Tanzania in SWISS AIR Page /Poland.

Steven Sambali

JF-Expert Member
Jul 31, 2008
352
170
Kwa wanaojulia lugha za Eastern Europe,
Hii artical ipo kwenye Swiss air page (Poland). Nimejaribu kuibadilisha iwe ya Kiingereza ila hawa google wanatafasiri kivyao baadhi ya maneno. Anyway hilo si muhimu. La muhimu hapa ni kuona kuwa SWISS AIR wanatufagilia kwa kuweka hii habari kwenye ukurasa wao.
Unaweza kuifungua na kui-mark hiyo habari, na baadaye ubonyeze upande wa kulia wa mouse na zitatokea opition kadhaa, chagua ile ya PAGE INFO/ TRANLSATE in English. Itabadisha na kuweka katika English(kwa wale walikuwa hawafahamu). Ila kichwa cha habari kinatakiwa kisomeke kama
:TANZANIA, AMBAYO HAMUIFAHAMU - TRIP YA AGNIESZKA RODOWICZ:

GONGA HAPA
 
Hii nayo ni habari nzuri.
Wakiwa wengi wanatua Tanzania, bei zinaweza kushuka na hivyo kuvuta watalii wengi kuja kwani ikifika peak, bei zinakwenda juu hadi zinakatisha tamaa. I hope watakuja wengi au niseme watarudi wengi. Sijui LUFTHANSA wameishia wapi? Miaka hiyo ukienda DIA utawaona wengi sana wakitua na wakati wa Mwinyi wakakimbia karibu wote. Nafikiri Tanzania inarudi kidogokidogo kwenye barabara.

Egypt Air kurejesha safari zake nchini
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,March 03, 2009 @07:38

Kukua kwa sekta ya utalii na usafiri wa anga nchini kumelihamasisha Shirika la Ndege la Misri (Egypt Air) kuanza safari zake tena baada ya kuacha kuja nchini Aprili 2004. Akizungumza na wadau wa usafiri wa anga, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Meneja wa Shirika hilo nchini, Wael Eldemerdash, alisema shirika hilo limeamua kurudisha safari zake baada kubaini kuwa sekta ya utalii inakua kwa kasi na hivyo itachangia shirika lake kufanya biashara nzuri wakati huu.

"Kukua kwa sekta ya utalii na biashara nchini, kumetusukuma kuanzisha safari za ndege zetu nchini ili kuongeza kasi ya watalii kutoka Misri kuja Tanzania na wafanyabiashara kuja kuwekeza nchini," alisema Eldemerdash.

Katika utafiti waliofanya kwa mwaka mmoja, walibaini kuwa sekta ya utalii nchini inakua kwa kasi, hivyo shirika lake pamoja na kuanza safari, litaanzisha mpango wa ushirikiano na Shirika la Ndege la Tanzania ili kufanya biashara ya usafiri wa anga vizuri na kwa pamoja.

Shirika hilo ambalo litaanza safari zake Juni mwaka huu, limeboresha huduma zake kwa kuleta ndege kubwa na kuongeza safari kutoka moja ya wakati ule hadi nne ambazo zitakuwa Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili kila wiki. Kwa kuanzishwa safari hizo, meneja huyo anaamini litaongeza idadi ya watalii kutoka nchi za Mashariki ya Kati na za Kiarabu kuja nchini kwa gharama nafuu, ambapo awali watalii kutoka nchi hizo walihitaji ndege mbili au zaidi ili kutua katika ardhi ya

Tanzania kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam. Balozi wa Misri nchini, Hael Adel Nass, alisema kuanzishwa kwa safari kati ya Cairo na Dar es Salaam, kutaongeza na kukuza biashara ya utalii kati ya nchi mbili hizi ambazo zitakuwa zikitembeleana mara kwa mara.

Kuanzishwa safari ya shirika la ndege hiyo nchini, kutaongeza pia kasi ya uwekezaji katika sekta ya utalii na katika sekta nyingine zikiwamo za biashara ambazo zitapatikana nchini. Naye mdau wa shirika hilo nchini, Mustafa Rajani alisema, Watanzania na Wamisri watapata fursa nyingine ya kutembeleana bila kuzunguka, kama ilivyokua nyakati zilizopita
 
Naskia na Turkey nao wataleta ndege zao Dar!

Sasa ATC kwa nini wasireciprocate? Nao wapeleke ndege huko?
 
Naskia na Turkey nao wataleta ndege zao Dar!

Sasa ATC kwa nini wasireciprocate? Nao wapeleke ndege huko?

Pana wakati nilisoma kuwa Air Tanzania walikuwa wameruhusiwa kutua Germna na German wakasema wataanza kuleta ndege zao. Ila sina uhakika walikuwa waje Condor Air au Lufthansa. Sijui iliishia wapi maana kwa hizi ndege zetu kutua ndani ya Europian Union, sijui kama wataruhusiwa.

