Tanzania iko tayari kuongozwa na mwanamke?

Darwin

JF-Expert Member
May 14, 2008
908
56
Wako wamama wengi wasomi na wenye uchungu wa nchi, kiu ya maendeleo, wazalendo.

Sizungumzii itikadi za vyama,

Je TZ iko tayari kuongozwa na mwanamke? JFs mnafikiri ni mwanamama yupi anafaa kuingoza TZ?
 
Wako wamama wengi wasomi na wenye uchungu wa nchi, kiu ya maendeleo, wazalendo.

Sizungumzii itikadi za vyama,

Je TZ iko tayari kuongozwa na mwanamke? JFs mnafikiri ni mwanamama yupi anafaa kuingoza TZ?

Ni kweli kuna kinamama waliosoma na wanafanya kazi vizuri sana mfano yule MD wa NBC holding somebody Agnelus Lupembe, kuna Lawyer mmoja Ms Hawa Senare (REX Attorney), etc. Hata hivyo binafsi pamoja na ufanisi ambao wameuonyesha nadhani bado hawafit nafasi ya Urais. Nadhani hawa tuwatumie tu kama ma CEO wa mashirika hii nafasi ya Upresident bado kidogo.
 
Hakuna mwanamke aliye tayari kuongoza nchi........ Kama ni changes tungeanza na kuandaa vijana

period...!!
 
Tatizo si whether ni mwanamke au mwanaume. My problem ni competence na self confidence. Team player. A kina mama wetu bado waoga. ukiona mbabe basi ujue ana ngao somewhere inayompa nguvu. TUNATAKA MTU MWADILIFU, ANAYEWEZA KUKEMEA NA AKATENDA KWA VITENDO ANAYOYESEMA WAZIWAZI BILA KUOGOPA. tANZANIA TUNAHITAJI MTU JASIRI NA MNG'AMUZI WA MAMBO na sio mtu wa kuburuzwa na kuendesha nchi kishikaji!!!!!
 
Je TZ iko tayari kuongozwa na mwanamke? JFs mnafikiri ni mwanamama yupi anafaa kuingoza TZ?[/QUOTE]

Upo karne ya ngapi? (Darwin 12 February 1809 – 19 April 1882), wake up this is 21st century.
 
Swali Tanzania iko tayari au Watanzania wako tayari kuongzwa na rais mwanamke?
 
Naona wengi mnajibu swali 'Je wanawake wako tayari kuiongoza Tanzania?'.

Kuna wanawake wengi sana nchini wenye uwezo wa kuiongoza nchi.

Tukirudi kwenye swali husika, mi naona Tanzania bado haiko tayari kuongozwa na kiongozi wa jinsia yoyote.

Bado tumekaa kutawaliwa. Kwakuwa wengi wetu tunamaarifa finyu, sisi bado ni watu wa kutawaliwa tu.
 
Hakuna mwanamke aliye tayari kuongoza nchi........ Kama ni changes tungeanza na kuandaa vijana

period...!!

MTM,
Kasema nani?
Hebu nipeni muone kazi!
Lakini hao vijana unaowafagilia wewe kwani umeambiwa vijana ni wa kiume tu?
 
Hii mada ni muflis, kama ile ya kutaka uwiano wa wabunge waume na wake wa 50:50. Hizi mada mbili ni watoto mapacha vimbaumbau, waso na miguu wala mikono.
 
Hii mada ni muflis, kama ile ya kutaka uwiano wa wabunge waume na wake wa 50:50. Hizi mada mbili ni watoto mapacha vimbaumbau, waso na miguu wala mikono.

Naona wewe ndio umepotea njia kabisa.

Bunge la Liberia lina wabunge wanaume na wake 50:50?
Bunge la Ujerumani lina wabunge wanaume na wanawake 50:50?

Rudia post kwanza, sijaipost kwa ajili ya usawa na wanawake na wanaume katika kazi.

Nakuongezea swali jingine,
Utachagua kuongozwa na mwanaume fisadi katika nchi na asiyejali watanzania wenzake au utachagua mwanamke mzalendo mwenye kuijali nchi yake na watu wake?
 
Wako wamama wengi wasomi na wenye uchungu wa nchi, kiu ya maendeleo, wazalendo.

Sizungumzii itikadi za vyama,

Je TZ iko tayari kuongozwa na mwanamke? JFs mnafikiri ni mwanamama yupi anafaa kuingoza TZ?

Hii mada ni muflis, kama ile ya kutaka uwiano wa wabunge waume na wake wa 50:50. Hizi mada mbili ni watoto mapacha vimbaumbau, waso na miguu wala mikono.

Mtoa mada arudi akajipange upya, sijui chimbuko la mada nini au nini anataka tuelewe. NIONAVYO MIMI.
 
