Tanzania iko mbioni kujiingiza vita vya DRC

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
549
Kwa mara ya kwanza Tanzania kupitia Benard Membe imesema iko tayari wakati wowote kujiingiza katika vita vya DRC kwa lengo la kumsaidia Joseph Kabila dhidi ya waasi wa M23, chini ya mpango wowote(UN, SADC, AU au LIWALO NA LIWE)

Source:BBC
 
Kwa mara ya kwanza Tanzania kupitia Benard Membe imesema iko tayari wakati wowote kujiingiza katika vita vya DRC kwa lengo la kumsaidia Joseph Kabila dhidi ya waasi wa M23, chini ya mpango wowote.

Source:BBC

waanze kumuondoa kabila kwanza ambaye ni msaliti wa wakongoman
 
Membe anatakiwa kuchunga mdomo wake. Kwenye ulingo wa diplomasia kuna mambo ya kusema hadharani na kuna mengine unayasema ndani. Nahisi ambition ya Membe ya kuwa rais 2015 inaanza kuathiri utendaji wake wa kazi.
 
Safi sana askari wetu wanaoteana vitambi hawana kazi waende wakale jasho lao sasa
 
Amalize kwanza ya Malawi, Asijifanye USA ya Africa wakati uwezo hana.!
 
This wont be a wise move, why take sides while the region at least three presidents KABILA,KAGAME UNDER THE CHAIRMANSHIP OF MUSEVEN, have given the MOU, and agreement, and this evening news Kabila is ready to sit on round table for finding the amicable solutions.
Why now jump on taking sides.....!! LOOO.
 
Mbona hawakuingiza jeshi Libya kupambana na waasi waliomuua Gaddafi??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
DRC ni muhimu kiuchumi na usalama kwa Tz. Tusilalame kupinga kila kitu bila hoja za msingi.

Ni kweli kabisa Congo DR inachangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania mfano ujenzi wa barabara ya kutoka Tunduma - sumbawanga hadi kasanga port ziwa Tanganyika.Wacongo ndo waliosukuma ujenzi wake ili kupitisha mizigo yao nasi tutanufaika na barabara hiyo hasa vijiji vya pembezoni vilivyotelekezwa na CCM kwa muda mrefu.
 
Tanzania tuna interest ya Kabila kuwa raisi na hatuwezi kuwaachia magaidi wakamtoa kijana wetu wakati tuna nia, uwezo na sababu za kusaidia. Hakuna kuweka siri hawa magaidi wakijua jeshi la Tanzania lipo hawatarudia tena na kama wanataka mabadiliko wafuate siasa.

Vilevile ni lazima tuelewe hawa jamaa wamechukua East Congo ambako ndiko upande wetu na wanakwamisha biashara nyingi sana. Wakati wa kufikiria jeshi letu ni imani tu umekwisha kwani uchumi sasa si wa nchi pekee bali ni wa zone hivyo Congo inatuathiri kiuchumi pia
 
Tulienda Morocco kuzuia jamaa wa Alqaida kuchukua kule wakati wa George Bush na tukapewa $600B za barabara na umeme
 
Kwa mara ya kwanza Tanzania kupitia Benard Membe imesema iko tayari wakati wowote kujiingiza katika vita vya DRC kwa lengo la kumsaidia Joseph Kabila dhidi ya waasi wa M23, chini ya mpango wowote(UN, SADC, AU au LIWALO NA LIWE)

Source:BBC

Ili ni tatizo la kukosa busara. M23 wanataka kuwasaidia wa-Congo, Tanzania inataka kumsaidia m-Congo mmoja, Joseph Kabila!!! Hivi vita vya Kagera hatukujifunza tu kusaidia rafiki, Obote.

Kwanza huyo Joseph Kabila hana uraia wa Tanzania kweli, maanake ata JKT alihudhuria - operation vyama vingi pale Makutupola mwaka 1992?
 
hoja nnaunga mkono, ila tungeanza na kuwawekea vikwazo wale wote wanaounga mkono waasi!
 
Tanzania ikipeleka jeshi Kongo bi Joyce Banda karibu Tanzania waislamu tutakupa msaada kuchukua ziwa lote la Nyasa na hata ukitaka kuchukua kipande cha nchi kavu mpaka Mtwara.

Hatuoni sababu ya kuunga mkono jeshi letu kwenda Kongo huku serikali hiyo hiyo imepuuza madai yetu yote na hata masheikh kadhaa bado wako ndani ambapo msingi wa tuhuma dhidi yao ni madai ya waislamu.

Kwa upande mwengine jeshi litakalokwenda huko tutamuomba Mungu awapatie kipigo baada ya kipigo ikiwa si kutoka M23 basi janga baada ya janga kama vile Ebola au kipindupindu.

Tunajua kuwa hii ni kazi ya kutumwa kama ilivyokuwa kwa Uganda,Burundi na Kenya huko Somalia.Nchi hizo pamoja na kufanya kazi zilizotumwa lakini zinaambulia matusi na kejeli tu.Kwa akili zetu za kiafarika bado ziko mbioni kuitikia utumwa mwengine.

Kufanikiwa kwa jeshi huko DR of Congo tunajua itakuwa ni madhila mengine makubwa kwetu waislamu baada ya makampuni ya kiyahudi kudhibiti uchumi wote wa Kongo kwa msaada wa Tanzania.

Faida za kiuchumi kama matumizi ya bandari kupeleka mizigo huko wala si faida kitu kulinganisha na utu na imani zetu.Tumepata uzoefu wa hasara ambazo wenzetu wa Pakistan wamezipata kwa kusaidia kupitisha mizigo kupeleka Afghanistan.
 
Back
Top Bottom