Tanzania inayonifanya niwaombe msamaha wana JF

Masaka... sikujua unaguswa na matatizo ya Tanzania. Ulipojitokeza kutetea CCM miye nilikuwa nahesabu muda tu kabla "mwanga wa ukweli" haujakuzukia. Inasikitisha kuona CCM inapoteza mtetezi mzuri kama wewe. Nina uhakika watakumiss.

Ila nakuomba usikate tamaa, jaribu kutetea unayoweza kwani mchango wako ni muhimu sana na ulileta balance ya pekee humu. Chonde chonde usiache kukitetea chama chako.

Mwanakijiji, nitaendelea kubakia mwana ccm ila kuna wakati naona inabidi kusema yale yanayoumiza moyo kama nilichoona hapa. Kimeniumiza sana moyo kwa kweli.
 
Usikate tamaa mapema namna hiyo.. Bado una nafasi kubwa ya kukikosoa chama chako ukiwa ndani ya chama hicho

kamanda, bado niko ccm na sidhani kama kuna yoyote anayefikiria kuwa wanaccm wote watapotea kama ukungu jua linapowaka. Wana ccm wataendelea kuwepo ila kuna wakati inafikia mambo kama haya yasemwe wazi na wana ccm maana sisi ndio tunaongoza nchi na inabidi tushughulikie matatizo ya wananchi pia.
 
naona hizo video zimeondolewa zote ktk youtube....au...

Fuata ile web link niliyoweka. Inaonekana ile picha inakuwa blocked ikitaka kufunguliwa independently. Fuata ile web link niliyoweka chini ya picha. Au nenda youtube na usearch hyena square
 
Sasa wale wasafi walijifunza usafi kutoka kwa nani? Na wale waishio kwenye mwanga nani aliwatoa gizani?

mmoja kati yao aliwafundisha kufanya usafi na kuwaonyesha namna ya kupata mwanga na baadaye wakaambukiza dunia nzima kuanzia kwa mafarao wa misri hadi kwa mayahudi wa silicon valley...
 
Masaka, kama alivyouliza KKN, ulikuwa hujui matatizo ya Tanzania, au ulikuwa unatetea CCM kama mimi ninavyotetea Pan Africa, au uliyajua matatizo lakini hukujua mengine yanasababishwa na uongozi mbovu wa Sisi em, au ulikuwa unatetea maslahi fulani, au, ulikuwa unataka kuleta changamoto jamvini tu?

Sidhani kama clip ya dakika 20 ya Uwanja wa Fisi, ambayo hata haitoshi kuanza kueleza matatizo ya Tanzania, ikawa ndio epiphany kwako.

Nisaidie kuelewa kwa nini nisiseme ulikuwa una feki mawazo yako, una intellectual dishonesty.

Ahsante.
 
Kwa kweli inasikitisha sana hayo ndo maisha ya watanzania wengi!Yaani haihitaji kwenda chuo kikuu kungundua kuwa Tanzania tunaongozwa na mazezeta!yule binti katoa maoni mazuri sana!
 
Nimesoma ile habari ya michuzi kuhusu ziara ya Kelly Rowland uwanja wa fisi, kufuatilia comments za watu nikakuta link kwenda youtube kuona documentary kuhusu maisha ya uwanja wa fisi - inaitwa hyena square.

Kwa dakika 30 zilizopita nimekuwa naona hii picha huku machozi yakinitoka pwacha pwacha. Hali hii imenitisha na kuniogopesha kuhusu mwelekeo wa nchi yetu. Inaumiza kuwa wengine tunaishi maisha ya kula na kusaza huku wenzetu wakipitia maisha kama ya dada Eliza aliyotajwa kwenye hiyo movie.

Kama haya yanatokea Tanzania na mimi sikuyajua, sijui ni mengi kiasi gani ambayo siyajui. Hapana, hii imepita kipimo, kama hii haivunji moyo basi sijui nini tena kitabadili mwelekeo. Siwezi sasa kuendelea kuishi maisha mazuri wakati wengine wakiishi jehanam kama haya. Kama haya yanatokea Tandale ambako ni KM chache tu toka magogoni, sijui yanayotokea Iringa ni makubwa kiasi gani.

