Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Nikiangalia kwa kweli Tanzania ina matajiri walio na uwezo pengine kuizidi serikali ,kuna nchi moja jina kapuni ni ndogo tu ,ila nchi yenyewe ni tajiri na ina matajiri ,kiongozi mkuu siku moja machale yalimcheza na kuwaita matajiri wote ,ambao wana makampuni makubwa sana ,ya ujenzi na hata viwanda na mali zinginezo katika mkutano huo suali la kwanza aliwauliza kutokana na utajiri walionao ambao wameupata wakiwa ndani ya nchi wameifanyia nini nchi yao ,huku kiongozi huyo mkuu akiwa na data kamili za kila tajiri na pia akielewa kwa kina ni akina nani wanafanya juhudi za kujitolea kwa ajili ya nchi yao na hata wale wasiotoa nao pia alikwisha kuwa na taarifa nao.
Alipata majawabu mengi na yote hakusema kitu ila aliwambia wawe tayari kuisaidia nchi yao ,ikiwemo kujenga mabarabara mahospitali na mashule ikiwemo nyumba za ibada. Kwa kweli matajiri waliitikia wito na hata wale waliokuwa na ubakhili waliondoa ubakhili wao na kusaidia kwa kutoa michango na wengine kujengea nyumba sehemu zile ambazo wana asili nazo ,kwa mfano kijiji alichotoka kina nyumba hamsini mbovu mbovu zilizochoka na za zamani basi ,hujenga idadi ya nyumba hizo na kuwagaiwa wale wenye nyumba mbovu na zile nyumba mbovu hupigwa greda na sehemu hiyo huweza kujengwa shule au zahanati na misaada ikiendelea kwa aina hiyo kwa nchi nzima na maendeleo yalizidi kiasi kila mtu ana nyumba ya kisasa na sehemu bora za kufurahia watoto.
Je hapa tz matajiri tulionao wameifanyia kitu gani Tanzania ?