilimia 5.8, ndizi za kupika asilimia 5.0.

Vyakula vingine ni pamoja na viazi vitamu ambavyo vimepanda bei kwa asilimia 4.9, unga wa muhogo na nyama asilimia 4.8 kila moja, mapapai asilimia 4.0, unga wa ngano asilimia 3.7, unga wa mahindi asilimia 1.7, karanga asilimia 2.6, sukari asilimia 2.5 na mafuta ya kupikia asilimia 2.0 Bidhaa zisizo za vyakula ambazo pia zimeongezeka bei katika kipindi cha mwezi mmoja na kuchangia mfumuko wa bei ni pamoja na vifaa vya nyumbani, baiskeli, betri za magari, nyumba za kulala wageni na gharama za kusaga nafaka.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Oktoba hadi Novemba mwaka huu, bidhaa zote hizo zimepanda bei kwa asilimia kati ya 1.3 na 3.3

Mfumuko wa bei za nishati mbalimbali kwa mujibu wa NAO, umeongezeka kwa asilimia 1.8 kutoka asilimia 37.4 kwa mwaka ulioishia Oktoba 2011, hadi asilimia 39.2 kufikia Novemba mwaka huu.

Sambamba na mfumuko wa bei wa Taifa , fahirisi za bei za Taifa (kipimo cha mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotumiwa na jamii), zimeongezeka kutoka asilimia 100.20 Novemba 2010, na kufikia asilimia 119.41 Novemba, 2011.

Kwa upande wa nchini zingine za Afrika Mashariki , Kenya na Uganda nazo zinakabiliwa na tatizo kubwa la mfumuko wa bei .Nchini Kenya katika kipindi cha mwaka ulioishia Novemba 2011, mfumuko wa bei umeongezeka hadi kufikia asilimia 19.7 Novemba 2011 kutoka asilimia 18.9 Oktoba mwaka huu, wakati Uganda mfumuko umepungua kutoka asilimia 30.4 Oktoba na kufikia asilimia 29.0 Novemba mwaka huu.
 
ni maokeo ya sera na mipango mibaya ya serikali kutokuwa na mkakati madhubuti wa kupambana na hii hali. tutegemee mfumuko zaidi hasa ukizingatia kuwa bei za vyakula zitapanda zaidi kwa hakuna mavuna y amaana yanayotegemewa kabla ya mwezi july mwaka ujao.
'SERIKALI YA JK IMEDHUBUTU IMEWEZA NA INASONGA MBELE NA INFLATION " ili kuwaletea maisha bora kwa kila Mtz.
 
Tunapelekwa wapi jamani? NImeona analysis ya Waziri Kivuli wa fedha (Zitto) kuwa tangu baada ya bajeti, mdumko wa bei umesababisha nakisi ya asilimia 6 kwenye majeti. Hivi Mkullo na wenzake wana mipango gani ya kufidia pengo hili maana sioni dalili za kubana/kukata matumizi serikalini
 
=PRESS RELEASE=


Uchumi wa Taifa hatarini: Mfumuko wa Bei tishio kwa Serikali, Wafanyabishara na Wananchi.

Mfumuko wa Bei umezidi kuongezeka kama taarifa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu inavyoonesha kwamba, wakati mfumuko wa bei mwezi Julai mwaka huu (Bajeti ya mwaka wa Fedha 2011/2012 ilipokuwa inaanza) ulikuwa asilimia 13, umefikia asilimia 19.2 mwezi Novemba. Hii maana yake ni kwamba, Bajeti ya Serikali iliyopitishwa na Bunge mwezi Juni 2011, imepunguza uwezo wa kununua bidhaa na huduma kwa takribani asilimia 6. Hii ni sawa na shilingi 780 bilioni kuyeyuka katika Bajeti katika kipindi cha miezi Minne tu ya utekelezaji wa wake. Kutokana na kasi ya ukuaji wa Mfumuko wa Bei ni dhahiri kwamba, itakapofika mwisho wa mwaka wa Bajeti Serikali itakuwa imepoteza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kununua bidhaa na huduma kwa zaidi ya robo ya Bajeti yake.

Hali ni mbaya zaidi kwa wananchi kwani Mfumuko wa Bei za vyakula umekua kwa kasi kikubwa mno. Ofisi ya Takwimu imeonesha kuwa wakati mfumuko wa Bei za vyakula ulikuwa asilimia 14.8 mwezi Julai, umefikia asilimia 24.7 mwezi Novemba 2011. Ukilinganisha na bei za vyakula mwaka 2010, mwananchi amepoteza uwezo wa kununua chakula kwa zaidi ya robo katika ya Novemba 2010 na Novemba 2011. Jumla ya vyakula ambavyo mwananchi alinunua kwa shilingi 10,000 mwaka 2010, sasa atanunua kiwango kile kile kwa shilingi 12,500. Bei za vyakula zimeongezeka kwa kiwango hiki ilhali kipato cha mwananchi aghalabu kipo pale pale. Mwathirika mkubwa ni mwananchi wa kawaida wa kijijini ambaye mapato yake ni kidogo na hivyo sehemu kubwa huyatumia kununua chakula.

