Tanzania ina umwa

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Tanzania ina umwa, inaumwa homa kali
Taabani yaangamia, watu hawatafakali
Wenye nacho wanavuma, wakifaidi mali
Tanzania ina umwa jahazi lenda mrama

Ina madonda ya utumwa, ufisadi na majangili
Na vikwazo vya uduma, vyote vinatuhadhili
Maradhi yanayochoma, tupo kama tumbili
Madawa na usalama, vyote kwetu ni ghali
Tanzania ina umwa jahazi lenda mrama

Roho zetu zinauma, hali zetu ni dhalili
Viwanda bora vya umma, tumevitupa mbali
Wanatunyonya wazima, na tumeshika makali
Tanzania ina umwa jahazi lenda mrama

Wako wapi walio wema, viongozi maadili
Tunalia lia mama, wanauza zetu mali
Twanyonya wetu uzima, tumekuwa kandambili
Tanzania ina umwa jahazi lenda mrama

Twaburuzwa kama uma, usokuwa na makali
Tunachinjwa kama nyama, twaliwa kama ugali
Hatuna mbele wala nyuma, tupo dhofu hali
Tanzania ina umwa jahazi lenda mrama

Tusikubali kusimama, wala tusitulie tuli
Mafisadi wapo nyuma, tupigane tusikubali
Wapo kwenye nema wanatuona hatuna akili
Tanzania ina umwa jahazi lenda mrama

Bora tupate lawama, kuliko hii hali
Amkeni wana wema, tuondowe udhalili
Kusiwepo kusimama, tuondoe muhali
Tanzania ina umwa jahazi lenda mrama
 
Tanzania ina umwa, inaumwa homa kali
Taabani yaangamia, watu hawatafakali
Wenye nacho wanavuma, wakifaidi mali
Tanzania ina umwa jahazi lenda mrama

Ina madonda ya utumwa, ufisadi na majangili
Na vikwazo vya uduma, vyote vinatuhadhili
Maradhi yanayochoma, tupo kama tumbili
Madawa na usalama, vyote kwetu ni ghali
Tanzania ina umwa jahazi lenda mrama

Tatizo JF kuna watu fulani ni wavivu wa kusoma hapo wataishia ubeti
wa kwanza tu na wengine watalalamika eti ni ndefu!
 
Tatizo JF kuna watu fulani ni wavivu wa kusoma hapo wataishia ubeti
wa kwanza tu na wengine watalalamika eti ni ndefu!
Vijana wa siku hizi wmeathiriwa sana na video games, na ilo ndio tatizo kubwa sana, ile hali ya kujisomea hawana kabisa, na ukitaka uwafiche basi andika jambo lako kwa njia ya tamathali za semi au kimafumbo, hapo utawaacha mbali kabisa.
 
Back
Top Bottom