Kwa kuona haya, nitakuwa najidanganya kuendelea kutetea chama changu cha ccm hapa mtandaoni kama haya yanatokea wakati wachache tu kwenye chama wakinufaika na pesa zote za Tanzania. Sitaki tena kuwatetea wana ccm hapa mpaka watakapoanza kushughulikia matatizo ya wananchi.

Nawaomba msamaha wana JF ambao niliwasumbua hapa wakati ambao nyie mnajaribu kupigana kwa hali na mali kuisaidia Tanzania itoke kwa mafisadi wachache ndani ya chama chetu.

Hebu one mwenyewe hii clip ya youtube..

[media]http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM[/media]

[media]http://www.youtube.com/watch?v=LfQ-tHqGMDc[/media]

Ahsante sana Masaka, karibu niangushe chozi kwa uliyoyaandika, machozi yananilengalenga. Mungu akujalie maisha marefu ili ushiriki kikamilifu katika kupamabana na mafisadi ndani ya nchi yetu.
 
Hey guys, this is interesting stuff! Can someone assist me. I wanna down load the videos and save them in my computer. Its good for show casing. Mama Mwaituka who is mentioned in this video is she the same Madam who has been living with HIV/AIDS for almost twenty years? She is doing great job in helping other young girls to get out of this plight

PM
 
Masaka, kama alivyouliza KKN, ulikuwa hujui matatizo ya Tanzania, au ulikuwa unatetea CCM kama mimi ninavyotetea Pan Africa, au uliyajua matatizo lakini hukujua mengine yanasababishwa na uongozi mbovu wa Sisi em, au ulikuwa unatetea maslahi fulani, au, ulikuwa unataka kuleta changamoto jamvini tu?

Sidhani kama clip ya dakika 20 ya Uwanja wa Fisi, ambayo hata haitoshi kuanza kueleza matatizo ya Tanzania, ikawa ndio epiphany kwako.

Nisaidie kuelewa kwa nini nisiseme ulikuwa una feki mawazo yako, una intellectual dishonesty.

Ahsante.

sema chochote utakachofikiri kuhusu mimi lakini sidhani kama kitamsaidia Eliza au watoto wengine walionekana kwenye documentary au ambao hatujui saa hiii wanapitia nini katika maisha yao ya kila siku Tanzania.

Wakati mwingine picha moja tu (kama ile ya mtoto wa kivietnam anayekimbia mabomu ya kimarekani akiwa uchi na kulia kwa uchungu) inaweza kubadili mtazamo wote wa jamii nzima kuhusu suala fulani.

Endelea na ubishi wako wa kisomi ambao mpaka leo hii na mimi nilikuwa naufanya bila kugundua kuwa ubishi wa kisomi hauleti suluhisho lolote la matatizo. Kwa ubishi huu unaotaka kuuanzisha labda kwa nia ya kubadili mwelekeo wa thread hii, jua kuwa utabishana na wengine lakini sio mimi.

Asante.
 
NI kama ile video ya mapanki Darwin's Nightmare!ambayo wabunge waliijadili na wengine wakadai Hubert Supper akamatwe.Wakati yalionyeshwa maisha halisi ya mtanzania wa hali ya chini na watu wanavyokula mapanki huku minofu ikipelekwa ulaya!Masaka unahitaji kuangalia hiyo video pia!
 
Nimesoma ile habari ya michuzi kuhusu ziara ya Kelly Rowland uwanja wa fisi, kufuatilia comments za watu nikakuta link kwenda youtube kuona documentary kuhusu maisha ya uwanja wa fisi - inaitwa hyena square.

Kwa dakika 30 zilizopita nimekuwa naona hii picha huku machozi yakinitoka pwacha pwacha. Hali hii imenitisha na kuniogopesha kuhusu mwelekeo wa nchi yetu. Inaumiza kuwa wengine tunaishi maisha ya kula na kusaza huku wenzetu wakipitia maisha kama ya dada Eliza aliyotajwa kwenye hiyo movie.

