Omutwale
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,429
- 1,045
Nina uhakika wa asilimia 100% kuwa hata kabla Serikali ya ccm haijaondoka madalakani, suala la ushoga lita-RASIMISHWA Tanzania. Na si kweli kwamba, kupinga kwa kauli kunakofanywa na serikali ni kutoridhia ushoga. Atakaye taka kubisha, abishe. Atakayetaka kutusi, afanye hivyo. Lakini ukweli wa mazingira ya kihistoria utasimama hivyo daima.
Ni mwaka 1994 wakati somo la UKIMWI linapigiwa chepuo kuingizwa S/M, Watanzania walikuwa wanapinga sana kwa kutoa sababu kuwa suala la kuzungumzia mambo ya ngono mbele ya watoto wao ni kinyume na maadili. Neno kondomu lilikuwa haramu. Leo tunashuhudia Watanzania walewale wanaimba hadharani "Usione soo kusubiri au tumia kondomu" Baba na bintiye sasa wanakaa sebuleni, wanaangalia wote mwanzo-mwisho matangazo ya TACAIDS yasiyokuwa na tafsida hata chembe, na lile la pedi nalo linapita .... wala hakuna wa kumwonea soo mwenziwe anymore! Zaidi utasiki Baba anamwambia mwanae; hapo Mjomba Mrisho Mpoto kakoleza!
Juzi juzi tu kina Mongella walipokwenda Beijing, Watanzania wakasema hao wanawake wanajifurahisha tu na hayo maazimio yao. Na kweli moyoni Waafrika wengi nami nikiwemo tumebaki kuamini na kuishi na wanawake kama wasaidizi na si kinyume chake. Lakini angalia jinsi waasisi wa masuala ya jinsia walivyoweza kupigania agenda yao na kuipenyeza katika mataifa yetu kupitia serikali na serikali kuizamisha kwenye ngazi ya familia. Kila uchao utasikia campaigns mara Gender-Based-Violence, Women Rights, Rights of Inheritance, Property Rights, etc na kubwa kuliko yote ni Gender Mainstreaming iliyowezesha kuifanya jinsia kuwa suala mtambuka na kusababisha mabadiliko ya sera na sheria mbalimbali. Matokeo yake kwenye ngazi ya jamii ni wanafamilia mfano wa kambare-kila moja ni mkubwa kwa mwenzie na hivyo kusababisha ndoa nyingi hasa za waliopata kozi ya Dr. Rose Shayo (Gender-Elimu ya Juu) kufungwa Jmosi na kuvunjika Jpili! Ngazi ya serikali tunaona vyeo vya sandakalawe-wabunge wasio na majimbo wala kazi, majaji wa kike wasio na sifa na nafasi zingine nyingi tu ambazo lengo ni kufikia malengo na kuwafurahia Wahisani (Kina Cameron).
Mtu yeyote mwenye akili anaamini chandarua si suluhisho la kudumu kuondoa malaria. Sasa iweje kama hayawani mtaani anajua huu ukweli kwa nini serikali badala ya kuziba vifuu na kusisitiza kufyeka machaka, wao wanahamasisha vyandurua? Ukipata ukweli wa lililowafunga viongozi wako kungamua jambo rahisi kama hili, basi huna budi kuafikiana nami kuwa tayari nchi yetu inawatambua mashoga na haki zao na hivi punde itatamka wazi. Lakini mambo mengine si mpaka usikie; kama kusoma hujui hata picha ukutani huioni? Nani, wapi imeandikwa na lini ccm walikwambia hii ni nchi ya kibepari ; lakini ukweli ni upi?
Ni kazi rahisi sana kulifanikisha hili la ushoga na kiufupi tukubali tu kwamba tayari tuko kwenye Taifa linalowatambua mashoga. Tunaona media zinafanya endorsement campaigns kwa kuwatumia Bongo Superstars (Banana zorro, Mzee yusuph, na wengine). Wanauzunguka mbuyu kwa kuyafanya haya ni matangazo ya ya uzazi wa mpango...(walio wengi wanaona huu mfano uko kaskazini ya ukweli ulio kusini!). Hii ni science of behavioral change using marketing techniques! Shtuka! Rais wako tayari amearikwa na anakwenda kuhudhuria mkutano juu ya masuala ya uzazi wa mpango. Nakudokeza, kaa chonjo kusikia maazimio ya mkutano. Ogopa mpango unaokamilishwa taratibu bila haraka (gradually). Mara zote unajikuta umeishatumbukia na kuwa mlevi wa lile unalodai unalipinga kwa nguvu zako zote. Tukubali tu, wakati wakubwa (Obama na Cameroon) wanatamka hadharani kuweka sharti la haki za mashoga si kwamba ndo muda huo lango la ushoga lilikuwa linafunguliwa rasmi, bali ilikuwa ni kuwashtueni wale wote mnaodhani bado hamjarasimisha ushoga kuwa tayari mko kwenye ukanda wa ushoga. Jiulize, kama huna waumini, msikiti utajenga wa nini? Nyongeza ya hapo, Katiba tunayobadilisha sasa ilikuwa inaukubali ushoga! Wasiojua waulize, wanaojifanya kujua wabishe, na wale wasio na hoja kabisa-matusi ruksa!
Siku njema.