Tanzania imetumia zaidi ya bil 5 kununua mitambo ya kuingilia matangazo ya tv, radio na simu

hawajanunua bali ni mkopo toka serikali ya CHINA. Lengo ni kudhibiti vituo vya matangazo vitavyovunja sheria za nchi yetu likiwemo la matangazo yatayohatarisha umoja wa nchi yetu, pia matangazo ya uchochezi na kutawala mawasiliano ya taifa kwani hakuna taifa lisilo na udhibiti wa anga na mawasiliano yake


NOTE
Naunga mkono ujio wa mitambo hii bali ni kuwa na matumizi mazuri yasiyopendelea upande wowote bali kitumike kuimarisha haki . matumizi ya mitambo hii ikitumika vibaya inaleta madhara makubwa ya taifa letu kwani utakuwa ni mwanzo wa kuzika uhuru wa vyombo vya habari na mawasiliano ya wananchi.

Kwenye red: Na kwa akili yako unaamini kabisa kwamba serikali ya magamba iko katika mstari wa mbele katika kutenda haki?
Pili: Kutokana na yaliyojiri kwa rada -- jee unafikiri ufisadi hakuna kabisa katika dili hii?
 
Kuthibiti vyombo vya habari (bila shaka dhidi ya utawala wa CCM) kuna maana moja tu -- ya kuendeleza udikteta, kitu ambacho Kikwete alikikataa juzi.
 
Viongozi wa nji hii wanatupeleka kubaya sana na hapo 10% kama kawaida,da kweli hii nchi ina mambo ya ajabu sana tizama wameshindwa kuajiri walimu wanahangaika na mambo yenye maslahi yao binafsi
 
taarifa za kiintelijensia hazinaga sorce, ukitaka pick it, usipotaka ipotezee
DUU! nchi hii noma...Wabunge watulaghai, viongozi wa serikali, vyama vya siasa, na NGOs ndo usiseme..na hata vijiweni mwetu wanataka kubwabwaja tu na wakitakiwa kutoa chanzo cha habari wanakuja juu! DUU! ndo maana iliwahi kusemwa: 'no research no right to ....
 
hawajanunua bali ni mkopo toka serikali ya CHINA. Lengo ni kudhibiti vituo vya matangazo vitavyovunja sheria za nchi yetu likiwemo la matangazo yatayohatarisha umoja wa nchi yetu, pia matangazo ya uchochezi na kutawala mawasiliano ya taifa kwani hakuna taifa lisilo na udhibiti wa anga na mawasiliano yake


NOTE
Naunga mkono ujio wa mitambo hii bali ni kuwa na matumizi mazuri yasiyopendelea upande wowote bali kitumike kuimarisha haki . matumizi ya mitambo hii ikitumika vibaya inaleta madhara makubwa ya taifa letu kwani utakuwa ni mwanzo wa kuzika uhuru wa vyombo vya habari na mawasiliano ya wananchi.

Hapo pekundu, mikopo huwaga na vipaumbele? Kama ndivyo, kipaumbele ni kujenga hospital na vituo vya afya kupunguza vifo hasa vya wasio na uwezo ambao ni watanzania wengi au ni kupambana na habari zisizoleta vifo vya moja kwa moja? Ukiacha walipa kodi wako wafe wote nani atalipa mikopo hiyo?

Kwenye bluu,Je huo mtambo una "kipima usawa" pia
 
HAWAJANUNUA bali ni mkopo toka serikali ya CHINA. Lengo ni kudhibiti vituo vya matangazo vitavyovunja sheria za nchi yetu likiwemo la matangazo yatayohatarisha umoja wa nchi yetu, pia matangazo ya uchochezi na kutawala mawasiliano ya taifa kwani hakuna taifa lisilo na udhibiti wa anga na mawasiliano yake

HAPANA, KUKOPA NI KUNUNUA MAANA LAZIMA UTALIPIA HATA KAMA NI KESHO. PIA KWA UMASIKINI WETU HASA WAKATI HUU HATA UMEME HATUNA WANGESUBIRI; HAKUNA HAJA (PRIORITY) YA MITAMBO HII KWA SASA
 
Is that true? Can you share with us the source of your "uzi"?
 