Kama haya yanatokea Tanzania na mimi sikuyajua, sijui ni mengi kiasi gani ambayo siyajui. Hapana, hii imepita kipimo, kama hii haivunji moyo basi sijui nini tena kitabadili mwelekeo. Siwezi sasa kuendelea kuishi maisha mazuri wakati wengine wakiishi jehanam kama haya. Kama haya yanatokea Tandale ambako ni KM chache tu toka magogoni, sijui yanayotokea Iringa ni makubwa kiasi gani.

Kwa kuona haya, nitakuwa najidanganya kuendelea kutetea chama changu cha ccm hapa mtandaoni kama haya yanatokea wakati wachache tu kwenye chama wakinufaika na pesa zote za Tanzania. Sitaki tena kuwatetea wana ccm hapa mpaka watakapoanza kushughulikia matatizo ya wananchi.

Nawaomba msamaha wana JF ambao niliwasumbua hapa wakati ambao nyie mnajaribu kupigana kwa hali na mali kuisaidia Tanzania itoke kwa mafisadi wachache ndani ya chama chetu.

Hebu one mwenyewe hii clip ya youtube..

[media]http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM[/media]

[media]http://www.youtube.com/watch?v=LfQ-tHqGMDc[/media]

Watu tuko Ulaya na tunajua yanayoendelea Tanzania na ufedhuli wa CCM, wewe uko Dar unajifanya hukujua yanayoendelea hapo hapo Dar?

Kweli unahitaji Youtube ili kujua yanayoendelea hapo nchini?
 
JE ile video ya Darwin's Nightmare!nayo pia inaonyesha maisha ya mtanzania!Cha ajabu wabunge waliijadili wakidai ni uongo!Wakati ni ukweli mtupu.
 
Asiye funzwa na Mama yake basi Ulimwengu humfunza .Masaka kabla jogoo hajawika umekuwa Saulo na sasa Paulo .Niliyajua haya nikawa najiuliza kama akili yako ina akili .Nikajua ina akili ila unasumbuliwa na ulaji .

Kutuomyesha kwamba umejua ugumu wa CCM na Serikali na kuonyesha kwamba JF hatuna fitina wala majungu na viongozi ila tuinalia maumivu ya kweli basi ondoa lile bandiko lako la kuwa mpigania CCM ndiyo tukuelewe .Anza na hilo then uje kuniunga mkono kususia Vodacom.
 
Mwaka 2006 nilitembelea BONGO wakati mambo ikiwa mbaya sana kwa wananchi kwa ajili ya UKAME NA UMEME ULIOSHINIKIZWA NA UJAMBAZI WA RICHOMD.

Nilipokuwa kwenye mizunguko yangu kwenye jiji la Dar ikiwa ni pamoja na kuonana na watu wangu nilimpa ride mtu maeneo flani na pembeni kulikuwa na saloon ya kina dada ambao walikuwa wamekaa nje kwasababu hakuna biashara na hata air condition haifanyi kazi na kafeni kenyewe kaliko ndani kanapuliza joto badala ya hewa nzuri.

Ghafla akatokezea CHINGA MMOJA ambaye alikuwa amepigika kinoma huku malapa aliyovaa yakiwa hovyo hovyo huku kisigino kikiwa kinakanyaga chini wakati akitembea.....Ikanifanya nijiulize alikuwa wapi wakati wa kampeni za CCM...Na ama malapa hayo yaliyokwisha vibaya sana ni yale aliyopewa kwenye kampeni ya 2005!

Huyu chinga likuwa akiuza vyupi na sidiria akiwa amekamata mkononi huku akimlilia dada mwenye saloon anunue walau sidiria moja ili aweze kwenda kula!

Mjadala uliendelea huku chinga akiongea hadi mapovu meupe yakimtoka pembezoni mwa mdomo na huku akionekana kuwa maisha ni magumu na hata hali yake kiafya ni mbovu kutokana na mlo wa kubabia babia!

Mimi kuwa kwangu pembeni kulinipa shida kwani nilkuwa sijui nimtetee yupi!
Chinga anasema hajala na anategemea kina dada wananunue sidiria ili walau akale...

