Tanzania imenunuliwa rasmi na mabeberu by prof Mukandara from proud faces to beggers!

KAMBOTA

Senior Member
Mar 21, 2011
176
103
Ndugu wana jf leo nimemkuta jamaa mmoja ndani ya daladala ameshika kitabu kilichoandikwa na professor Rwekaza Mukandara kinakwenda kwa jina la From proud faces to beggers aisee nilipitisha macho kidogo kwenye kurasa kadhaa aisee ile ni balaa duuh!

Ingawaje huyu professor anahusishwa na CCM ila kiukweli ile ni kazi kubwa natamani wanaharakati wote kama Mwanakijiji, Slaa, Chahali, Ulimwengu, Ndimara, Mwangulumbi, Kubenea,Ngurumo, Matiya na wengine wengi wafanye yafuatayo;

Kwanza waipitie kwa umakini mkubwa
Pili watafsiri na kusambaza kazi hiyo
Tatu wajenge hoja kuhakikisha inatumika kwenye mtaala wa elimu wa primary, secondary na vyuo
Mimi nitaiandika pia kwa uwezo wangu

Nadhani hili likifanyika sasa watanzania watabaini jinsi nchi hii ilivyouzwa kinyemela kiasi kwamba kutoka enzi hizo Tanzania ikionekana mkereketwa wa harakati za uhuru barani Afrika kiasi kwamba mji wa Dar es salaam ukaanza kuitwa Maka ya Afrika mpaka leo hii tumegeuka ombaomba wa kutupwa kiasi kwamba tumebaki kusikiliza amri za mabwana wakubwa kutoka London, Newyork na Paris...Inasikitisha sana!
 
hujakisoma vizuri ni full unafki huyo mukandara ni BOOTLEAKER hamna lolote
 
Ni matumaini yangu katika siku za hivi karibuni husemi ufuatao wa W. B. Yeats utatimilika hapa kwetu: "Turning and turning in the widening gyre. The falcon cannot bear the falconer: Things fall apart; the centre cannot hold; mere anarchy is loosed upon the world." Kwa jinsi mambo yanavyoenda hapa nchini kwetu ni vigumu kuamini kama balaa hiyo haitatufikia- kama ni bado!
 
kwani we hujui? mbona Bush alikuja kumalizia deni sasa hadi risiti ya kuinunua Tanzania wamarekani wanayo, unashangaa nini?
 
Back
Top Bottom