jamani, jana nilipata mshituko wa ajabu, nilikwenda pharmacy moja nikakutana na akina mama wawili wanatafuta gloves eti wametumwa na zahanati ya "KIWANJA MPAKA" iliyoko soko matola Mbeya kuwa wakatafute hivyo vifaa kwa ajili ya ndugu yao anaetarajia kujifungua. Kwa bahati mbaya katika duka hilo gloves zilikuwa zimekwisha wakachanganyikiwa- walikuwa hawajui waende wapi saa tatu na nusu usiku. Hii haingii akilini? Gloves za shilingi mia mbili hazipo?
Pole sana ndugu yangu. CCM wamekandamiza Bilioni mbili na ushehe leo tu! Ndio Maisha Bora hayo ya Captain wa mafisadi.