Tanzania hatuhitaji Katiba kabisa, tunahitaji usimamizi wa sheria zilizopo tu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,909
51,904
Watu wamekuwa wakipiga kelele kila kona kuwa Tanzania inahitaji katiba mpya.Ziko nchi duniani hazina katiba kabisa.Mojawapo ni Uingereza.Haijawahi kuwa na katiba na haina katiba kabisa.Wanaishi kwa uttawala wa sheria tu.Kila mtu anakuwa mtii kwa sheria zilizopo basi.

Tanzania tuna sheria za kila kitu.
Ukiongelea bunge kuna sheria zake.Ukiongelea haki za binadamu kuna sheria za haki za binadamu zipo.UKiongelea uhuru wa habari ziko sheria za habari.Ukiongelea sheria za ajira zipo.Ukiongelea uchaguzi.Ziko sheria za uchaguzi.

Ukiongelea maadili wala huhitaji kuweka mambo ya maadili ya viongozi kwenye katiba kuna sheria ipo na kamishina wa maadili yupo.

Sasa kama zipo sheria zote hilo likatiba la kitu gani? Kinachotakiwa ni sheria zilizopo kusimamiwa basi hakuna haja ya kupoteza pesa kuhangaikia hilo dude linaloitwa katiba.Tuige nchi zisizokuwa na katiba

Tanzania inahitaji utawala wa sheria sio utawala wa katiba.
 
NADHANI ULIPASWA KUULIZA UMUHIMU WA KATIBA KABLA HUJATOA MAONI YAKO. KWANI INAONYESHA HUJUI UMUHIMU WA KATIBA. KATIBA NDIO INAHALALISHA SHERIA NYINGINE. HIZO SHERIA ULIZOZITAJA ZINAPATA UHALALI WAKE KUTOKA KWENYE KATIBA. HIVYO BASI, KAMA KATIBA NI MBOVU NA HIZO SHERIA ZITAKUWA MBOVU.
KUNA UMUHIMU WA KUWA NA KATIBA ITAKAYO TENGENEZA MISINGI YA UTAWALA BORA, UTAWALA WA SHERIA NA DEMOKRASIA. KATIBA ITAKAYO WAPATIA NGUVU WANANCHI KATIKA KUAMUA JUU YA MAENDELEO YAO.
KATIBA ILIYOPO IMEFANYA MENGI, LAKINI BADO HAIJAYAFIKIA HAYO MAHITAJI YA MSINGI KWA KIASI KIKUBWA CHA KUTUFANYA TUSIDAI KATIBA MPYA.
 
KATIBA NDIO INAHALALISHA SHERIA NYINGINE. HIZO SHERIA ULIZOZITAJA ZINAPATA UHALALI WAKE KUTOKA KWENYE KATIBA.

Katiba inafaa zaidi kwenye Mashirika yasiyo ya kiserikali yasiyokuwa na sheria zao sio kwenye serikali ambayo ina sheria za kusimamia mambo yake

Mchakato wa kutengeneza sheria hautegemei katiba.Miswada ya sheria hutengenezwa na wataalamu waliobobea wa eneo husika na kupitiwa na wataalamu wa sheria kisha hupelekwa bungeni kujadiliwa na kupitishwa na kutiwa sahihi na raisi.
 
Itakuwaje akiingia Rais ambaye atatumia udhaifu wa katiba iliyo mbovu kuihujumu nchi? Ila sina shaka na uwezo wako maana hata kutofautisha Bilioni na Trilioni huwezi.
 
Watu wamekuwa wakipiga kelele kila kona kuwa Tanzania inahitaji katiba mpya.Ziko nchi duniani hazina katiba kabisa.Mojawapo ni Uingereza.Haijawahi kuwa na katiba na haina katiba kabisa.Wanaishi kwa uttawala wa sheria tu.Kila mtu anakuwa mtii kwa sheria zilizopo basi.

Tanzania tuna sheria za kila kitu.
Ukiongelea bunge kuna sheria zake.Ukiongelea haki za binadamu kuna sheria za haki za binadamu zipo.UKiongelea uhuru wa habari ziko sheria za habari.Ukiongelea sheria za ajira zipo.Ukiongelea uchaguzi.Ziko sheria za uchaguzi.

Ukiongelea maadili wala huhitaji kuweka mambo ya maadili ya viongozi kwenye katiba kuna sheria ipo na kamishina wa maadili yupo.

