Mongoiwe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 524
- 263
Inashangaza Tanzania kujiita Kisiwa cha amani, nchi yenye utulivu, huku tukilalamikia kuongezeaka kwa vitendo vya Uharifu kuwa kunatokana na Idadi kubwa ya wakimbizi ambao wametokana na Nchi zenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, huku Tanzania hiyo ikiendelea na usafirishaji wa Siraha haramu katika nchi zinazopigana vita.
Katika hali isiyotazamiwa katikati ya Jiji la Mwanza kuna idadi ya vifaru 11 vya kijeshi vikiwa katika mabehewa ya Treni mali ya kampuni ya TRL eneo la 'Mwanza South', Inasemekana kuwa vipo hapo kugonjea kusafirishwa kwa Meli kuvuka kwenda nchini Sudani kupitia Uganda.
Haijafahamika Vifaru hivyo vimetokea wapi kupitia Reli ya kati, lakini duru za Kijeshi zimebainisha wazi kuwa huenda vikawa vimetokea katika Bandari ya Salama.
Kwa wanaokaa Jijini Mwanza maeneo ya Mkolani, Nyegezi, Buhongwa na hata Malimbe watakuwa wameviona vifaru hivi kwa vile vinaonekana kwa urahisi sana uwapo katika barabara ya Mwanza Shinyanga hata katika gari ingwa vimefunikwa kwa Maturubai.
Vifaru hivi vimeoneka hapo kuanzia Jumamosi mpaka jana Jumapili jioni na kwa sasa vinadaiwa vimepakiwa katika meli kusafirisha Usiku.
Iwapo ni kweli Vifaru hivi ambavyo vimeonekana hapa Mwanza vinasafirishwa kwenda nchini Sudani basi jambo hili litazidi kuingiza Tanzania katika kashfa ya biashara usafirishaji siraha haramu ama kudhihirisha repoti ya CCTI kuhusu Meremeta iliyoandaliwa na Mwanakijiji.