Ilikuwa chance moja nzuri sana. Tatizo si tu kurusha ndege, hapa ndege huwa ni tangazo moja kubwa sana la biashara. Mtu akiona ndege imendikwa Air Tanzania itamkaa sana kichwani kuliko akiona kwenye TV tangazo welcome to Tanzania.

Ssiku moja nategemea atatokea mtu atimize hizo ndoto za kuwa na shirika la ndege la Tanzania.
 
Tanzania hatuna tabia ya kujitangaza, tunaendekeza msemo wa chema chajiuza kibaya chajitembeza. hatujui kuwa biashara ni matangazo
Tuamkeni toka huu usingizi mzito.
 
Tanzania hatuna tabia ya kujitangaza, tunaendekeza msemo wa chema chajiuza kibaya chajitembeza. hatujui kuwa biashara ni matangazo
Tuamkeni toka huu usingizi mzito.
Ni kweli mkuu tuna tatizo hilo,ila nafikiri kuna mapungufu yanayochangia sisi kuwa/kubweteka katika promo.
 
Swiss Air is 100 per cent owned by LUfthansa as KLM owned by Air France so there is no need for LUFHTANSA to send its metal to DAR, they route their pax through Zurich as AF does in Amsterdam.
 
there is three major Airline alliance and each of them has services to DAR and all of them transfer their pax through the its partners hub.

One World - BA - LHR-DAR - partners- American Airline, Iberia, Finnair, LAN and Malev serves DAR indirect through LHR

Skyteam - KL - AMS-DAR - partners - Northwest, Delta, Continental, Air France, Aero Flot serves DAR through AMS

Star Alliances - LX - ZRH-DAR - partners- LUfthansa, United Airline, Air Canada, Turkish, BMI, Us airways and Lot polish serves DAR through ZRH
 
Hayo Mkuu ni mambo ya JK, hiyo unayoona ni paid advertisement na haijawekwa hapo kwa kuwa Swiss Air wanaipenda sana TZ. hiyo ni campaign ya kuitangaza Tanzania kiutalii iliyoanzishwa na JK, kutokea CNN, London Bus, sasa huko tena. Ahsante JK, kazi zako tunaziona.
 
Hayo Mkuu ni mambo ya JK, hiyo unayoona ni paid advertisement na haijawekwa hapo kwa kuwa Swiss Air wanaipenda sana TZ. hiyo ni campaign ya kuitangaza Tanzania kiutalii iliyoanzishwa na JK, kutokea CNN, London Bus, sasa huko tena. Ahsante JK, kazi zako tunaziona.

Dar,
Siyo kweli uliyoyaandika. Kama ingelikuwa hivyo basi hiyo artical ingelikuwa hata kwenye site nyingine za Swiss Air, huoni hilo tangazo. Pia huyo dada ni mwandishi wa habari kwenye gazeti kubwa kabisa la Poland lililo pamoja na mengineyo. Yeye ni mpiga picha, msafiri na mwandishi wa habari. Ukiangalia katika site yake hii :- Agnieszka Rodowicz » Tanzania utaona kuwa chini kabisa kuna nembo ya Swiss air ambao kwa haraka haraka nafikiri ndiyo waliomdhamini.
Maadamu dada ni mtu wa gazeti, nafikiri Swiss air walimpa ticket na Gazeta Wyborcza(Wiborcha) wakampa pesa na dada akaanza safari. Mwaka jana kuna jamaa mwingine wa gazeri hilo alitumwa kwenda Afrika na akaanzia Tanzania. Alikuwa kadhaminiwa na Polish Tv.

Ukitaka artical ya yule dada na picha alizoweka basi soma hapa na ukifika chini nenda next page. Ila fanya mchezo uleule yaani una mark page na kuitafasiri kama nilivyoandika mwanzo (kuiweka kwenye English). http://www.agnieszkarodowicz.com/?cat=75&paged=3
 
Hayo Mkuu ni mambo ya JK, hiyo unayoona ni paid advertisement na haijawekwa hapo kwa kuwa Swiss Air wanaipenda sana TZ. hiyo ni campaign ya kuitangaza Tanzania kiutalii iliyoanzishwa na JK, kutokea CNN, London Bus, sasa huko tena. Ahsante JK, kazi zako tunaziona.

Haya ndiyo mambo Malcom x alikataa, unarukia tu habari kwa kuwa lengo lako ni kumsifia JK unaanza tu popote! Yasikilize yachuje, na fanya intelligent decision sio kukurupuka tu mkuu! Huu ni upuppism!
 
Back
Top Bottom