Mwanadada wa saluni naye akawa anadai hata yeye anafunga biashara muda si mrefu ili akajaribu kuangalia kama nyumbani kuna chakula kwani hajafanya biashara kwa karibu wiki nzima kwasababu ya umeme.

Mabishano yalikuwa makali...Lakini wote walikuwa hawana makosa...UCHUMI WETU ULIKUWA UMELALA EXCEPT KWA MAFISADI MAFIOSO ambao wao mambo yao ni mswano tu ndani ya viyoyozi na akaunti zinazoingiza mabilioni ya jasho la wananchi na migenerator huku wakiendelea kulipwa pesa za wananchi kwasababu tu RICHMOND iliyoshindwa ku provide umeme wa dharura kwa wananchi na hivyo mabilioni yao ya kodi kupewa kina ROSTAM,MKAPA,KIKWETE,LOWASSA,MRAMBA,MGONJA NA MAFIOSO WENGINE WA CCM!

Dada wa Saluni naye alikuwa akihitaji sidiria lakini hana pesa...Chinga akaomba walau mia saba ili akale kwa kushusha bei ya sidiria kutoka 1200...Dada akawa still hana...Na chinga akaanza kuchukia akidhani kuwa Dasa ni tajiri mwenye roho mbaya!

Nikatoa elfu nikampa nikamwambia ampe Dada hiyo sidiria...
Nikachoma gari moto huku machozi akinitoka!

EMPATHY TUME LACK...Afadhali sasa wengine nao wamegundua na kulia baada ya Kelly.
 
Matatizo kama ya uwanja wa fisi yapo karibu across nchi zote chini ya jangwa la sahara. Hayo unayoona leo mkuu ni afadhali kuliko hali ilivyokuwa takriban miaka 5 iliyopita.

Bado kuna mengi ya kufanyika kuondokana na dhahama iliyopo pale uwanja wa fisi na hali ni mbaya zaidi huko kwenye machimbo ya madini ambapo watoto wadogo baina ya miaka 10 - 18 wanatumikishwa vibaya sana.

Juhudi za pamoja zinahitajika ( serikali na sisi wananchi) kuondoa/kupunguza mabalaa pale uwanja wa fisi. Kwa mfano suala la umalaya watoto wadogo wanafanya/wanafanyishwa umalaya pale lakini tujiulize wateja wa hao malaya ni kina nani? kwa namna moja au nyingine ni sisi? wenye hali ya kujiweza kidogo. Ushauri wangu ni kila mtu wa nafasi yake asaidie kupiga vita janga hili badala ya kulaumu tu.
 
Masaka kama nyie CCM HAMUTAWAKAMATA MAFISADI...Then hata hiyo kauli yako ya kumpa KIKWETE ambayo sasa unaibadilisha kuwa eti akisafishe chama...Inaonyesha bado hutaki kukubali kuwa KIKWETE NI FISADI MAFIOSO!
 
Endelea na ubishi wako wa kisomi ambao mpaka leo hii na mimi nilikuwa naufanya bila kugundua kuwa ubishi wa kisomi hauleti suluhisho lolote la matatizo. Kwa ubishi huu unaotaka kuuanzisha labda kwa nia ya kubadili mwelekeo wa thread hii, jua kuwa utabishana na wengine lakini sio mimi.

Asante.

Mada hapa ni epiphany uliyo ipata baada ya kuona clip ya dakika 25 ya maisha Uwanja wa Fisi.

Jibu swali: Hukuyajua matatizo ya Tanzania au ulikuwa huna intellectual honesty, una feki mawazo?

Kama una nia kweli ya kusaidia nchi yako, tusaidie kuelewa watu kama wewe -kabla hujapata epiphany - ambao bado wanatetea ufisadi, ni nini kinawafanya wawe hivyo. Tusaidie kuelewa hilo.

Hayo mambo ya Uwanja wa Fisi hukuyajua? Jibu swali.

Na kama yale mawazo yako ya mwanzo yalikuwa ndio "ubishi wa kisomi" sidhani kama huo usio elimika utakao kuja nao sasa hivi utasaidia.
 
Back
Top Bottom