Tanzania: In Search of the Talented Tenth - Kuwatafuta Moja ya Kumi Wenye Talanta

Huyu si marehemu? How did he make the list? I know he was very talented but I thought we were looking at the 10% who will be the driving force of Tanzanian development. Na Filbert Bayi is past his prime.

Muziki wa Mbaraka Mwinshehe ume influence wengi, umeburudisha wengi, umefariji wengi, na bado ujumbe katika nyimbo zake uko relevant leo hii.

Martin Luther King Jr ni marehemu lakini mmoja kati ya watu wanaoenziwa sana na kutolewa mifano katika mambo mbalimbali leo hii. Alichosimamia wakati wa uhai wake ni kanuni ambazo zitakuwa relevant milele na milele hata kama yeye keshakufa.
 
Yup unayosema ni kweli mkuu. Ila I was under the impression kuwa hii thread ni ya top 10% ya watz sasa na siyo the top 10% most talented Tanzanians of all time. Or did I get this thread wrong? Maana the driving force of any economy is the people who are currently alive and the dead wana baki kuinfluence the living 10%.
 
Kuna watu bado wana influence katika contemprary world ingawa tayari wameshakufa mamia ya miaka. Angalia katiba ya Marekani. Unataka kunambia kwa namna moja au nyingine hai influence uchumi wa Marekani? Je watunzi wake bado wako hai?

Kwangu mimi kama mtu mchango wako bado uko relevant katika maisha ya leo nakuhesabu bado upo. Hata Companero mwenyewe amerejea dhana ya W.E.B. DuBoise ambaye ni marehemu tokea sijui 1963.
 
Nathani inahitaji ubobezi ili mtu aitwe mtaalam wa taaluma fulani. First degree pekee haitoshi. Mhasibu awe na CPA/ACCA/ CIMA etc, Mwanasheria awe na Uadvocate na wasio na regulators kama wachumi japo uwe na Phd.

Jamaa hana sifa zakuitwa mchumi
 
Wadau usiku ni mwingi. Nitaendelea na mjadala huu kesho. Kwa leo napenda kuweka mambo haya sawa kuhusu hii mada.

JK: Hii ni orodha ya watu 4,000,000 sio 10 na inagusa fani zote muhimu, ndio maana pembeni nimeweka fani zao na pia wasifu wao upo hapo kwenye majina yao, ukiyabofya utaingia kwenye mitandao ya wasifu.

NN: Kweli wapo waliokufa ambao wametoa mchango mkubwa na michango hiyo bado inatusaidia leo ila hapa tuangalie wenye talanta walio hai na namna ambavyo tunaweza kuunganisha talanta zao kuleta mapinduzi.

MF: Vigezo vilivyotumika vimo ndano ya wasifu wa watu hao navyo ni mvuto wao kwa wananchi, mchango wao kwa jamii, ukinara wao katika fani zao pamoja mabadiliko yaliyotokana na mchango wao kwetu.

ZK: Ili jamii yoyote iendelee kwa kasi ya ajabu inahitaji viongozi, watawala, wavumbuzi na watendaji ambao ni vinara katika nyanja hizo, yaani, ambao ni 1 ya 10 ya wenye talanta katika fani husika na wanaonyesha njia.
 
Hashimu role model, wa nini, kushika crotch na ku tweet amefeli drug test?

Prof Ndulla huyu aliyekuwa chini ya Balali muda wote ufisadi unaendelea BOT?

What is the point of this thread anyway? the entire premise is unforgivably copy paste of some petty top-down black bourgeoisie in W.E.B. Isn't this the same model we have had since independence?

What we need is a paradigm shift, a transformation of the matrix, from top down to bottom up.

I would rather pump some Booker T Washington with some modern day Garveyites.

Blu Ray:

W.EB alijaliwa kuishi maisha marefu. Na katika maisha yake ali-move kutoka katika perspectives zake. Kipindi cha mwanzo ali-support capitalism, baadaye akawa mjamaa.

Moja ya motive ya kuandika talented tenth ilikuwa ni kutoa hoja za kumjibu Booker T Washington. Booker alitaka watu weusi kujishughulisha na kisomo cha kazi za mikono kwanza kabla ya kudai elimu ya juu.

