Tanzania ina wanawake wahandisi wanne tu!

CPU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
3,863
686

CHAMA cha Wahandisi Washauri Tanzania (ACET), kimesema kuwa idadi ya wanawake wahandisi Tanzania ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine kwani mpaka sasa wahandisi waliopo ni wanne. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa ACET, Mwesigwa Kamulali, alisema pamoja na idadi hiyo ndogo amewataka wanawake wenye taaluma ya hiyo kujiunga na chama hicho ili kuweza kushirikiana na kutoa huduma katika jamii.

“Tungependa kuwa na wahandisi wengi wanawake kama tulivyo sisi wanaume, tukiangalia idadi ya wahandisi wanne haitoshelezi kabisa kutoa huduma za ushauri wa kihandisi kwa ufanisi,” alisema Kamulali. Alisema Chama cha Acet awali kilikuwa na wanachama tisa lakini mpaka sasa kina wanachama hai 94 ambao ni sawa na asilimia 47 ya wazalendo wahandisi washauri. Katika hilo, alisema chama hicho kinatarajia kufanya Jubilei ya kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake Januari 27 mwaka huu.

Alisema katika Jubilei hiyo wanatarajia kuwa na wajumbe 200 na wageni kutoka nje 14 ambao watatoka Afrika ya Kusini, Botswana, Zambia, Kenya, Uganda , Sudan, Nigeria na Tunisia. Kamulali alisema katika maadhimisho hayo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda.
 
si kweli,labda sema kuwa wahandisi washauri(consultant engineer) walio wanachama wa ACET na takwimu hizo za wahandisi hata ukienda erb haziko sawa maana siyo wahandisi wote wanajisajili erb hapa tanzania hawaoni umuhimu wake
 
Elimukwanza
Si kweli kwamba wahandisi hawaoni umuhimu wa kujisajili na ERB, tatizo ni kuwa ili usajiliwe kwa mfano kama professional Engineer unatakiwa uandike Technical report ya experience yako kama mhandisi kwenye field at three years after graduating. Wengi wanafanya hivyo na kuwa registered, wengine report zao hazikubaliwi na Board na hutakiwa kudia kuandaa upya. Pia kuna baadhi ya Wahandisi hawafanyi kazi za kihandisi per see, kiasi kwamba wanashindwa kuandika Technical report hasa design ambayo ni muhimu sana kwenye field hii.
Umihimu upo kwani kuna baadhi ya kazi/assignments huwezi kufanya kama hujawa registered. Sema tu enforcement ya sheria husika haijaeleweka kwa watu wengi.
 
Hii habari ni maalum kwa ajiri ya kushawishi wanawake wajitokeze kwa wingi kusajiri . . . hamjagundua tu?
 
Hii habari ni maalum kwa ajiri ya kushawishi wanawake wajitokeze kwa wingi kusajiri . . . hamjagundua tu?
Hata mie nilipoiona nikashangaa, mbona tupo wengi tu!!!
japo bado hatujawa washauri.
nyie waandishi mnapotosha habari ya kitaalamu mnaifanya ya kizushi au umbea!
Faida ya kujisajili kwa sie ambao sio consultants ni ndogo sana, hailipi (kwangu at least)
 
Back
Top Bottom