- Lakini at the same token inasemekana alifukuzwa nchini na awamu ya kwanza, sasa nani ni mkweli? Maaana mimi maisha yangu yote utottoni nakumbuka alikua akiiishi Kenya alirudi pale tu siasa zetu zilipobadlika, sasa mkuu unafikiri ni kwa nini?
William @ NYC, USA.
Mbona unazunguka tu hutuelezi nani alimfukuza , na kwa nini? Au wewe una bifu na serikali ya awamu ya kwanza? Maana watu wamequote kwamba huyu mtu alitumiwa na Nyerere enzi hizo hata akaweza kumkamata Mwijage kule Swaziland. Hili hujakanusha , ila anapiga blah blah za kwamba alifukuzwa nchini. Na nakumbuka kwenye kile kitabu cha mwijage, alieleza jinsi huyu bwana alivyokuwa karibu na usalama wa Taifa, huku akitumia Bhalaghashia yake na unajimu kuonekana mtu safi , na hivyo kuwanasa watu mitegoni kiurahisi.
Ni sio siri, baada ya kujua ukweli ule wa Mwijage, yeye Shehe Yahaya hajawahi kupinga hilio. Tena basi, ndipo wengi tukaanza kumshuku huyu mtu na umeona jinsi alivyopuuzwa kwenye utabiri wake mwaka 2010. Aliposema Mgombea mmojawapo kati ya CHADEMA na CCM atakufa kabla ya uchaguzi, watu wakamshambulia, na matokeo yake akashindwa kukamilisha consipiracy yake. Slaa na Kikwete bado wanaishi. Hapo ndo alipoumbuka, kwani sasa akajitokeza waziwazi kwamba unajimu wake ulikuwa wa kisanii na alikuwa anatumia well calculated figures kutoka intelligency mbalimbali duniani kutoa utabiri wake. Tumeona alivyokubali mwenyewe kuwa anamlinda JK kwa majini yake. Sasa tukisema alikuwa msanii unabisha nini? Huyu mtu alikuwa ni sawa na assassin wengine wengi tu kama Carlos the Jackal, maana alikuwa anaandaa akili za watu kupokea matukio ya maangamizi in advance kwa "utabiri" wake wa kuelezwa mikakati na usalama wa viongozi.....
Tunaomba ueleze ni nani alimfukuza nchini, na ni nani alimrejesha pia....