Ukiangalia kwa undani utakuta mfumuko wa bei wa bidhaa kama mchele, sukari, nyama na samaki umekua maradufu. Bei ya mchele imekua kwa asilimia 50, sukari asilimia 50, nyama asilimia 30 na Samaki kwa takribani asilimia 40. Bidhaa hizi zote ni muhimu sana kwa afya ya binadaamu na hasa watoto kwa upande wa vyakula vya protini. Tusipokuwa makini na kupata majibu sahihi ya tatizo la mfumuko wa bei za vyakula, wananchi wengi na hasa watoto watapata utapiamlo na Taifa kuingia gharama kubwa katika kuwapatia huduma ya afya.

Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula, mfumuko wa bei wa mafuta ya taa na gesi asilia unapaa kwa kasi kama moto wa nyikani. Wakati mafuta ya taa yamepanda bei kwa asilimia 71 katika ya mwezi Novemba mwaka 2010 na mwezi Novemba 2011, bei ya gesi asilia imepanda kwa asilimia 35. Madhara ya hali hii ni makubwa mno maana wananchi watakimbilia kwenye matumizi ya mkaa na kuni, hata hivyo bei za mkaa zenyewe zimepanda kwa asilimia 24. Kwa hali hii, na kutokana na ukweli kwamba wananchi wengi wa Tanzania wapo kwenye mpaka wa umasikini na daraja la kati chini, juhudi za muongo mzima za kupunguza umasikini zitafutwa ndani ya mwaka mmoja tu.

Mfumuko wa Bei unasukuma Watanzania wengi zaidi kwenye dimbwi la umasikini, unapunguza uwezo wa Serikali kutoa huduma za jamii kupitia Bajeti na hata kutimiza mipango ya miradi ya maendeleo kama miundombinu ya barabara, umeme, bomba la gesi, madaraja nk. Mkakati mahususi unatakiwa kubadili hali hii. Hatua zifuatazo zinapendekezwa ili kuuhami uchumi na kupunguza upandaji wa kasi wa gharama za maisha.

1. Kuongeza uzalishaji wa chakula kwa kuweka mbinu za kukuza uchumi wa vijijini ni njia mojawapo endelevu ya kupunguza mfumuko wa Bei hapa nchini. Serikali sasa iache maneno matupu kuhusu sekta ya uchumi vijijini kwa kuelekeza nguvu nyingi huko. Serikali iruhusu na ivutie kwa kasi na kutoa vivutio kwa wazalishaji binafsi wa Sukari na mpunga katika mabonde makubwa. Waziri wa Kilimo na Maafisa wake watoke Ofisini na kuhimiza uzalishaji mashambani, fedha zielekezwe kujenga miundombinu ya barabara vijijini.

Vyakula vilivyolundikana mikoa ya Mbeya, Iringa na Rukwa ambapo Serikali iliahidi kununua na kutotimiza ahadi yake vinunuliwe mara moja na kusambazwa mikoa yenye shida ya chakula kama Mwanza, Mara, Kagera na mikoa ya Kaskazini. Chakula kukuta msimu mwingine katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ni kashfa kubwa kwa Serikali na inaonesha Serikali isivyokuwa makini na maisha ya wananchi.

Wakati huu ambapo tunaweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa chakula, Serikali inunue chakula cha kutosha na hasa mchele na sukari kutoka nje na kukisambaza kwenye soko ili kupunguza upungufu wa bidhaa (scarcity) katika masoko.

Mfumo uliotumika kununua Sukari tani laki moja hivi karibuni usitumike tena kwani ulizaa rushwa ya hatari na ufisadi ambao haujaripotiwa kwenye kutoa vibali. Wizara ya Kilimo iruhusu wauzaji kutoka nje walete sukari nchini moja kwa moja na kununuliwa na Bodi ya Sukari kisha kuiuza kwa wauzaji wa Jumla. Mfumo wa kutoa vibali umeonesha kutokuwa na tija na kwa kweli kunufaisha maafisa wachache wa Wizara ya Kilimo na Bodi ya Sukari.

