Askofu Kilaini: Tanzania inahitaji rais kama Kagame

kiche

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
456
155
Wakati nchi ikizidi kuyumba kwa ombwe la uongozi,Askofu msaidizi wa jimbo la bukoba amepigilia msumari kwenye kidonda kwa kusema kuwa kwa sasa kwa jinsi hali ya nchi ilipofikia Tanzania inahitaji rais kama paul kagame ili kuinusuru nchi,amedai kuongoza kwa 'mkono wa chuma' ndiko kunaweza kulinusuru taifa kwa sasa, na mtu sahihi kwa kuongoza ni lazima awe na uwezo kama kagame ambaye ni rais wa Rwanda.

Askofu huyo, alisema tatizo kubwa linaloikabili Tanzania wakati huu, ni kumpata kiongozi ajaye atakayekuwa tayari kufa kwa ajili ya kuwashughulikia mafisadi bila kuwaonea huruma, huku akisisitiza kuwa Rais Kagame wa Rwanda ni mfano wa viongozi wanaohitajika sasa kuiongoza Tanzania.

Kauli Kikwete ni changuo la Mungu

Akizungumzia kauli yake aliyowahi kuitoa mwaka 2005 kwamba mgombea urais kupitia CCM Rais Jakaya Kikwete alikuwa ni chaguo la Mungu , Askofu Kilani alifafanua kwamba alichosema ni kwamba, ‘Sauti ya watu ni sauti ya Mungu,' kwani mgombea huyo alikuwa amechanguliwa na watu kwa asilimia 80, alichomaanisha ni kwamba mgombea huyo amekubalika na watu.

maoni yangu:

kwanza kwa mara ya kwanza namuunga mkono askofu kilaini kwa kauli hii,nchi kwa sasa imefikia hatua mbaya sana kwa atakayepinga kwa hali ambayo taifa limefikia naamini kuwa atakuwa mmoja wa wale ambao wanalimaliza taifa hili au ni mtu asiye na uwezo wa kutambua jema na baya.

Nawasilisha.
 
Nakubaliana nae kwa 100%, Rwanda wapo juu sasa na nchi iliyotoka kwenye Genocide, hawana madini ila wana mbuga moja yenye sokwe mtu na wanalima kahawa lakini wanapiga hatua nzuri sana.

Tunahitaji mtu kama kagame kwa miaka 20 hivi ili abadili akili za watanzania ili wawe wazalendo
 
wakati nchi ikizidi kuyumba kwa ombwe la uongozi,askofu msaidizi wa jimbo la bukoba amepigilia msumari kwenye kidonda kwa kusema kuwa kwa sasa kwa jinsi hali ya nchi ilipofikia tanzania inahitaji rais kama paul kagame ili kuinusuru nchi,amedai kuongoza kwa 'mkono wa chuma' ndiko kunaweza kulinusuru taifa kwa sasa, na mtu sahihi kwa kuongoza ni lazima awe na uwezo kama kagame ambaye ni rais wa rwanda.

Askofu huyo, alisema tatizo kubwa linaloikabili tanzania wakati huu, ni kumpata kiongozi ajaye atakayekuwa tayari kufa kwa ajili ya kuwashughulikia mafisadi bila kuwaonea huruma, huku akisisitiza kuwa rais kagame wa rwanda ni mfano wa viongozi wanaohitajika sasa kuiongoza tanzania.

kauli kikwete ni changuo la mungu

akizungumzia kauli yake aliyowahi kuitoa mwaka 2005 kwamba mgombea urais kupitia ccm rais jakaya kikwete alikuwa ni chaguo la mungu , askofu kilani alifafanua kwamba alichosema ni kwamba, ‘sauti ya watu ni sauti ya mungu,' kwani mgombea huyo alikuwa amechanguliwa na watu kwa asilimia 80, alichomaanisha ni kwamba mgombea huyo amekubalika na watu.

maoni yangu:

kwanza kwa mara ya kwanza namuunga mkono askofu kilaini kwa kauli hii,nchi kwa sasa imefikia hatua mbaya sana kwa atakayepinga kwa hali ambayo taifa limefikia naamini kuwa atakuwa mmoja wa wale ambao wanalimaliza taifa hili au ni mtu asiye na uwezo wa kutambua jema na baya.

Nawasilisha.

hata mimi namuunga mkono. Hii nchi tunahitaji rais mwenye vision na anayeelewa ni wapi nchi iwe baada ya kipindi fulani. Si hawa ambao ndoto yao ni kuwa rais basi.
 
Mi pia nilimwelewa mda mrefu..nafikili alìhusianisha na msemo wa "Vox Populi,Vox Dei" =The Voice of the pple,The Voice of God".....lakn badae tumegundua it wasn't....
 
JK utaficha wapi uso wako??miaka 4 hii utaweza kurudisha imani kwa walalahoi kama ilivyokuwa kabla 2005??maana hata ungetakiwa kupewa utakatifu naamini ungepata bila kupingwa kabisa maana hata makanisa yoote yalikupa support yao moja kwa moja ila kwa sasa.........hata wakiweka jiwe hapo naona kabisa nchi itaenda tu bila tatizo!!!
 
Inasikitisha kuwa na kiongozi ambaye anaogopa waharifu!!,ni nani atakuwa mtetezi wa wanyonge kama kiongozi awezi kuwashughulikia wakandamizaji,kuna kipindi pinda aliwai kusema kuwa eti hawa watu wakiguswa nchi itayumba!!ni upumbavu wa aina yake.
 
