Tanzania ina nguvu kubwa ya jeshi kusini mwa Africa

Acheni kuwaza vita jamani, na mkae mkijua hapo mbabe pekee atakuwa ni yule atakaepata suport ya kina Obama. Kwa hiyo mjue kabisa kitakachotokea. Kwanza kama vp si tuwaachie tu mbona si tuna maziwa kibao? kiding! Misri wanakomalia lake victoria wamalawi wakichukua nyasa na bado wakenya wanafaidi k'njaro du! tukifanya mchezo wajukuu wetu watakuja kutuchapa fimbo kwa uzembe.
 
Ushindi wa vita - nyingi ni gorilla - ktk Africa unategemea vitu vingi. Vifuatavyo kwa 'order of importance' ni:-. 1. mbinu za kivita za ki gorrila. 2. Uzalendo na 'determination' ya jeshi 3. Idadi 4. Technolojia 5. Support ya w'nchi 6.Washirika nje ya nchi
 
Malawi wana jeshi la anga bora zaidi ya tz. Marubani wengi wa precisionair wanatoka Malawi Airforce.
 
Idadi ya wanajeshi haina maana sana. Kigezo muhimu ni ujuzi na vifaa vya kivita walivyonavyo wanajeshi hao.
Wanajeshi wa Tanzania wamezoea kuonea raia tu, na wanatumiwa na watawala kukandamiza haki za wananchi badala ya kutetea maslahi ya Taifa.
Wanajeshi wa Tanzania wanatumika kulinda uporaji wa raslimali za Tanzania kuzipeleka kwa wageni nje, kulinda viongozi mafisadi, kupiga virungu na mabomu ya machozi wananchi wanaodai haki zao kwa amani, n.k.
Kwa mtaji huu, jeshi la Tanzania litashindwa vibaya sana na Malawi kwa sababu ya laana iliyojikusanyia kwa vitendo vyake hivyo vyote.

:israel: Mkuu Heshima yako! Hapo kwenye redi nyekundu plz revise it, elimika tofauti kati ya Polisi na JWTZ. Nadhani wadau wengi ktk uzi huu unaposema Jeshi wanamaanisha TWTZ kwa dhana ya ulinzi wa mipaka, but hilo la kuzuia maandamano na kupiga virungu, Mhhh...tafakari...! :israel::israel:
 
Idadi ya wanajeshi haina maana sana. Kigezo muhimu ni ujuzi na vifaa vya kivita walivyonavyo wanajeshi hao.
Wanajeshi wa Tanzania wamezoea kuonea raia tu, na wanatumiwa na watawala kukandamiza haki za wananchi badala ya kutetea maslahi ya Taifa.
Wanajeshi wa Tanzania wanatumika kulinda uporaji wa raslimali za Tanzania kuzipeleka kwa wageni nje, kulinda viongozi mafisadi, kupiga virungu na mabomu ya machozi wananchi wanaodai haki zao kwa amani, n.k.
Kwa mtaji huu, jeshi la Tanzania litashindwa vibaya sana na Malawi kwa sababu ya laana iliyojikusanyia kwa vitendo vyake hivyo vyote.

Ni mpumbavu pekee anayewezatoa analysis kama hii. Naona mawazo mengi humu ni kama ya watoto wasioelewa hata wanalolijadili. Mnadhalilisha jamii forums.
 
Kimsingi sitaki kuunga mkono thread hii. Ijulikane leo kwamba nguvu za jeshi lolote ni kipimo cha utendaji kazi wake, basi. Hata kama una zana za kivita class one, kama wasomi wetu wa uchumi, huwezi ku claim ama kuonekana uko powerful, Tanzania haina historia ya kupigana vita nyingi, so kusema iko vizuri kijeshi is highly questionable. Ni ukweli pia kwamba ari, kujituma na kujiamini kuliwafanya Vietnam kuonekana powerful na sio vitambi ama kufyeka nyasi ikiwa tu kuokoa raia wakizama si zaidi ya mita 2000 baharini ni kitendawili.

Binafsi sipendi kuongelea suala la nguvu za jeshi kwa kuwa kwanza jeshi letu ni wasiri mno na pili hakuna anayeweza ku analyze military capability kwa uwazi akaachwa. So wanaosema kinyume na mimi ama ni ubishi tu ama wanataka kuona maafa ndipo wakubali mawazo yangu.

Tusiwe wepesi kuunga ama kukataa hoja ila tuwe na uhakika na maneno yetu bila chembe ya mashaka. Vita isome kwa jirani yako usiiombee ije kwako, ni hatari. Mods funga hii maneno mbofu sana.

G Kassanga
Tabora.
 
Ni Nyerere ama Nyenyere ilimaanisha, jibu hapo kisha tuendelee...
Ni Tabora hii, utaipenda tu.
 
Hey wakubwa, wingi wa wanajeshi co nguvu ya jeshi,,uingereza kanchi kadogo but ilitawala africa, usa, etc, kwa dunia ya sa hv hatuangalii wingi wa watu bali matokeo, israel taifa dogo lenye wanajeshi apprx 100,000 tu lakini lipo ktk top 10 ya majeshi yenye nguvu duniani ambayo hayo mengine yana millions of soldiers,

Tusijipe moyo kwa kuwa tuna wanajeshi wengi je tuna vifaa vya kutosha? Angalia south africa ni powerful kwa africa but wana wanajeshi 55000 tu.
 
Zoooote tuzianike hapa

tafuteni toka kwenye sources zote mzilete hapa ili tuwasaidie watu wetu ambao wanatutegemea sisi wana JF kuwafanyia kilakitu

attachment.php
[/CENTER][/IMG]
 
Sisemi kwamba Tutapigwa!! Kumbuka wasoma biblia Wafilisti walikuwa na Jeshi Kubwa lakini kamanda wao Goliath Alipigwa na kijana mdogo Daudi Tena kwa Jiwe, La muhimu Mungu awe upande wetu
 
Tanzania kijeshi iko imara sana maana hata wachina hapa tz wapo wengi sana..na pia kuhusu silaha hii huwa ni siri ya nchi na walinzi wake...kwani wewe tangu umezaliwa umeshawahi hata kuona silaha zimenunuliwa lini na wapi.

Lakini kwenye maonesho unaona vitu vya kisasa na haujui vimekuja lini, so hope kwamba nchi yetu iko imara sana muhimu hapa ni watu kutoandika upuzi kiasi cha kutoa siri za ndani ya nchi yetu kuweni makini sana coz hata hawa jamaa nao wanaona haya yanyoandikwa hapa na kuyafanyia utafti kwa makini sana so nakuomben tuwe makin jaman
 
Yule mama anaamini Uingereza wanaweza kumsaidia maana alipokwenda UK akarudi na kutangaza USHOGA Ruksa Malawi, kama ni vita Kamandi ya Songea wanamaliza kila kitu na tayari wemeshaanzaanza maandalizi muhimu
 
Back
Top Bottom