2. Kitengenezwe kiwanda cha kutengeneza gesi ya matumizi nyumbani (LPG extraction plant) kwa haraka ili kupunguza bei ya gesi, kuepuka kuagiza gesi kutoka nje na hivyo kuokoa fedha za kigeni na kutengeneza ajira hapa nchini. Kupanda kwa bei ya gesi asilia kunatokana na kwamba Tanzania inaagiza gesi hii yote kutoka nje ilhali malighafi ya kutengeneza gesi ipo hapa Tanzania na kwa kweli huchomwa moto (flared). Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini liingie ubia na kampuni Binafsi ili kuwekeza katika kiwanda cha kuzalisha gesi hatimaye kushusha bei na hivyo kuwezesha wananchi wengi zaidi kutumia gesi kwa matumizi ya kupikia n.k, hivyo kutunza mazingira.

3. Ushuru wote unaokusanywa kwenye Mafuta ya Taa upelekwe Wakala wa Nishati Vijijini ili kufidia kupanda kwa bei ya mafuta ya Taa. Mfumuko wa Bei katika bidhaa ya mafuta ya taa unatokana na uamuzi wa kuwianisha bei ya mafuta ya taa na diseli ili kuondoa tatizo la uchakachuaji wa mafuta. Tatizo limeondoka (au hatulisikii tena) lakini wananchi wanaumia sana. Uamuzi sahihi wa kisera ni kupanua huduma za umeme vijijini kwa kuipa fedha zinazotokana na ushuru wa mafuta ya taa Wakala wa Umeme Vijijini. Usambazaji wa Umeme Vijijini utaongeza shughuli za kiuchumi vijijini, kukuza uchumi wa vijijini, kuongeza mapato ya wananchi kwa kuongeza thamani za mazao yao na hivyo kupunguza athari za mfumuko wa bei.

4. Sera ya Matumizi ya Serikali iangaliwe upya kwa kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi yasiyo ya lazima, na kuelekeza fedha nyingi zaidi katika uwekezaji umma (public investments). Matumizi Mengineyo ya Serikali yanaongeza fedha kwenye mzunguko ama kwa kulipa watu wachache stahili mbalimbali kama posho n.k au kwa kununua bidhaa na huduma bila mpango, na hivyo kusukuma bei kuwa juu kinyume na uhalisia wa soko. Tafiti za mfumuko wa Bei Tanzania zinaonyesha kwamba sera za fedha na zile za matumizi (monetary and fiscal policy) zina nafasi kubwa katika kukuza mfumuko wa bei. Hivi sasa nakisi ya Bajeti inayopelekea Serikali kukopa kwa kwa kiwango kubwa inapandisha gharama za viwanda kukopa mitaji ya muda mfupi na hivyo kuongeza gharama za uzalishaji na kasha bei za bidhaa. Wizara ya Fedha ambayo mpaka sasa imekaa kama imeishiwa namna ya kufanya, inapaswa kuamka na kutoa maelekezo mapya kwa Wizara, Idara na Wakala za Serikali kuhusu namna ya kubana matumizi na kuziba mianya yote ya kukwepa kodi.

Hitimisho
Serikali imeonesha udhaifu mkubwa sana katika kusimamia uchumi katika nusu ya kwanza ya Bajeti ya mwaka 2011/2012 ambayo pia ni Bajeti ya kwanza ya kipindi cha pili cha Serikali ya awamu wa Nne. Kuna hatari ya dhahiri kwamba ifikapo mwezi Januari 2012 tutakuwa tumerejea mfumuko wa Bei wa kiwango cha mwaka 1992 (21.9%). Tusipochukua hatua za haraka tutafikia na hata kuzidi mfumuko wa Bei kiwango cha juu kabisa ambacho kilifikiwa mwaka 1994 (33%) na hivyo viwanda kushindwa kukopa kwenye Mabenki kwa mahitaji yao ya haraka ya mitaji ya muda mfupi, wazalishaji wadogo kushindwa kulipa mikopo yao kwenye Taasisi za fedha na hivyo kufunga uzalishaji, Shirika la Umeme kushindwa kabisa kulipa gharama za mafuta ya kuendesha mitambo na kipato cha mwananchi kutomudu gharama za za kila siku. Uchumi utadorora kabisa. Taifa litakuwa hatarini.

Wizara ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania na Wizara ya Kilimo na Chakula iamke kuhami uchumi dhidi ya adui namba moja, Mfumuko wa Bei. Huu sio wakati wa kupiga porojo, viongozi wafanye kazi zao, Wananchi wajitume.

Inabidi sasa turejee kauli mbiu za miaka 50 iliyopita za Uhuru ni Kazi. Tuseme Demokrasia ni Kazi. Demokrasia sio lelemama.

Ndg. Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli Fedha na Uchumi
18 Disemba 2011

MN, naona hukuipandisha jukwaani. Nimeiambatanisha toka kwa ZK
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zuberi Zitto Kabwe ameishukia serikali kwa kuonesha udhaifu katika kuinua uchumi wa nchi na kutoa ushauri kwa Serikali ya CCM.
 