Mtoa mada arudi akajipange upya, sijui chimbuko la mada nini au nini anataka tuelewe. NIONAVYO MIMI.

Exactly! Uonavyo WEWE. [Kiswahili lugha yetu]

Swali lilikua:

Kama Tanzania ina wamama wengi wasomi na wenye ufanisi, uchungu wa nchi, wajasiri.
Je akitokea mwanamke kama hao niliowataja hapo juu kwamba anatataka kuongoza nchi.
Watanzania mtakua tayari kumkubalia?
 
Naona wewe ndio umepotea njia kabisa.

Bunge la Liberia lina wabunge wanaume na wake 50:50?
Bunge la Ujerumani lina wabunge wanaume na wanawake 50:50?

Rudia post kwanza, sijaipost kwa ajili ya usawa na wanawake na wanaume katika kazi.

Nakuongezea swali jingine,
Utachagua kuongozwa na mwanaume fisadi katika nchi na asiyejali watanzania wenzake au utachagua mwanamke mzalendo mwenye kuijali nchi yake na watu wake?

Nitajibu thread yako isio na kichwa wala miguu.

Sihitaji mwanasiasa aniongoze.

Umenielewa?
 
Utayari wa nchi kuongozwa na kiongozi mwanamke hakuhitaji gender balance bali kama kuna mwanamke ana uwezo na anasimama, anaongoza Tanzania bila tatizo lolote na Watanzania watampa kura za ushindi wa Kishindo, subirini Mama Migiro 2015 muone.

Nchi kama Norway na Finland zimekuwa zikiongozwa na marais wanawake kwa miaka mingi, mpaka watoto wa nchi hizo wanawauliza wazazi wao, "hivi mwamaume anaweza kuwa rais?".

Waziri Mkuu wa Kwanza mwanamke Bibi. Bandaranaike alipo twaa madaraka dunia nzima walishangaa kwa kufikiri hawezi. Alipokuja Indira Gadhi vivyo hivyo na alipouwawa Sonia Gadhi wahindi wameamini hakuna kiongozi bora kama mwanamke

Dunia inatawaliwa na mfumo dume, wanaume ndio wengi wanamashaka na uwezo wa wanawake. Na wanawake pia walioathiriwa na mfumo huo, ndio maadui wakuu wa wanawake wenzao kwa kuamini 'women's place ni jikoni and that they are no good for nothing except in bed!.

Tunayo list ndefu hapa bongo za wamama washoka ambao wakishika uongozi wa nchi, ni heshima, adabu na maendeleo kwa kwenda mbele. Tuwape nafasi, tuone kazi na tuone mambo.
 
Mwanamke anaweza kuongoza nchi lakini asiwe na mme kwasababu atampotosha
Nimependa point yako hasa the bolded part.

Kwa kusoma michango ya hii thread peke yake, tunapata kwamba wanaume wa TZ bado hawako tayari kuongozwa na mwanamke.Kwa hali hii, mwanamke mwenye kuongoza kama atatokea maana wapo wengi wenye uwezo ( ila wana waume!) basi ni mawili akubali mumewe atawale kwa niaba yake japo indirectly au awe ni mwanamke asiye na mume.Tatizo pia linakuja.Kuna unyanyapaa wa wanawake ambao hawajaolewa katika jamii za kiafrika (kumbuka rais wa Liberia aliwahi kuolewa ila wakaachana na huyo mume kwa sasa ni marehemu). Ikitokea mgombea ni mwanamke ambaye hajawahi kuolewa, basi hiyo itakuwa ndiyo agenda ya kummaliza.

Rais mwanamke akitokea, basi akubali kunyanyasika atakapokuwa amerudi ikulu/nyumbani baada ya saa za kazi maana mume atataka kumwonyesha kwamba yeye bado ndiyo boss hapo nyumbani kama alivyokuwa anafanya mume wa Dr. Specioza Kadzibwe aliyewahi kuwa makamu wa rais Uganda.Akubali vipigo, kejeli na hatimaye kuachana na huyo mume.Baada ya kuachana akubali kusingiziwa kuwa amemuacha mumewe kwa sababu amepata cheo na kumuona mumewe si mali kitu tena!
 
Last edited:
Kwa jinsi siasa zetu zilivyo na mizengwe itakuwa ngumu sana Mwanamke kuongoza but may be angeweza kupunguza matatizo nafikiri Dr. Asha Rose Migiro anaweza
 
Wapo i can Pinpoint only two haraka haraka,Prof Tibaijuka she can, na Dr Asha Rose Migiro,hebu tuwafikirie hawa na ikibidi 2015 Migiro asimame through CCM na Tibaijuka through Chadema bcs these two parties are the only one can lead this country.
 
Back
Top Bottom