Mkuu wangu Bulga ndio Oatmeal isipokuwa oatmeal inakuwa precooked kama unga wa mahindi tunaopata kutoka Mexico upo ambao ni pre cooked.Nilipoona mara ya kwanza nilifikiri Oatmeal ndiyo ile tuliyokuwa tunapata lunch tuliyozoea kuiita bulga, lakini kwa uchunguzi zaidi ni tofauti maana Oatmeal maji moto yanatosha kuchanganya mkoroga na mlo umekamilika, lakini ile bulga ilihitajika kupikwa kweli kweli kwa wenye miraba minne kuchochea kuni. Na ukila mtu wajisikia umetulia class room ya extended, upper primary, na hata kule secondary level education.
Unimekumbusha niwapate hawa wa USAID niwaulizie ile kitu iko wapi, maana wanafunzi na wanachuo wa siku hizi wakiipata ile hata maandamano yatatoweka.
Halafu ktk majadiliano haya ni muhimu tuingize vitu vya maana kama hivi kwani nilitaka tu kuongezea kwa nini haswa serikali yetu iliposisitiza KILIMO KWANZA haikuchukulia kipaumbele kilimo cha ngano badala ya mahindi kwani ngano unaweza tengenza vyakula vingi toka mikate, chapati, keki, mandazi (donuts), pasta na vyakula vyote vya Kitaliani wakati mahindi ndio Ugali tu, na kilimo chake kingeweza kulimwa na wananchi wenye mashamba madogo madogo.