Nashukuru kwa kufafanua kauli yake, coz watu walikuwa wakimalizia na kama kibwagizo, Jk alikubalika lakini hakutumia fulsa hiyo kuwatumikia waliompenda, na ndiyo maana baada ya kumaliza muda wake JK atakuwa ndo rais atakayechukiwa na watz kuliko Rais yeyote aliyewahi kutawala Tz, badala ya kueendeleza upendo aliopewa bure ameishia kutafuta chuki.
 
JK utaficha wapi uso wako??miaka 4 hii utaweza kurudisha imani kwa walalahoi kama ilivyokuwa kabla 2005??maana hata ungetakiwa kupewa utakatifu naamini ungepata bila kupingwa kabisa maana hata makanisa yoote yalikupa support yao moja kwa moja ila kwa sasa.........hata wakiweka jiwe hapo naona kabisa nchi itaenda tu bila tatizo!!!

Mhe akiamua anaweza kurudisha imani kwa wanachi,kwa sasa watu wanachotaka ni kuwashughulikia mafisadi tu,hakika nakuambia kuwa siku akiamua kufanya maamuzi magumu wananchi hawatamsahau,wananchi wanakerwa sana na jinsi watu wanavyofisadi nchi na bado wanapeta.
 
kwa hiyo kwa sasa sio chaguo la Munguy? aeleze kwa sasa JK ni chaguo la nani sasa
 
Nashukuru kwa kufafanua kauli yake, coz watu walikuwa wakimalizia na kama kibwagizo, Jk alikubalika lakini hakutumia fulsa hiyo kuwatumikia waliompenda, na ndiyo maana baada ya kumaliza muda wake JK atakuwa ndo rais atakayechukiwa na watz kuliko Rais yeyote aliyewahi kutawala Tz, badala ya kueendeleza upendo aliopewa bure ameishia kutafuta chuki.

Ni kweli watu weeengi sana walimwamini J.K...Kuna wamama walikuwa wanalia kwa furaha na upendo pale alipowapa matumaini ya maisha,uhakika wa maji,mikopo na huduma za afya!Upendo wa weng umegeuka chuki,tulimtumainia sana lakin ametuangusha.....!!kuna hata raia wa kgen walingia ktk mkumbo wa kupenda...niliwah kumuuliza mmoja!kwanin umempenda J.K?Akanijibu...."Amo Quia Amo"= "I love bcoz I love"
 
duh cjui huyu ndo bingwa wa kujikomba kwa viongozi?mnajua kupelekwa bukoba ilikuwa ni adhabu?amejitambua
 
Ni kweli watu weeengi sana walimwamini J.K...Kuna wamama walikuwa wanalia kwa furaha na upendo pale alipowapa matumaini ya maisha,uhakika wa maji,mikopo na huduma za afya!Upendo wa weng umegeuka chuki,tulimtumainia sana lakin ametuangusha.....!!kuna hata raia wa kgen walingia ktk mkumbo wa kupenda...niliwah kumuuliza mmoja!kwanin umempenda J.K?Akanijibu...."Amo Quia Amo"= "I love bcoz I love"

Umenikumbusha mkuu!!kwa mtu anayefahamu,hivi yale mabilioni ya kikwete yaliishia wapi???
 
Wakati nchi ikizidi kuyumba kwa ombwe la uongozi,Askofu msaidizi wa jimbo la bukoba amepigilia msumari kwenye kidonda kwa kusema kuwa kwa sasa kwa jinsi hali ya nchi ilipofikia Tanzania inahitaji rais kama paul kagame ili kuinusuru nchi,amedai kuongoza kwa 'mkono wa chuma' ndiko kunaweza kulinusuru taifa kwa sasa, na mtu sahihi kwa kuongoza ni lazima awe na uwezo kama kagame ambaye ni rais wa Rwanda.

Askofu huyo, alisema tatizo kubwa linaloikabili Tanzania wakati huu, ni kumpata kiongozi ajaye atakayekuwa tayari kufa kwa ajili ya kuwashughulikia mafisadi bila kuwaonea huruma, huku akisisitiza kuwa Rais Kagame wa Rwanda ni mfano wa viongozi wanaohitajika sasa kuiongoza Tanzania.

Kauli Kikwete ni changuo la Mungu

Akizungumzia kauli yake aliyowahi kuitoa mwaka 2005 kwamba mgombea urais kupitia CCM Rais Jakaya Kikwete alikuwa ni chaguo la Mungu , Askofu Kilani alifafanua kwamba alichosema ni kwamba, ‘Sauti ya watu ni sauti ya Mungu,' kwani mgombea huyo alikuwa amechanguliwa na watu kwa asilimia 80, alichomaanisha ni kwamba mgombea huyo amekubalika na watu.

maoni yangu:

kwanza kwa mara ya kwanza namuunga mkono askofu kilaini kwa kauli hii,nchi kwa sasa imefikia hatua mbaya sana kwa atakayepinga kwa hali ambayo taifa limefikia naamini kuwa atakuwa mmoja wa wale ambao wanalimaliza taifa hili au ni mtu asiye na uwezo wa kutambua jema na baya.

Nawasilisha.

Yaani kama wadau mnakumbuka hata Mh Kagame aliwahi kuulizwa anahitaji nini ili kulikomboa bara la Africa, alisema Mungu angekuwa amemuweka kwenye nchi yenye rasilimali kama Tz na yeye akawa rais basi angekuwa super power wa africa na Dunia hii. Naunga mkono hoja ya Kilaini kwani ni kweli sasa hv Tz inahitaji rais mkono wa chuma na asiye na makundi na anaekerwa na umasikini wa watanzania.
 
Dr.slaa is the Tanzanian Kagame! ndo maana magamba wanaogopa sana na kumwaga propaganda kila siku! ila WATASHINDANA SANAA, HAWATASHINDA! WATANZANIA mungu yupo nasi msife moyo our kagame is on the way!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom