Sioni chama cha ku-replace ccm, chadema ??
Suala siyo chama cha replace,ila ni mabadiliko yatakayobadili hali hii mbaya ya maisha!
Wana JF nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana kile kilichokuwa kinajiri kwenye nchi ya jamaa zetu wa kule Kaskazini mwa Afrika yaani TUNISIA. Jina la TUNISIA linafanana kwa namna jina la Tanzania lilivokaa yaani TANZANIA. Zote zinaanza na "T" na kumalizia''A''
SIfamojawapo ya marais wa nchi zote mbili ni WAISLAMU.
Tunisia imekumbwa na mgogoro wa kisiasa ULIOSABABISHWA NA MAANDAMANO YA WANANCHI WAKILAMIMIKIA MAMBO MUHIMU YA MAISHA yakiwa ni pamoja na:Baada ya Wa-Tunisia kuanzisha maandamano kupinga hali hizo tatu muhimu,KAMA KAWAIDA YA UTAWALA DHALIMU POLISI WALIANZA KUZUIA MAANDAMANO KWA NGUVU IKIWEMO KUTUMIA RISASI ZA MOTO iliyopelekea watu karibia 200 kupoteza maisha.
- Kupanda kwa gharama za Maisha.
- Ukosefu wa Ajira.
- Rushwa na Ufisadi uliokithiri mipaka.
Baada ya mauaji Rais ZINE el BEN aliamua kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya ndani. Bado haikusaidia kitu maandamano yakawa yako palepale,Rais akaamua kulihutubia Taifa kwa njia ya TV akiahidi kupunguza gharama za vitu na kuongeza ajira,bado Watunisia hawakumwelewa. Jana Ijumaa 15/01/2011 Zine Ben Ali AKAAMUA KUMWAGA MANYANGA, NCHI IMEMSHINDA NA HAITWALIKI.
Rais huyu ameitawala Tunisia kwa zaidi ya miongo 2(23 years). Jana amekimbia nchi maana imemshinda. Huyu Rais ana tuhumiwa kuwa MARA TU BAADA YA KUINGIA MADARAKANI ALIANZISHA SERA YA UGENISHAJI(UBINAFSISHAJI) na akaanza kuyauza Mkampuni na Mashirika ya Umma kwa kasi ya ajabu HUKU YEYE MWENYEWE AKIMTUMIA MKEWE KUJINUFAISHA NA UGENISHAJI HUO.
LESSON: Haya matukio ya Tunisia yana shabihiana kabisa na KILE KINACHOENDELEA HAPA kwetu Tanzania. Kwamba Watawala wetu hawa CCM wanatakiwa haya Matukio ya Tunisia wayachukulie kwa umakini mkubwa. Kwani kilichotokea TUNISIA CHAWEZA PIA KIKATOKEA HAPA TZ KIRAHISI KABISA NA CCM WAKAMWAGA MANYANGA.
Hali zote zilizosababisha Rais wa Tunisia hata hapa TANZANIA zipo na ziko wazi kabisa. Kwa hiyo ni swala la muda tu. MUDA UTAKAPOFIKA POLISI WATAFANYA MADUDU YAO KAMA WALIVOFANYA ARUSHA. HAPO NDIPO NCHI NZIMA ITAKAPOWAKA MOTO. Hakuna kifaru wala RISASI itazuia UMMA UKIAMUA KUING'OA SERIKALI KWA MAANDAMANO.
Kwa hiyo CCM kaeni mkao wa kula. Vuguvugu limeshaanza. Kikwete get prepared for the IKULU EXIT unless you change the situation.
Hali ya Ufisadi bado inazidi kuitesa na kuinyanyasa CCM na serikali yake. Huo ndiyo ukweli.Hizi zote ni dalili mbaya sana kwa serikali iliyoko mamlakani. Kwa hiyo nasema CCM get prepared,the time is nigh! SOMO LIMESHATOLEWA NA WANANCHI WA TUNISIA. Who will be next??
- SERIKALI YA CCM TAYARI MMESHAUA HUKO ARUSHA.
- PESA YA KUILIPA DOWANS(RICHMOND) INATAYARISHWA.
- EWURA TAYARI WAMESHAPANDISHA UMEME BAADA YA KUWAPA BARAKA ZAKO.
- PETROL/DIESEL IMEKUWA IKIPANDA KILA SIKU.
- THAMANI YA SHILINGI INAZIDI KUPOROMOKA NA HUJACHUKUA HATUA YOYOTE.
- MIGOMO VYUO VIKUU IMEANZA KUTIKISA NCHI UDOM,UDSM na kwingineko.
Lazima kuwe na sera na mikakati baada ya mabadiliko sio kuleta mabadiliko baade hakuna dira, mikakati na strategy kwa nza ya ku-replace maisha ya sasa
It takes courage for which we Tanzanians are lacking!
ndio tusiowataka nyinyi na mitazamo yenu kwani nani hajui kimetokea nini tunisiaHivi mnajua kilichotokea Tunisia au mnapiga makelele tu nasie twataka ? Yaani hiyo habari yote hapo juu itawauza kwa bei rahisi kabisa maana hakuna cha kweli kilichoandikwa na ambacho kiliwasha moto wa mabadiliko ya Tunisia na kilichotokea.
Ndugu zanguni kilichojiri Tunisia ambacho hakikuelezwa hapo ni kisa kidogo sana na ambacho hapa kwetu imekuwa ni tukio la kawaida,kama umewahi kusikia hawa jamaa zetu wamachinga wauzao bidhaa zao bila ya kuwa kibali au sehemu maalum ya kufanyia biashala zao,mgambo au asikari wa tunisia walimwagia jamaa mbogamboga zake zikiwemo nyanya na bidhaa zingine wakimtuhumu kuwa akiuza bila ya kibali (machinga kwa hapa kwetu) ,jamaa alichezea kisago kitakatifu cha mgambo hao ila baada ya kumaliza ,jamaa alijiwasha moto na kufariki ,hapo ndipo cheche zilipoanza na habari zake kuenea kama moto wa nyasi huku zikiwapandisha wananchi mori wa kuisakama serikali na hadi hapa tulipofikia raisi ameshakimbia nchi na jamaa wanasema haitoshi wale waliomzunguka wote nao waondoke. Mnayaweza ? Hivi Kikwete aliwafukuza watu huko vijijini si mliwapokea kwa zulia jekundu au si kweli ? Wacheni longolongo zenu.
yes! We can
Matatizo ya Kenya Ivory Cost Tunisia Zimbabwe you name it........yote yanafanana ni udikteta, viongozi wengi hawapendi kuachia madaraka akiwemo Kikwete.Matatizo ya Tunisia unayajua vizuri lakini? Kabla ya Tunisia walisema ifanyike kama Kenya, then kama Ivory Coast... na sasa Tunisia!
wana JF na watanzania kwa ujumla nina wazo ambalo naweza kusema kuwa tuatakuwa tumetatua matatizo mengi sana katika nchi yetu hii.
Mimi binafsi nimependa sana walichofanya watunisia ..... Hivi sisi hatuwezi fanya kitu kinachofanana na hicho? Maana Nchi hii siielewi kabisa kama vile hakuna Raisi au Waziri wa mambo ya ndani.
Mambo yanafanykia kienyeji sana kila mtu anatoa tamko wenye nchi wamekaa kimya sasa hii nchi au jalala?????
Hebu tuone mbinu waliyo tumia watunis nasi tu transfer hiyo mbinu jamani.
Sijawahi kuona utawala wa hovyoo kama utwala wa awamu hii ya mwisho ya JK naona mpaka ipite miaka miwili hivi tweweza fanya waliyo fanya watunis.
Tafakarini wana JF na WaTZ wote.
Nawasilisha ni mawazo tuuuuuu.....