Tanzania imetumia zaidi ya bil 5 kununua mitambo ya kuingilia matangazo ya tv, radio na simu

Kama ni kwa ajili ya usalama wa nchi na wananchi wake sina tatizo.

Ndugu zetu watanzania amkeni, yaani kuna mtu anadhani hii ni kwa ajili ya usalama wa nchi? Jifunze kwa watawala wa kihimla wa nchi za Arabuni na mashariki ya mbali. Watu wanaopenda usalama wa nchi wangewekeza hela hizo katika huduma za jamii kuliko kupoteza hela ya hayo mambo ya kijasusi.

Wakati miradi ya maji inashindwa kuendelea kwa kukosa hela, wao wanakimbilia mitambo ya kusikiliza simu na kukatiza matangazo ya radio!!!!!!!!!!!!!!!!!

Hapo pekundu, mikopo huwaga na vipaumbele? Kama ndivyo, kipaumbele ni kujenga hospital na vituo vya afya kupunguza vifo hasa vya wasio na uwezo ambao ni watanzania wengi au ni kupambana na habari zisizoleta vifo vya moja kwa moja? Ukiacha walipa kodi wako wafe wote nani atalipa mikopo hiyo?

Kwenye bluu,Je huo mtambo una "kipima usawa" pia
je ukitibu watu na kuacha vita vya wenyewe kwa wenyewe kama rwanda? kipi ni bora zaidi
 
Wamepiga marufuku maandamano na mikutano ya CHADEMA sasa hawtaki hata Lissu aonekane kwenye Luninga. Si wakifute tu chama cha CHADEMA itakuwa rahisi. Mnaogopa kunyimwa pesa na wafadhili mnabakia kufanya mambo ya kijinga tu . Nchi imejaa wendawazimu watupu!

sasa imekuwa kila jambo likifanywa ni about CDM ... hehehe pro cdm hebu jaribuni kufikiria nje ya box for once

kama ni kweli hichi kifaa/ mtambo ni muhimu kwa usalama wa taifa.. katika maisha kuna vitu ambavyo ni need & want ... hili jambo ni need ... hatuwezi kuwa na taifa lenye holes kibao katika usalama wake ..
 
Hata cmd wakiingia madarakani watautumia mtambo huu.
Kama una manufaa kwa usalama wa nchi sio mbaya, wasiutumie vibaya tu
 
hawajanunua bali ni mkopo toka serikali ya CHINA. Lengo ni kudhibiti vituo vya matangazo vitavyovunja sheria za nchi yetu likiwemo la matangazo yatayohatarisha umoja wa nchi yetu, pia matangazo ya uchochezi na kutawala mawasiliano ya taifa kwani hakuna taifa lisilo na udhibiti wa anga na mawasiliano yake

NOTE
Naunga mkono ujio wa mitambo hii bali ni kuwa na matumizi mazuri yasiyopendelea upande wowote bali kitumike kuimarisha haki . matumizi ya mitambo hii ikitumika vibaya inaleta madhara makubwa ya taifa letu kwani utakuwa ni mwanzo wa kuzika uhuru wa vyombo vya habari na mawasiliano ya wananchi.

Kama kweli unaamini kwamba iko siku serikali kama hii inaweza kuwa na matumizi mazuri ya mitambo kama hii basi siku hiyo itakuwa ni siku Yesu/Issa anarudi duniani.

Kuna mwenye akili ya kuweza kufanya hivyo hapo juu, kwenye serikali?
 
Mnashangaa na kujiuliza nini sasa..? Inamaana hamjui ndio maandalizi ya upatikanaji wa katiba mpya??? Viva ccm kwa maandalizi ya ki intelejinsia...iyo ni game technic aka opportunity napita tuu mtaa huu jamani mi sio mwenyeji
 
hawajanunua bali ni mkopo toka serikali ya CHINA. Lengo ni kudhibiti vituo vya matangazo vitavyovunja sheria za nchi yetu likiwemo la matangazo yatayohatarisha umoja wa nchi yetu, pia matangazo ya uchochezi na kutawala mawasiliano ya taifa kwani hakuna taifa lisilo na udhibiti wa anga na mawasiliano yake

NOTE
Naunga mkono ujio wa mitambo hii bali ni kuwa na matumizi mazuri yasiyopendelea upande wowote bali kitumike kuimarisha haki . matumizi ya mitambo hii ikitumika vibaya inaleta madhara makubwa ya taifa letu kwani utakuwa ni mwanzo wa kuzika uhuru wa vyombo vya habari na mawasiliano ya wananchi.

Naheshimu sana uhuru wako wa mawazo, lakini sikubaliani nawe katika kuunga mkono ujio wa mitambo ya aina hii kwa sababu zifuatazo:

1. Tanzania haina historia ya kuwepo kwa matangazo ya TV ama Radio ambayo yamewahi kuhatarisha usalama wa nchi kwa kiwango cha kuhitaji mitambo hii. Kama una kumbukumbu na jambo lolote lililowahi kutokea na kutishia amani ya taifa likiwa limesababishwa na matangazo ya Tv ama Radio hebu naomba utueleze

2. Uwepo wa mitambo kama hii unaweza kutumiwa vibnaya sana kama itatokea kiongozi dikteta maana anaweza kuamua kukata matangazo ya radio ama TV yoyote mradi tu hapendi msimamo wa chombo hicho kwa maslahi binafsi na kwa kisingizio cha kuwa matangazo yanahatarisha amani ya taifa.

3. Nani ataamua kuwa matangazo haya ni hatari au la na hivyo kufikia uamuzi wa kuyakata? nini hatma ya uhuru wa habari Tanzania katika mazingira kama hayo?

4. Tanzania tuna matatizo mangapi yanayohitaji misaada ama hata mikopo ya haraka kusaidia kuokoa jahazi kwa maslahi ya taifa? Tuna vitanda vya kutosha mahospitalini? Tuna maktaba na maabara katika shule zetu za kata? Tuna vitabu vya kutosha katika shule zetu za kata? Tuna barabara nzuri zinazopitika wakati wote walau mijini? (Ondoa vijijini ambako ni donda ndugu)

Na mwisho kipi bora? Kutumia mabilioni kwa ajili ya kuzuia na kukata matangazo ya radio na Tv ama fedha hizo kuzielekeza kwenye huduma za kijamii kwa manufaa ya taifa zima?

Kweli Tanzania yenye Neema inawezekana!!!!!! Shame on US!!!!!!
 
1. pindi tv ya taifa na magazeti yalipotangaza dr. slaa hawezi kuwa rais huu ni mfano wa habari inayohatarisha usalama wa taifa na ilitolewa kwenye habari za radio na tv zetu na sms za matusi dhidi ya slaa zikasambaa kwenye kila mitamo ya simu

2. ni kumbana rais na vyombo vyake kwenye katiba mpya na chombo hiki kisimilikiwe na serikali bali kimilikiwe na bodi ya wahariri

​4.mikopo inamasharti ndio maana leo ukienda kukopa bank wanakuambia mkopo huu kafanyie biashara gani
 
hawajanunua bali ni mkopo toka serikali ya CHINA. Lengo ni kudhibiti vituo vya matangazo vitavyovunja sheria za nchi yetu likiwemo la matangazo yatayohatarisha umoja wa nchi yetu, pia matangazo ya uchochezi na kutawala mawasiliano ya taifa kwani hakuna taifa lisilo na udhibiti wa anga na mawasiliano yake

NOTE
Naunga mkono ujio wa mitambo hii bali ni kuwa na matumizi mazuri yasiyopendelea upande wowote bali kitumike kuimarisha haki . matumizi ya mitambo hii ikitumika vibaya inaleta madhara makubwa ya taifa letu kwani utakuwa ni mwanzo wa kuzika uhuru wa vyombo vya habari na mawasiliano ya wananchi.

GODWINE,
Kwa kuwa hakuna sheria iliyotungwa itakayoongoza matumizi ya chombo hicho ( Ikiwa habari hiyo ni ya kweli - mimi sina hakika), na kwa kuwa Serikali na vyombo vyake vyote vya dola ikiwemo Jwtz wameonesha upendeleo kwa chama tawala, kwa hiyo basi, ni dhahiri kwamba chombo hicho kitatumika dhidi ya maoni ya wanaharakati na wapinzani, haswa ktk kipindi hiki nyeti cha madai ya katiba mpya.

Kumbuka bado nafuatilia ni kwanini Star tv haikuonekana sehemu kubwa ya Mbulu, Tundu Lissu alipokuwa anajadili yaliyojiri dodoma pale Movenpick akiwa na Mnyaa wa CUF.
 
Rada feki ha!ha!ha! sasa Mitambo ya kuingilia matangazo ya radio na tv ha!ha! nani alikuwa dalali au mtu wa kati katika deal hii! ha! ha! ha!
Baaaaaaaaaasi! kuliko kutumia mijipesa mingi hivyo si wangepiga marufuku tu chombo chochote cha habari ambacho kitatangaza kinyume na wanavyotaka wao! ha! ha! ha! kweli wanatapatapa ha! ha! ha!
 
Ni ngumu kutoa source kwani imetoka kwa moja ya kamanda wa kikosi cha anga, ambaye bado yu kazini akilitumikia jeshi la wananchi wa tz(JWTZ). kuweka jina lake ubaoni ni hatari kwa mtoa habari mwenyewe.

Umesomeka Kamanda Mkuu! Keep it up!
 
At times nahoji VIPAUMBELE vya Taifa letu. Hawa viongozi wetu wanaendesha nchi bila DIRA. Wanaangalia upepo jana uliendaje,ili leo watumie resurces za umma kwa faida yao na kuangalia impact ya mambo kwa wananchi ndipo wa-act kwa kuicombat situation. Sometimes I also wonder about this post, CAG! Mwenye post hii anaweza kubadilisha minds, mitazamo/perspectives za jamii kwa kutegemea na hali ya mfumo,na uhusiano na utawala uliopo.. Kama mnahisi mko positive na matumizi hayo ya serikali katika mitambo hii,then you should as well be positive na kunyang'anywa funguo za ofisi Tido Mhando!
 
Huu ni uongo hakuna kitu kama hicho kwa tv zipi zinazoweza kuleta madhara tv na redio zenyewe zinashika dar salaam tu zipo kiduchu ni upuuzi kutunga huu uongo wakitangaza tu ujinga deffender za polisi zinatosha kuwatuliza kwenye simu ndo daaah siku nyiingi mitambo ipooo zinadakwa na hakuna mjanja anayetumia simu kupiga hizo dili
 
hawajanunua bali ni mkopo toka serikali ya CHINA. Lengo ni kudhibiti vituo vya matangazo vitavyovunja sheria za nchi yetu likiwemo la matangazo yatayohatarisha umoja wa nchi yetu, pia matangazo ya uchochezi na kutawala mawasiliano ya taifa kwani hakuna taifa lisilo na udhibiti wa anga na mawasiliano yake

NOTE
Naunga mkono ujio wa mitambo hii bali ni kuwa na matumizi mazuri yasiyopendelea upande wowote bali kitumike kuimarisha haki . matumizi ya mitambo hii ikitumika vibaya inaleta madhara makubwa ya taifa letu kwani utakuwa ni mwanzo wa kuzika uhuru wa vyombo vya habari na mawasiliano ya wananchi.

Aliyekwambia itatumika kwa uzuri ni nani? Yaani unakuwa km huwajui magamba??? Haya we tulia uone yatakayotokea.....
 
Back
Top Bottom