Sasa kama zipo sheria zote hilo likatiba la kitu gani? Kinachotakiwa ni sheria zilizopo kusimamiwa basi hakuna haja ya kupoteza pesa kuhangaikia hilo dude linaloitwa katiba.Tuige nchi zisizokuwa na katiba

Tanzania inahitaji utawala wa sheria sio utawala wa katiba.

Kumbe we ni mjinga kabisa
 
Itakuwaje akiingia Rais ambaye atatumia udhaifu wa katiba iliyo mbovu kuihujumu nchi? .
Angalia kipengele mfano cha viongozi kuwa na maadili hakimo kwenye katiba iliyopo lakini angalia majipu yanavyotumbuliwa kwa viongozi wakora wanavyoburuzwa mahakamani kwa sheria za uhujumu uchumi.

Hapo Sheria iko kazini sio katiba iko kazini!!! kwani katiba haina hicho kipengele !!!!
 
Ili kuwa na ufanisi inabidi Rais naye awe na mamlaka ya kuangaliwa utendaji wake,pia kuzuia Rais kuwa kama mungu mtu
 
Ili kuwa na ufanisi inabidi Rais naye awe na mamlaka ya kuangalia utendaji wake,pia kuzuia Rais kuwa kama mungu mtu

Hiyo ni kazi ya bunge.Bunge likiona utendaji wa Raisi hauridhishi linaweza piga kura ya kutokuwa na imani naye
 
NADHANI ULIPASWA KUULIZA UMUHIMU WA KATIBA KABLA HUJATOA MAONI YAKO. KWANI INAONYESHA HUJUI UMUHIMU WA KATIBA. KATIBA NDIO INAHALALISHA SHERIA NYINGINE. HIZO SHERIA ULIZOZITAJA ZINAPATA UHALALI WAKE KUTOKA KWENYE KATIBA. HIVYO BASI, KAMA KATIBA NI MBOVU NA HIZO SHERIA ZITAKUWA MBOVU.
KUNA UMUHIMU WA KUWA NA KATIBA ITAKAYO TENGENEZA MISINGI YA UTAWALA BORA, UTAWALA WA SHERIA NA DEMOKRASIA. KATIBA ITAKAYO WAPATIA NGUVU WANANCHI KATIKA KUAMUA JUU YA MAENDELEO YAO.
KATIBA ILIYOPO IMEFANYA MENGI, LAKINI BADO HAIJAYAFIKIA HAYO MAHITAJI YA MSINGI KWA KIASI KIKUBWA CHA KUTUFANYA TUSIDAI KATIBA MPYA.

Wewe ndiyo inaelekea haujui maana ya Katiba, Katiba ni karatasi tu ambayo imeandika jinsi jambo fulani linavyopaswa kufanywa na siyo zaidi ya hapo lkn mwisho wa siku unahitaji watu wa kuweza kuetekeleza kile kilichoandikwa kwenye hiyo karatasi!
Tatizo letu Waafrika tukijifunza kaneno basi tunajifanya ndiyo wataalamu klk hata wale walioanzisha, Katiba hata nyumbani kwako unayo sema labda haujaiandika tu ya jinsi wewe na familia yako mnavyoishi!

Hivyo Tanzania hatuhitaji Katiba mpya kwa tunayo tayari ila kama kuna ulazima wa maboresho ufanywe lkn siyo kupoteza fedha kuunda nyingine huwo ni upuuzi!
 
Ili kuwa na ufanisi inabidi Rais naye awe na mamlaka ya kuangalia utendaji wake,pia kuzuia Rais kuwa kama mungu mtu

Kwani kuna tatizo gani la Raisi kuwa kama Mungu mtu? Mwisho wa siku ni lazima kuwe na Kiongozi ambaye ndiyo mkubwa wa kila mtu, mbona nyumbani kwenu hausemi Baba yako ni Mungu mtu? Si anaamka asubuhi anatengewa maji ya kuoga, anapikiwa chakula, anawekewa mezani, anaondolewa vyombo anaoshewa vyombo, anafuliwa nguo, anapigiwa pasi, anasafishiwa nyumba, anatandikiwa kitanda, mpaka labda hata anaogeshwa na yeye kazi yake ni kutoa Amri tu na hakuna wa kupinga hapo nyumbani Je yeye ni mbona haumuiti Mungu mtu?
 
Watu wamekuwa wakipiga kelele kila kona kuwa Tanzania inahitaji katiba mpya.Ziko nchi duniani hazina katiba kabisa.Mojawapo ni Uingereza.Haijawahi kuwa na katiba na haina katiba kabisa.Wanaishi kwa uttawala wa sheria tu.Kila mtu anakuwa mtii kwa sheria zilizopo basi.

Tanzania tuna sheria za kila kitu.
Ukiongelea bunge kuna sheria zake.Ukiongelea haki za binadamu kuna sheria za haki za binadamu zipo.UKiongelea uhuru wa habari ziko sheria za habari.Ukiongelea sheria za ajira zipo.Ukiongelea uchaguzi.Ziko sheria za uchaguzi.

Ukiongelea maadili wala huhitaji kuweka mambo ya maadili ya viongozi kwenye katiba kuna sheria ipo na kamishina wa maadili yupo.

Sasa kama zipo sheria zote hilo likatiba la kitu gani? Kinachotakiwa ni sheria zilizopo kusimamiwa basi hakuna haja ya kupoteza pesa kuhangaikia hilo dude linaloitwa katiba.Tuige nchi zisizokuwa na katiba

Tanzania inahitaji utawala wa sheria sio utawala wa katiba.
The constitution call was/is for the power hungry individuals with their goons behind them singing the chorus without understanding the meaning. A common Tanzanian only needs better life not technical documents that most will become past tense without seeing. We need medicines in the hospital, easier ways of educating our kids, freedom to move without hinderance within our country and the like. FULL STOP.
 
maximum pumba,

leta rasimu ya warioba alafu compare and contrast na hii katiba yenu inayobeba majizi hapo ndiyo utajua tz inahitaji katiba mpya.
 
Itakuwaje akiingia Rais ambaye atatumia udhaifu wa katiba iliyo mbovu kuihujumu nchi? Ila sina shaka na uwezo wako maana hata kutofautisha Bilioni na Trilioni huwezi.
Unaweza kuwa na katiba nzuri halafu ukakosa viongozi wenye weledi wa kuisimamia. Nionavyo uwe na katiba nzuri au mbaya bila ya kuwa na viongozi wenye weledi na maono ni tutaishia kulalama.
 
Watu wamekuwa wakipiga kelele kila kona kuwa Tanzania inahitaji katiba mpya.Ziko nchi duniani hazina katiba kabisa.Mojawapo ni Uingereza.Haijawahi kuwa na katiba na haina katiba kabisa.Wanaishi kwa uttawala wa sheria tu.Kila mtu anakuwa mtii kwa sheria zilizopo basi.

Tanzania tuna sheria za kila kitu.
Ukiongelea bunge kuna sheria zake.Ukiongelea haki za binadamu kuna sheria za haki za binadamu zipo.UKiongelea uhuru wa habari ziko sheria za habari.Ukiongelea sheria za ajira zipo.Ukiongelea uchaguzi.Ziko sheria za uchaguzi.

Ukiongelea maadili wala huhitaji kuweka mambo ya maadili ya viongozi kwenye katiba kuna sheria ipo na kamishina wa maadili yupo.

Sasa kama zipo sheria zote hilo likatiba la kitu gani? Kinachotakiwa ni sheria zilizopo kusimamiwa basi hakuna haja ya kupoteza pesa kuhangaikia hilo dude linaloitwa katiba.Tuige nchi zisizokuwa na katiba

Tanzania inahitaji utawala wa sheria sio utawala wa katiba.
Nakubaliana na wewe kwa sababu hujui unachojaribu kukisema hapa! kumbe wewe juha kalulu huna habari kwamba Katiba ndio sheria mama?! Sasa kumbe bila sheria Mama/Msingi hizo unazotaka zisimamiwe zingetoka wapi?! Nenda jifunze hilo kwanza ndio urudi hapa uandike tena! Bs
 
Katiba ndio sheria mama

Sheria zote zinapotengenezwa ni independent.Hakuna sheria yenye baba wala mama.Uingereza wana sheria tu bila katiba sababu waamini kila sheria inajitegemea kuanzia kutungwa hadi kutumika.Hiyo inayoitwa sheria mama ni utapeli.
 
Usiishi kwa kukariri; hapa sio uingereza! The worlds two largest democracies; India na Marekani zina katiba na zote zilikuwa makoloni ya mwingereza lakini waliandika katiba badala ya kufuata utaratibu wa Waingereza ambao wana katiba ambayo haikuandikwa! Katiba ni dira kuu inayoelekeza sheria nyinginezo; katiba ni kabrasha lisiloepukika hususani kwa vinchi vyetu hivi visivyokuwa na taasisi imara! Ndio maana uliwaona wabunge wa ccm katika BMK walihangaika usiku na mchana kuhakikisha wanapata katiba inayolinda maslahi yao! Katiba ni muhimu lakini sio ile inayopendekezwa ya Six na Nyoka wa makengeza; hapana!!
 
Back
Top Bottom