Nilidhani wanao tayari maana kuna siku JK alikuwa maeneo fulani simu kushney kabsaaaa
 
Jamaa wanaufanyia majaribio ya kufa mtu kwa watu. Kuna dogo mmoja walim plant aokote begi la dola feki kule morogoro wamekuwa wakimutumia kama majaribio baada ya kumtia hofu anatafutwa. Dogo amekuwa on Run kwa muda mrefu sasa na simu za ndugu na jamaa zake zote wame zibug, kuna muda walimkamata wakamfunga vifaa fulani vya kujua anakuwa wapi halafu wakamuachia. Yule dogo alikimbia mpaka siku moja akajichanja akajichomoa kichuma fulani akakitumbukiza chooni. Baada ya muda majamaa wakfika huko kijijini swekeni kinoma wakachimbua choo. Hii ni kama hadithi lakini imetokea na hayo majaribio yamekula mamilioni ya shilingi. Kuna watu watawekewa vichuma hivyo kufuatiliwa nyendo zao na mawasiliano yao.
 
wazo ni zuri tu, cha msingi ni jins vifaa hvyo vitakavyo tumika.inabid ijulikane wazi kua vipind venye maudhui yapi ndo vitazimwa.alaf chama tawala kijue kua 2015 kitakua ni chama cha upinzani kwa hiyo kisitumie vibaya mitambo hiyo.
 
Wamepiga marufuku maandamano na mikutano ya CHADEMA sasa hawtaki hata Lissu aonekane kwenye Luninga. Si wakifute tu chama cha CHADEMA itakuwa rahisi. Mnaogopa kunyimwa pesa na wafadhili mnabakia kufanya mambo ya kijinga tu . Nchi imejaa wendawazimu watupu!
 
Hiyo ndiyo mitambo inayotumiwa na China kudhibiti habari. Bila shaka watawala wa Afrika wanatamani kuiga udikteta wa China manake wameshindwa utawala bora. Hiyo mitambo athari yake itakuwa mbaya sana. Watawala wabovu wataitumia kuwapata wapinzani na wanaharakati wanaowapinga ili kuwazima. Hapo utegemee kuna watu watauawa na hasa watumishi wa serikali wanaoibua issue maovu ya serikali ( whistle blowers) wataathirika kwa kiasi kikubwa.
 
hawajanunua bali ni mkopo toka serikali ya CHINA. Lengo ni kudhibiti vituo vya matangazo vitavyovunja sheria za nchi yetu likiwemo la matangazo yatayohatarisha umoja wa nchi yetu, pia matangazo ya uchochezi na kutawala mawasiliano ya taifa kwani hakuna taifa lisilo na udhibiti wa anga na mawasiliano yake


Hivi kunatofauti ya mkopo na kununua?Je huo mkopo hautalipwa?Liba ya mkopo huo kiasi gani?Nataifa litatumia kiasi gani kulipia wataalamu,spear-parts za mitambo hiyo?Ikumbukwe kwamba China ilitengeneza mitambo mingi ya aina hiyo kuwadhibiti raia wake.Hapa kuna mawili kwanza China katika mpango wake katika kuelekea katika demokrasia imeona mitambo hiyo haina tija pili labda imepitwa na wakati kiteknologia hivyo wameamua kutusokomezea:hatari::hatari::hatari::hatari::hatari::hatari::hatari::hatari:
 
Katika nchi masikini kama tanzania taifa letu limenunua mitambo ya kuingilia matangazo ya radio,television na simu na pia yenye uwezo wa kukata matangazo yake wakati wowote pale wanapoona hayana maslahi na watawala na taifa .

Mitambo hiyo iliyowasili hivi karibuni inatarajiwa kufungwa katika kikosi cha anga cha jeshi la ulinzi (JWTZ) kilichopo karibu na uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere . nadhani mtambo huu ukikamilika kufungwa utakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa habari na mawasiliano katika taifa letu


sawa mkuu wamesahau watafute namtambo wa kuingiliya mawazo ya watu tukiwaza maisha magumu unakukatisha kama MUNGU alivyo fanya kwenye ujenzi wa munala
 
wanakula za mwisho mgoja leo tujue hatima ya magamba tumpokee mnafiki mzee 6 kwenye upinzani hawalipue
 
Ni ngumu kutoa source kwani imetoka kwa moja ya kamanda wa kikosi cha anga, ambaye bado yu kazini akilitumikia jeshi la wananchi wa tz(JWTZ). kuweka jina lake ubaoni ni hatari kwa mtoa habari mwenyewe.
[/QUOTE
asante kwa taarifa mkuu, udikteta aliousema mkulu kwamba anataka kuujaribu ndio sasa utakamilika. mbona mijadala inayorushwa live kwenye vituo vya runinga itakuwa inaminywa ki aina. yangu macho. tumekwisha
 
watanzania tunaunga mkono vitu vya kipuuzi mno
kwanini unadhani hivi vitu ni vya kipuuzi? je unafahamu unaweza kupigana vita na nchi jirani nao wakazima mitambo ya mawasiliano yenu na wakaanza kuwashambulia na kurusha matangazo yao nchini kwenu. je tutafanya nini au haya si manufaa ya kuwa na mitambo ya kisasa ya mawasiliano...pia je ukiwa na shaka na watu fulani kuwa wanamawasiliano ya kigaidi je uwezi kufanya chunguzi kwa kuingilia mawasiliano yao kuokoa taifa?
 
Back
Top Bottom