Tanzania ina ombwe la uongozi?

KAPONGO

JF-Expert Member
May 29, 2009
1,661
668
Jambo kubwa lililojiri Tanzania katika siku za hivi karibuni, ukiachia mauaji ya kusikitisha yaliyotokea mjini Arusha, ni Uamuzi wa Waziri Ngeleja kutangaza kuwa 'serikali' imeamua kuilipa Dowans mabilioni ya fedha kutekeleza hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya ICC, iwapo hukumu hiyo itasajiliwa Mahakama Kuu.


Hata hivyo wakati Wananchi wakiwa bado hawajazinduka kutokana na mshtuko na ganzi waliyoipata kutokana na hukumu yenyewe na kauli hiyo ya 'serikali', ambayo kwa mtazamo wa wanaojali maslahi ya umma, haikutegemewa na inakatisha tamaa. Na sasa sauti kutoka nyikani zinasikia kupitia vyombo vya habari, vijiwe kikubwa zikihoji kujirahisi kwa serikali katika jambo zito kama hilo kwa mustakabali wa nchi, bila hata vyombo muhimu kama bunge, na baraza la mawaziri kupitia uamuzi huo na kutoa Msimamo wa pamoja kuhusu kadhia nzima..... Na tayari Waziri wa Afrika Mashariki Bw. Sitta ameshasikika akikosoa uamuzi wa Ngeleja, halikadhalika waziri wa fedha Bw. Mkullo ameshasema kuwa hazina haina fedha za kuilipa Downs.

Kwa hali hiyo, jambo moja linaweza kusadifu: Kuwa suala la Dowan ni Mradi wa kikundi cha watu wachache ndani na nje ya serikalini kinachotaka, piga ua, kujichotea mabilioni ya fedha za walalahoi, ambao ugumu wa maisha yao huongezeka kila uchao bila ya kuwa na nuru japo ndogo ya matumaini ya kuiona kesho yenye neema.

Kisichoingia akilini kuhusiana na sakata hilo ni usiri mkubwa wa ushughulikiaji wa jambo lenyewe na Ukurupukaji wa 'akina Ngereja' wa kukubali kirahisi kulipa bila kufanyika tafakuri ya kina kwa kutumia vyombo stahiki....Hivi Ngereja anakosaje subira na utashi wa kufikisha suala hilo katika kikao cha baraza la mawaziri ili lijadiliwe na kutolea maamuzi ya pamoja ya serikali! kabla ya kulipeleka bungeni kujadiliwa na kulitolea Uamuzi kwa niaba ya wananchi.... vinginevyo tuhuma zinazozidi kuenea hivi sasa mitaani kuwa huo ni mpango mwingine wa mafisadi kuifilisi nchi sanjari na kuhujumu uchumi, zinazidi kupata mashiko kila siku ipitayo!!


Sasa Yupo wapi yule kiongozi anayeelewa mahitaji ya dhati ya Watanzania na atakayekuwa tayari kuwatumikia wao tu kwa nguvu zake zote na maarifa yake yote...na asiye kukubali kurubuniwa na pandikizi lolote, na aliye tayari kuwaumbua na kuwasulubu wote atakao wabaini wanapora mali na kuhujumu uchumi wa nchi kwa dhahir ama kwa uficho, ..na afanye hivyo huku akiwa na macho makavu yasiyo na chembe ya woga..lakini asukumwe na uzalendo usio na shaka na uwe kwa kwa manufaa ya taifa? Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom