Tanzania hakuna amani, Amani ipo kwa wenye mafwedha USWISI na New jersey

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Amani maana yake ni nini?

Amani maana yake ni kuwapumbaza watanzania ili mafisadi waibe pesa, wapore maliasili na kuficha nje ya nchi?

Amani ni watanzania kufa kwa kukosa huduma za afya??

Amani ni watanzania kukosa elimu?

Amani maana yake ni wananchi kufa na njaa?

Amani maana yake ni waalimu kutishwa?

Amani maana yake ni Dr. Ulimboka kutekwa na kuteswa?

Amani ni mauaji ya kisiasa? Mifano ipo tajeni RIP Nyerere, RIP Kolimba, RIP Amina CHifupa, RIP chacha wangwe ... a list goes on

Amani ni migomoooo

Amani ni kuficha kuficha hela za Watanzania huko South Africa, Dubai, Swiss

Hayo yote hapo juu ni matendo mabaya kuliko vita. Maana watanzania wanateseka, vijana wanateseka, wanahangaika, dada zetu wa vyuo vikuu wanateseka na njaa, dada zetu wanajiuza ili wasife njaa, je kama wanakwepa njaa na Je ukimwi?

CHonde chonde watanzania???

Tuungane tudai hela zetu uswisi, tusiwaachie CDMA na ZItTo peke yao.

Tunataka huduma bora za afya, elimu bora, mikopo ya elimu kwa watoto wa masikini hasa wakulima vijijini


Maandamano na migomo

Tuanze na wafanyakazi wote pamoja na waalimu na madokta

TUCTA mpoooo, PESA Ipooooo - FEDHA zipo Uswisi

Madokta mpoo, pesa ipoooo

Walimu mpooo, fedha ipooo

Wakulima tupooo

Je tuungane vipi?

Wito wa maandamanoooo, migomoooo
 
TZ kuna ukondoo, hakuna amani, na ndiyo maana wanatumia kila mbinu kunyamazisha wananchi wake, linapotokea gazeti la kuwafunua watu toka usingizini, kama Mwanahalisi, Govt inatumia mabavu yake kwa kutumia sheria kandamizi kulifungia! Wanapotokea wabunge machachari kama akina Lissu na Mnyika. akina Makinda, Lukuvi na Werema wanaamua kuzitafsiri kanuni za bunge watakavyo, ili mradi tu hoja za hivyo vichwa zisiwafikie wananchi, lakini wanasahau hakuna serikali ya mabavu iliwahi kudumu madarakani. waangalie mifano ya wenzao akina Idi Amin, Mobutu sese seko,Sani Abacha, Hosni Mubarak na Gadafi, wameishia wapi? Kama hawajaondolewa madarakani kwa aibu kubwa??!! Hata watawala wetu watambue jasho letu haliwezi kupotelea kwenye mabenki ya Uswisi, ingawa hadi hivi sasa wamejifanya mabubu kutotaka kutaja walioficha hayo mapesa Uswisi, lakini ili mradi mabilioni ya Sani Abacha yalirejeshwa Nigeria na mabilioni ya Mobutu nayo yalirejeshwa Congo, na wa-TZ tukiamua kukomaa kukomaa kwa nguvu zote, haya mapesa yetu kazima yatarejea!!!!
 
Na sisi watanzania tumewaachia wazalendo wachache wapiganie haki wenyewe, watanzania wengine hata kuwaunga mkono hatuna hata habari. Watawala wanajua huu udhaifu wa wananchi, ndo maana wanaendelea kutamba na kupora rasilimali za taifa na kodi zetu kuficha nje.

Ndo maana watu wanateswa, wanauawa, na kutishwa. sisi watanzania hatuamki.

Sababu nyingine ni kuwa mafisadi wametufunga kamba, ni ngumu kufungua.. ... Kamba yenyewe ni njaa kali, hali mbaya ya uchumi. Sasa unakuta uchumi wote na mapato wanachukua wao, mwananchi akiamka hana muda wa kufikiria na kutafakari siasa na ufisadi wa sisiem. Mwananchi akiamka anahangaika kutafuta walau mlo ama ada ya watoto. that is daily routine.

Kuthubutu: kama kila mtu atathubutu kujitoa angalau kwa siku 2 ama mpaka 5 kuandamana na migomo na hawa mafisadi wakatoka, hali itabadilika. Cha kufanya, kila siku mtu atenge angalau mia 200, then after 10 days, aweke stock ya msosi. Then siku ya mgomo na maandamano, itakuwa safi.

WHo to organize, how to coordinate people.

Usalama wa taifa - wale waaminifu/wazalendo na TUCTA na wanaharakati wanaweza kusaidia.

Wazungu wao wanapata mikopo kwa riba nafuuu kwa sababu fedha za mafisadi wameficha kule kwa riba sifuri. Hivyo hizo benki nchi kama Uswisi wanawawezesha wananchi wao kwa mikopo.

Nawasilisha.

Nipo tayari kujilipua kukomboa kizazi cha sasa na kijacho
 
Back
Top Bottom