Tanzania imeuzwa kwa Uingereza!

dabo kliki

Member
Sep 19, 2012
47
5
Nimekuwa nafuatilia taarifa toka serikalini muda mrefu sasa kuwa kati ya nchi zilizowekeza hapa TZ nchi ya Uingereza ndo inaongoza ikifuatiwa na Kenya. Ni jambo zuri kupata wawekezaji japo Tz tumekuwa na bahati ya kupata wadekezwaji. Sasa naomba kujuzwa kwa mwenye kujua pasi na shaka ni kwenye sector ipi, miradi ipi, iko maeneo gani, na michango yake kwa taifa inayomilikiwa na Uingereza
Kuna siku utasikia hiyo miradi ni pamoja na Mbuga ya Serengeti, usishangae maana hii ndo Tanzani jamani. Pale TIC nilienda kwa lengo la kupata taarifa hizi ila nilipigwa dana dana na kuulizwa maswali menhgi kwanini nataka kujua na nk nk nk mwisho nikaambiwa mambo mengine ni siri ya serikali na wawekezaji aka. wadekezwaji. Ebu mwenye taarifa atiririke hapa jamvini
 
Uliposema 'imeuzwa' tulitegemea ufafanuzi ni namna gani imeuzwa na kwa bei gani. La ajabu unaomba mwenye taarifa! Kabadilishe 'heading'
 
Nilivyosoma heading nikafurahi kwamba tutakuwa chini ya mwingereza. Kumbe longo longo
 
Back
Top Bottom