Na kutokana na influence ya Booker, mitaala ya vyuo vya watu weusi ilibadilishwa. Kwa mfano Howard University ambayo ilikuwa na mitaala sawa na vyuo vya wazungu ilibidi ibadili mitaala yake na kuwa chuo vya vocation. Mpango huu ni sawa na Tanzania iamue kubadili mitaala ya Chuo kikuu cha DSM na kutoa elimu ya VETA kwa sababu watanzania wengi hawajuhi ufundi seremala.

Matokeo ya kubadilisha mitaala ya vyuo vya watu weusi ili-detriment elimu ya juu kwa muda fulani. Na vilevile haikusaidia watu weusi kwa sababu industrialization ilishaingia Marekani. Watu badala kwenda kwa seremala kuchongewa furniture walikwenda moja kwa moja kwenye furniture zilizotengenezwa kiwandani.

Hivyo WEB alipotoa talented tenth alikuwa anasisitiza umuhimu wa elimu ya juu kwa watu weusi. Alikubali nafasi ya elimu ya ufundi na sayansi kimu ambayo Booker aling'ang'ania, lakini aliona pia kuwa elimu hii haikuzi talent yoyote kwa sababu haitoi analysis yoyote hile.

Mfano wa elimu aliyong'ang'ania Booker ni mfano wa elimu tuliong'ang'ania Tanzania toka tumepata uhuru. Toka tumepata uhuru tumesambaza elimu ya msingi kila kijiji. Tumejenga vyuo vya maarifa ya nyumbani, tuna vyuo vya ufundi stadi, tuna sekondari za kilimo na michapuo mbalimbali. Tuna vyuo vya ushirika, tuna chuo vya maji. Lakini bado mkulima mwenye nusu heka Marekani, ulaya au Asia anatoa mazao mengi kuliko mkulima wa Tanzania.

Nimekaa Ulaya, Nimekaa Marekani na sijaona mtu anapoteza miaka zaidi ya miwili kujifunza kuoka mikate, kuwa fundi seramala, kujifunza ubwana shamba au sayansi kimu. Ni Tanzania pekee yake mtu anakwenda chuo cha ustawi wa jamii na kupoteza miaka kujifunza kupiga randa.

Kwa upande wangu talented tenth ni kitu muhimu sana. Henry Ford aliweza kuweka watu wachache wenye vipaji kwenye ku-design magari, na watu wenye elimu ya kawaida kwenye assembly lines na kuweza kuongeza uzalishaji ambao ulisaidia wenye vipaji na wasio na vipaji. Na hii yote ni cookbook kutoka kwa Adam Smith, division of labour. Unaongeza uzalishaji pale unapogawa kazi, Job description kama anavyoita Ngabu.

Ukija kwetu tuna kiwanda kama Nyumbu. Lakini kutokana na configuration ya kiwanda, hata ukitoa assigment ya kutengeneza baiskeli 1000 kwa siku. Bado utendaji utashindikana.
 
Kweli kabisa Zakumi. Kuna watu wengi wenye vipaji bila umaarufu na kwangu mimi maendeleo wajibu au jukumu la ujumla (collective responsibility). Kila mtu anatoa mchango wake.

Haswa! Mimi hapa warehouse kuna meneja wa stratergy na vision ambaye job description yake ni tofauti na hao watu wa R&D. Wenzetu wanakuwa na dira na mwelekeo wa wapi wanataka kampuni yao iwe ktk miaka mitano, kumi, ishirini, na thelathini ijayo.

Tuna safari ndefu sana.

Yeap Safari ni ndefu sana. Na wakati mwingine utamaduni wetu (Ndivyo tulivyo unaongeza ugumu wa mambo).

Fanya kitu kwa mapenzi na kusaidia humanity. Lakini wengi tunafanya kwa sababu ni hot cake.
 
Zakumi asante kwa uchambuzi wako kuhusu nadharia ya moja ya kumi ambayo baadhi ya wadau walikuwa wanaihoji na kuuliza maana yake bila ya kusoma alichosema muasisi wake kwenye mtandao niliowapa. Nakubaliana kwa kiasi kikubwa na jinsi ulivyofananisha Elimu ya Kujitegemea ya Julius K. Nyerere na Elimu ya 'Kushusha Ndoo Pale Ulipo' ya Booker T. Washington. Hata Mwalimu mwenyewe alikiri kuwa mawazo yake yalitokana na huyu jamaa kama dondoo hii hapa chini inavyodhihirisha:

After independence the wider African community became clear to me. I was concerned about education; the work of Booker T Washington resonated with me. There were skills we needed and black people outside Africa had them. I gave our US Ambassador the specific job of recruiting skilled Africans from the US Diaspora. A few came, like you. Some stayed; others left. We should try to revive it. We should look to our brothers and sisters in the West. We should build the broader Pan-Africanism. There is still the room - and the need.

Kitu kimoja ambacho Zakumi unakisahau ni kuwa Mwalimu aligundua kuwa tuna safari ndefu sana kwenda kwenye hayo mapinduzi ya viwanda ndio maana alitaka tuwe na Elimu Kamili ya kujitegemea itakayotusaidia kuyamudu maisha yetu ya kawaida ambayo wengi wetu tutayaishi vijijini. Sasa hapo hatukumuelewa ndio maana leo tumebanana mijini japo fani zetu za useremala na ukulima zinafaa zaidi huko vijijini. Kinachotakiwa sasa ni kujenga pale alipoishia kwa kuhakikisha kuwa moja ya kumi ya kila Kijiji/mtaa inaongoza kuleta maendeleo katika vijiji/mitaa vyao. Na hivyo hivyo iwe kwa moja ya kumi ya wilaya, mkoa na taifa.
 
ten percent of what?? need to do what mbona hiyo theory is outdated kama baadhi mauti mnao waongelea.

wenzetu wame-rule like that for centuries, lakini walipotaka maendeleo ya society late thirties wakaona athari za ignorance in society. the danger was immense mpaka kufungua social welfare na free education for all. na huo ndio ukawa mwisho wa hao ten percent yako leo wapo in terms of life style and privilege only siitaji kueleza ni wewe kutafsiri. lakini there are so many who can challenge and contribute in society, make their names for themselves huo ndio umuhimu wa ku-educate umma mzima.

reason being the ten% wanaweza leta huo ubunifu lakini the 90% wasieshimu umuhimu wake na kuaribu maendeleo. amna kitu muhimu duniani kama elimu kwa wananchi wote the more you educate the better.

tatizo kubwa la umaskini amini usiamini ni cultural rather than the ability, that is a proven fact. mifano michache ya umaskini ni kuto jali elimu, kutokua na malengo yenye ukweli na kuishi kwa leo rather than plan for the future. hizi ndio sababu zinazoleta umaskini, hili watanzania wafaidike ni lazima viongozi wetu waache wao hizo tabia na zipelekwe chini. binadamu wa kawaida ni subject of manipulation you only need better ways to impose the thinking.

leo hii unawapeleka wanafunzi wakalime eti shamba la shule tena kwa zamu ya vidato form one mpaka five, six tu ndio wanapona, wakati wenzetu wametumia farasi mmoja tu ku plough shamba zima, au bull: lakini wapi hiyo wenzetu wamefanya before even the industrial revolution sasa huitaji msomi kukwambia hilo mfano hai wakujipunguzia kazi unao tayari.

we need better leadership, and the four economic factors. wenzetu leo wananaua mawazo mapya tu kwa mamilioni hiyo ndio umuhimu wa elimu ya juu kwa jamii.

mifano ya maendeleo kwa kweli tunayo atuhitaji, theories ambazo hazina scientific justifation na wala hazi prove chochote katika maendeleo ya jamii
 
Companero:

Kuna contrast kati ya Booker na W. E. B. Du Bois. Booker alizaliwa katika utumwa na alipata elimu kwa kufanya kazi. Na alipoanzisha Tuskegee Institute ali-model jinsi ya yeye alivyopata elimu kule Hampton Institute. Ali-enroll wanafunzi ambao walifanya kazi na kupata elimu.

Kwa upande mmoja au mwingine haya ni makosa makubwa yaliyofanywa na viongozi wengi weusi. Makosa ya ku-model mafanikio au struggle zao katika mitaala ya kishule.

Kuna kipindi mfumo wa Tanzania uli-model maisha ya Mwalimu. Kwa mfano, mwalimu baada ya kumaliza diploma ya Makerere alifanya kazi miaka miwili. Katika miaka ya sabini, kabla ya kwenda university mwanafunzi aliyemaliza form six ilibidi aende JKT na baadaye afanye kazi miaka miwili.

Hata majumbani, wengine tulipata shida kusoma tulivyotaka kwa sababu wazazi wetu kwa upande mwingine walitaka tukomae kwa kupitia njia zao.

Sina matatizo na elimu ya kujitegemea ambayo mwalimu aliandika vitabuni. Lakini nina matatizo makubwa katika implementation zake. Elimu ya kujitegemea ilimtaka mwanafunzi wa Tanzania kutumia kwa siku masaa 8 darasani na baadaye masaa 2 au 3 kwenye elimu ya kujitegemea. Hii ilikuwa ni kum-overload mwanafunzi. Mwanafunzi wa Tanzania hana tofauti na mwanafunzi wa Marekani au UK. Mpaka sasa ni miaka 40 na sijaona kitu chochote kinachoashiria kuwa Elimu ya kujitegemea ilileta mabadiliko yoyote zaidi ya abuses zinazofanywa na waalimu mashuleni.

Tukumbuke kuwa hata Sir. Isack Newton alipodondokewa na apple, alikuwa amepumzika chini ya mti. Mwanafunzi wa Tanzania hana muda wa kufanya contemplation. Sasa hiyo talent itakuzwa vipi? Wingi wa kazi za nguvu haukuzi talent hata siku moja.

Elimu sio chanzo cha mapinduzi ya viwanda. Chanzo cha mapinduzi ya viwanda ni economic needs. Hivyo kutumia elimu kama tool ya kuleta mabadiliko ya kijamii ni kukiuka misingi ya economic evolution.
 
Wingi wa kazi za nguvu haukuzi talent hata siku moja.

Hehehehe Zakumi, umewahi kupiga boksi warehouse? Hehehehe....ukipiga boksi masaa 8 kwa siku ukirudi nyumbani hoi. Huna hata muda wa kuangalia TV au kusoma gazeti. Ni kupata menu na kuangusha hadi kesho yake. Kazi za nguvu si mchezo bana. Mwambie huyo mjamaa mwenzako maana naona yeye yuko kwenye zone nyingine kabisa kifikra.

Elimu sio chanzo cha mapinduzi ya viwanda. Chanzo cha mapinduzi ya viwanda ni economic needs. Hivyo kutumia elimu kama tool ya kuleta mabadiliko ya kijamii ni kukiuka misingi ya economic evolution.

Waingereza wana msemo usemao 'necessity is the mother of (all) inventions'. Nadhani ndicho unachosema hapa. Mapinduzi ya viwanda yalitokea kwa sababu mahitaji ya vitu na bidhaa na mengineyo yaliongezeka kutokana idadi ya watu kuongezeka na hivyo kulazimisha watu wavumbuzi kuvumbua mbinu nyingine za uzalishaji bidhaa kwa wingi ili kukidhi ongezeko la mahitaji.
 
ten percent of what?? need to do what mbona hiyo theory is outdated kama baadhi mauti mnao waongelea.

wenzetu wame-rule like that for centuries, lakini walipotaka maendeleo ya society late thirties wakaona athari za ignorance in society. the danger was immense mpaka kufungua social welfare na free education for all. na huo ndio ukawa mwisho wa hao ten percent yako leo wapo in terms of life style and privilege only siitaji kueleza ni wewe kutafsiri. lakini there are so many who can challenge and contribute in society, make their names for themselves huo ndio umuhimu wa ku-educate umma mzima.

reason being the ten% wanaweza leta huo ubunifu lakini the 90% wasieshimu umuhimu wake na kuaribu maendeleo. amna kitu muhimu duniani kama elimu kwa wananchi wote the more you educate the better.

tatizo kubwa la umaskini amini usiamini ni cultural rather than the ability, that is a proven fact. mifano michache ya umaskini ni kuto jali elimu, kutokua na malengo yenye ukweli na kuishi kwa leo rather than plan for the future. hizi ndio sababu zinazoleta umaskini, hili watanzania wafaidike ni lazima viongozi wetu waache wao hizo tabia na zipelekwe chini. binadamu wa kawaida ni subject of manipulation you only need better ways to impose the thinking.

leo hii unawapeleka wanafunzi wakalime eti shamba la shule tena kwa zamu ya vidato form one mpaka five, six tu ndio wanapona, wakati wenzetu wametumia farasi mmoja tu ku plough shamba zima, au bull: lakini wapi hiyo wenzetu wamefanya before even the industrial revolution sasa huitaji msomi kukwambia hilo mfano hai wakujipunguzia kazi unao tayari.

we need better leadership, and the four economic factors. wenzetu leo wananaua mawazo mapya tu kwa mamilioni hiyo ndio umuhimu wa elimu ya juu kwa jamii.

mifano ya maendeleo kwa kweli tunayo atuhitaji, theories ambazo hazina scientific justifation na wala hazi prove chochote katika maendeleo ya jamii

Juma Contena:

Karibu jamvini. Ukweli wa mambo umasikini Tanzania haukuletwa. Umasikini ulikuwepo.

Hii theory haiko outdated. Kama ni hivyo UK, Canada, USA wasingetoa immigration visa kwa special talent category. Pamoja na kutoa elimu bure kwa watu wao, wanaelewa wazi kuwa kuna special talents. Na dynamic nzima ya uchumi wa Marekani unategemea special talents.
 
Hehehehe Zakumi, umewahi kupiga boksi warehouse? Hehehehe....ukipiga boksi masaa 8 kwa siku ukirudi nyumbani hoi. Huna hata muda wa kuangalia TV au kusoma gazeti. Ni kupata menu na kuangusha hadi kesho yake. Kazi za nguvu si mchezo bana. Mwambie huyo mjamaa mwenzako maana naona yeye yuko kwenye zone nyingine kabisa kifikra.

Waingereza wana msemo usemao 'necessity is the mother of (all) inventions'. Nadhani ndicho unachosema hapa. Mapinduzi ya viwanda yalitokea kwa sababu mahitaji ya vitu na bidhaa na mengineyo yaliongezeka kutokana idadi ya watu kuongezeka na hivyo kulazimisha watu wavumbuzi kuvumbua mbinu nyingine za uzalishaji bidhaa kwa wingi ili kukidhi ongezeko la mahitaji.

Nilipiga mabox kwenye distibution center. Nilichopata pale ni kujaza misuli tu kwenye mikono, nothing more.

Katika miaka ya 60, 70. Mashirika ya misaada yalitoa misaada mingi ya elimu Tanzania. Shule zilifunguliwa kila kijiji na elimu ya watu wazima kila kona. Kama elimu kilikuwa ni chanzo cha mafanikio ya maendeleo, basi Tanzania isingekuwa kwenye shimo la nchi masikini.

Nilipokuja Marekani nilifanya juhudi za kusoma au kuangalia documentary za inventors wao wa mwanzo, kama Edison, Benjamin Franklin, Wright brothers. Ukiangalia kwa undani elimu yao ni chini ya elimu ya form IV inayotolewa Tanzania. Lakini kulikuwa na vitu vilivyo-drive wao kuwa wavumbuzi. Na vitu hivyo ni mahitaji ya kiuchumi na sio elimu.
 
Zakumi,

..unafahamu lolote kuhusu mahusiano ya elimu ya ufundi Japan na technological revolution iliyotokea huko?

..kuna mahali nimesoma, if i am not mistaken, uliikandia elimu ya ufundi. je huoni umuhimu wa shule za ufundi kama Moshi Tech, Ifunda Tech, au Mazengo Tech?

..mimi tatizo langu ni kwamba hakuna a clear path inayomwezesha mwanafunzi aliyekwenda VETA kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu.

NB:

..samahani kama nimetoka nje ya mada.
 
Commandante:

Nadhani ni zaidi ya miaka minne sasa toka tujaridi hili. Katika kipindi hicho mijadala mbalimbali imezuka. Mmoja ukiwa ni ule wa Dr. Malima Bundala, Ndivyo Tulivyo.

Vilevile katika kipindi hiki cha miaka minne nime-graduate katika perispectives zingine pia. Lakini pamoja na yote hayo Talented Tenth iliyoandikwa na W. E. B. Du Bois mwaka 1903 bado ni Analysis nzuri kwa nchi zinazotaka kupiga maendeleo kwa kutumia engineering kama Tanzania.

Mpaka sasa juhudi kubwa zinafanyika kuelimisha watu lakini configurations za watu wenye elimu wafanye nini imekuwa kitendawili mpaka sasa. Na hapa ndipo linapokuja swali la minimum requirements ya nchi ku-launch development revolution or Renaissance. Je Tanzania imeshafikia minimum requirements?
Zakumi, ulijadili hayo hapa hapa jamvini?!

Btw, ninyi nyote mliochangia hii mada nadhani ni mjumuiko wa hiyo talented tenth. NN anajijua yumo ila kwa makusudi tu hujing'atua from time to time...
 
ZK: Naona 1 ya 10 yetu huko USA inaanza ku-take the lead hapa: http://www.dicotaus.org/

NN:Maboksi nimebeba mkuu, kipindi hicho ndipo nilipokutana na ex-Mjamaa Zakumi ndani ya DHB

JK: Nazifuatilia hoja zako kwa karibu nitazijibu kwa kina akili yangu ikitulia maana sasa imejaa sana.
 
Jenerali ulimwengu
john rutaisingwa
elvis musiba
ben r mtobwa
MZEE MWANAKIJIJI
 
Last edited:
Zakumi,

..unafahamu lolote kuhusu mahusiano ya elimu ya ufundi Japan na technological revolution iliyotokea huko?

..kuna mahali nimesoma, if i am not mistaken, uliikandia elimu ya ufundi. je huoni umuhimu wa shule za ufundi kama Moshi Tech, Ifunda Tech, au Mazengo Tech?

..mimi tatizo langu ni kwamba hakuna a clear path inayomwezesha mwanafunzi aliyekwenda VETA kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu.

NB:

..samahani kama nimetoka nje ya mada.

Ndio nimekandia kwa sababu Moshi Tech, Ifunda Tech, au Mazengo Tech wanakwenda kwa kuchaguliwa na sio kwa mapenzi yao. Mtu ambaye hataki kuwa fundi kwanini upoteze muda wako kumfundisha ufundi?

Kuhusu Japan:
Japan ni nchi ya ustaraabu kwa muda mrefu. Lakini kuna kipindi walihamua ku-preserve utamaduni wao na hivyo kukataza influence ya kutoka nje na kuzorotesha maendeleo yao. Lakini hayo yalibadilika wakati Marekani walipotaka kufungua biashara kinguvu na wajapani.

Wamarekani walimpeleka Commodore Matthew Perry kulazimisha urafiki wa kibiashara. Commodore alipowasili Japan alipiga mizinga kutoka kwenye manowari zake za kivita ambayo iliwaogopesha sana waJapan. Na waJapan walipoona Manowari za kisasa ndipo walipoelewa kuwa sera zao za ku-preserve utamaduni wao ziliwafanya kuwa backward kuliko western countries. Hivyo walianzisha programs za ku-compete na west.

Nilipokuwa Ulaya nilijifunza kuwa waJapan wali-recruit ma-profesa wengi kutoka Ujerumani katika miaka ya 1850. Na hili kufanya hivyo waliwalipa maProfesa hao mishahara iliyokuwa zaidi ya mara kumi ya kile walichopata Ulaya. Na vilevile walianza kupeleka waJapan kusoma nje. Hivyo programs zao za mwanzo zilikuwa ni kwenye ku-master technology.

Katika maelezo yangu naweza nikawa nimejikanyaga lakini link hii inaweza kukupa nini alichofanya Mfalme Meijdi http://afe.easia.columbia.edu/japan/japanworkbook/modernhist/meiji.html
 
Zakumi, ulijadili hayo hapa hapa jamvini?!

Btw, ninyi nyote mliochangia hii mada nadhani ni mjumuiko wa hiyo talented tenth. NN anajijua yumo ila kwa makusudi tu hujing'atua from time to time...

Steve D:

Sio jamvi hili. Tulikuwa darhotboard.
 
ZK: Naona 1 ya 10 yetu huko USA inaanza ku-take the lead hapa: http://www.dicotaus.org/

NN:Maboksi nimebeba mkuu, kipindi hicho ndipo nilipokutana na ex-Mjamaa Zakumi ndani ya DHB

JK: Nazifuatilia hoja zako kwa karibu nitazijibu kwa kina akili yangu ikitulia maana sasa imejaa sana.

Companero:

Organization za watanzania Marekani uwa zinaanza na kufa hivi hivi. Behind the scene watu wana motives nyingine. Na zile motives zinashindwa ku-mature watu wanajiondokea.
 
Back
Top Bottom