Hawa mapapa wanaona watu hawajui chochote kinachoendelea lakini nawaambia ya kwmb siku NGUVU YA UMMA watakapochafukwa na Mioyo,ndg zangu nawaambia ya kwmb hapatatosha hata kidogo wao wanaona raia ni lala lakini Mi ninachoweza kusema ni kwmb siku hazigandi na haina budi siku hiyo kufika penda usipende lakini itatokeaga tu! Tuombeni Uzima tu!

Zitto tupo pamoja A to Z shaka ondoa kama una cha ku2juza we angusha tu kwn raia kinachotugharimu ni elimu tu na unaona shule za KATA ilivyomzigo kwa wanafunzi wanaosoma humo wakati watoto wa mafisadi wote wako nje! Acha tu watuburuze watakavyo maana siku inakuja!
 
Tatizo kubwa linalotukumba nikuingiza siasa kwenye masuala ya msingi,hali ni tete jaman lakni serikal haion hata kidogo
 
Bila kulifanyia kazi suala la mafuta, tutakuwa tunajidanganya kila siku.
 
Hawa mapapa wanaona watu hawajui chochote kinachoendelea lakini nawaambia ya kwmb siku NGUVU YA UMMA watakapochafukwa na Mioyo,ndg zangu nawaambia ya kwmb hapatatosha hata kidogo wao wanaona raia ni lala lakini Mi ninachoweza kusema ni kwmb siku hazigandi na haina budi siku hiyo kufika penda usipende lakini itatokeaga tu! Tuombeni Uzima tu!

Zitto tupo pamoja A to Z shaka ondoa kama una cha ku2juza we angusha tu kwn raia kinachotugharimu ni elimu tu na unaona shule za KATA ilivyomzigo kwa wanafunzi wanaosoma humo wakati watoto wa mafisadi wote wako nje! Acha tu watuburuze watakavyo maana siku inakuja!
Mie nadhani Watanzania wanapenda "AMANI" na kwa hiyo kwao kuwa na uongozi "MBADALA" tofauti na wa Chichiemu ni kuhatarisha "amani" ya Tanzania.

Nadhani na nionavyo mimi bado tunakazi kubwa ya kuelimisha umma hasa vijana ili waweze kujua kuwa nchi ni ya kwao na kuwa mabaya yanayotendeka sasa yatakuja kuwagharimu wao baadaye watakapokuwa ndo wenye nchi. Vijana wa Tanzania, bado hawajaamka japo kuna dalili kidogo ya kuanza "kuamka" kutoka usingizini.

Kazi bado ipo. Lakini, naamini tutafika. Pole pole ya Kobe....!
 
Ok Baada ya kusoma nimegundua kuwa ni Zitto Kabwe, hakika ni mawazo mazuri sana Zitto, Niliandika kutokujua mchapaji lakini nimeona kuwa ni Kabwe; Sikujui wewe ni nani uliyeainisha utafiti huu juu ya hali ya uchumi hasa suala la Inflation, ila hakika umenigusa sana kwa kuwa maeneo yote uliyoyataja hata mimi huwa yananiumiza, gas, chakula, mafuta ya taa na bidha nyingine za viwandani.

Serikali kwanini haioni kuwa hili suala linawaumiza watu wake jamani, na tuna Think tank wakutosha kwa nini wasitumike kulinusuru taifa?
 
Tanzania's year-on-year inflation rate rose for the 13th straight month to 19.2 per cent in November from 17.9 per cent in October, the National Bureau of Statistics (NBS) said on Friday. Food and fuel price rises have been driving the year-on-year inflation rate higher in east Africa's second-largest economy, with no sign of respite. "The annual headline inflation rate for the year ended November 2011 has further increased to 19.2 per cent compared to 17.9 per cent registered in the year ended October 2011," NBS said in a statement. "Again, the food and non-alcoholic beverages inflation rate has increased to 26.1 per cent in November 2011 from 24 per cent recorded in the year ended October 2011." Food and non-alcoholic beverages have a 47.8 per cent weighting in the country's basket of goods used to measure inflation. Among food prices that increased were the national staple maize, rice, bread, wheat flour, cassava, meat, oil, Irish potatoes, sweet potatoes and sugar. NBS said the year-on-year inflation rate for energy rose to 39.2 per cent in November from 37.4 per cent in October. Stripping out food and energy prices, the annual inflation rate edged up to 8.8 per cent in November from 8.5 per cent in October. On a monthly basis, consumer prices rose 1.4 per cent in November from October.
hi yoooooooooooooooooba, tufilwe mnyambala!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom