Tanzania inayonifanya niwaombe msamaha wana JF

pole sana bwana masaka kama ndio umeyajua baada ya kumuona kelly amekwenda uko...ila sasa inabidi uanze kuwa mzalendo wa nchi yako kwa kutembelea sehemu nyingi zenye shida na hapo ndipo utakapozidi kukiona hicho chama unachokitetea kichungu.
 
pole sana bwana masaka kama ndio umeyajua baada ya kumuona kelly amekwenda uko...ila sasa inabidi uanze kuwa mzalendo wa nchi yako kwa kutembelea sehemu nyingi zenye shida na hapo ndipo utakapozidi kukiona hicho chama unachokitetea kichungu.

Naam, kuna umuhimu wa Masaka kutembea zaidi ili aifahamu hali halisi ya maisha ya Watanzania wengi ambayo ni ya dhiki kubwa.
 
Nashukuru kuwa umekubali makosa yako,kitu ambacho kinahitaji uajsiri sana,haswa kwa sisi watanzania.

Naamini kuwa Chama si tatizo, bali ni wale viongozi na vibweka vyao ndio wametumia chama kama mwanvuli wa kufanya uharamia wao.....hawa mimi nina waita ni majambazi ni maharamia ambao wameteka chama.

Kilichobaki, wewe ni kusaidia wanachama wenzako ambao bado ni wengi wasafi mkiokoe chama chenu.

BRAVO MASAKA.....hii ndio tunaita Utaifa kwanza and then Chama au Mke.

Ni kweli Mwanatanu, si lazima uikane CCM ndio uwe Mzalendo... Waweza kuwa kama akina Sendeka ndani ya CCM. Hivyo basi Kwa hili la Masaka nina Mashaka na wewe
 
Masaka umeanza kugundua heee!?

Ukifikiria hali kama hii ambayo inatokea Uwanja wa Fisi ambako si mbali toka ikulu, inatisha kufikiria nini kinaendelea kwingine kule wapiga picha wasikofika.
Inafikia wakati mambo kama haya yamguse hata Kikwete mwenyewe.
 
Ukifikiria hali kama hii ambayo inatokea Uwanja wa Fisi ambako si mbali toka ikulu, inatisha kufikiria nini kinaendelea kwingine kule wapiga picha wasikofika.
Inafikia wakati mambo kama haya yamguse hata Kikwete mwenyewe.

Does government operate using JF comments?!

Makahaba 63 Dar mbaroni

2008-06-21 21:24:43
Na Mwanaidi Swedi Jijini


Watu 63 wanaodhaniwa kuwa hufanya biashara chafu ya kujiuza miili yao almaarufu kama makahaba wamenaswa na polisi Jijini na kutiwa mbaroni, huku saba kati yao wakitajwa kuwa ni wanaume.

Watu hao wamekamatwa wakati polisi wakiendesha msako dhidi yao katika maeneo mbalimbali Jijini.

Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mark Kalunguyeye, amesema tukio hilo limetokea jana, majira ya saa 4:00 na saa 6:00 usiku huko Manzese Uzuri, Manzese Darajani na eneo maarufu kwa shughuli hiyo chafu la Manzese Uwanja wa Fisi.

Kamanda Kalunguyeye amesema kuwa makahaba hao ni wale ambao wanaishi kwenye nyumba zao kama watu wengine wa kawiada, lakini shughuli yao kubwa imebainika kuwa ni kujiuza miili yao.

Amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

Wakati huohuo, mwanamke mmoja aitwaye Anna Mkate, 28, amefariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi cha mchanga wakati akichimba kokoto.

Kamanda Kalunguyeye amesema tukio hilo limetokea jana katika eneo la Bunju A.

Amesema Kamanda Kalunguyeye kuwa mwanamke huyo amekutwa na umauti huo wakati akiwa kazini akichimba kokoto na wenzake wawili, ambao wao walinusurika.




Amesema kuwa ahdi sasa, mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mwananyamala.
  • SOURCE: Alasiri
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom