kuberwa
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 570
- 125
Haiingii akilini kwamba Kenya wanaweza kuingia kwenye vita leo hii? Sidhani kuna any push factor to this extent mpaka wanaamua hivi! Na sidhani kama wana uchumi mzuri kiasi hicho wa kuafanya waende vitani leo hii! Nadhani huu ni mkakati mpya ambapo hata Tanzania inaweza kutumika siku moja. Imeonekana kuwa ni gharama sana kutumia vifaa vya kivita kutoka Ufaransa au Markani au kuleta wanajeshi Obvious, ni gharama kisiasa kwa mataifa haya na ni gharama hata kimahusiano maana tayari wanashutumiwa kwa mambo wanayoyafanya huko Libya na kwingineko. Sasa njia pekee ni kuwatumia majirani, kwa mkataba maalum.
Nikiangalia Historia ya Kenya na Somalia, bado hainiingii akilini kabisa. Na usisahau hao Al-Shabaab wakati mwingine wamekuwa wakiishi ndani ya Kenya na wakipanga mipango yao kutokea Kenya na hata baadhi ya Suply (bidhaa za matumizi) hupitia huko muhimu zaidi Mirungi (miraa) kutoka Kenya!
You may be interested on this link: allAfrica.com: Kenya: America Bans Kenyan Linked to Al-Shabaab
possible kabisa mkuu, maana hawa wamarekani wamekuwa vinara wa vita. Na most times wanapigana mbali na kwao hivyo miundombinu na wananchi wao hawadhuriki kamwe except wanajeshi. Wamejenga kambi za kijeshi all over prime areas ili waweze kudictate... Kwa uono wangu nahisi Afrika mashariki tumeingiliwa kwa janja hii. Soon watajenga kambi kwenye eneo hili ili watumalize kwani eneo halitakalika... Eeh Mungu tunusuru na fitna hii. Amin