Tanzania inahitaji compulsory voting for 2015 and beyond!

Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,316
10,782
Salaam wanaJF!

Baada ya pilika pilika za uchaguzi mdogo wa Igunga, sasa mambo yanarudi kama yalivyozoeleka. Kuna mengi ambayo nimejifunza, na natumaini wanaJF, watanzania wote na vyama vya siasa wa/vimejifunza pia. Lakini kuna jambo moja ambalo mimi nimejifunza toka uchaguzi wa mwaka jana na sasa juzi tena jambo hilo limejitokeza, na kunifanya nipendelee kulisema.

Kama ilivyokua mwaka jana, katika uchaguzi mdogo wa Igunga takwimu zimeendelea kuonyesha kwamba idadi ya wananchi wanaojitokeza kupiga kura inakua ni ndogo mno ukilinganisha na wale walijiondikisha!! Pale Igunga katika waliojiandikisha (170,000+) ni wananchi 50,000+ tu ndio waliopiga kura!! Hii ina maanisha waliopiga kura hawakufika hata nusu ya waliojiandikisha!!

Pendekezo langu:
Ili kuepuka tatizo hili kwa kipindi hiki cha kuandika katoba mpya, suala la compulsory voting lazima lijumuishwe kwenye katiba hiyo. Sheria na kanuni za kufanya compulsory voting ifanye kazi lazima ziwekwe wazi; pamoja na adhabu zake. Kwa namna hii hakika litasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la wananchi kujiandikisha na kutumia hizo kadi kama vitambulisho tu badala ya kupigia kura.

Jisomee hapa chini juu ya compulsory voting kwa ajili ya uelewa zaidi, na kufahamu nchi gani zinatumia utaratibu huu.

Compulsory voting - Wikipedia, the free encyclopedia
Compulsory Voting
Compulsory voting around the world | Politics | guardian.co.uk
Compulsory Voting: Debatabase - Debate Topics and Debate Motions
BBC NEWS | UK | UK Politics | Britain 'needs compulsory voting'
Compulsory Voting | Voter Turnout | International IDEA

 
Back
Top Bottom