''...Tanzania haitakalika''

Hao waliolipa na kurudi chuoni wametoka wapi? Je wao sio watanzania? Unapaswa kelewa kuwa kuna watanzania wa uwezo tofauti tofauti na msimamo wa serikali ni kuwasaidia wale wanaoshindwa, kama wewe ulivyoshindwa na ikakusaidia. Ninachopinga mimi ni kulazimishana kuamini kuwa watanzania wote hawawezi kujlipia.

Ndugu yangu, watanzania walio wengi wanamaisha duni, kipato chini ya dola moja...ukiangalia kwa makini suala hili tunataka kujenga tabaka la masikini na wenye nacho, serikali haishindwi kuwalipia hao wasio na uwezo, angalia ni kiasi gani tunateketeza pato la taifa kwa mambo yasiyo na msingi? Ufisadi ? chaguzi? the list is very wrong...wenye uwezo sawa wachangie wale akina Kayumba nao???
 
Jawabu ni kulipia elimu ya juu! Watz tumekuwa watu wa kulalamika mno!

Dawa ya deni ni kulipa..hata kama inabidi ukope!!!
 
Tupende tusipende elimu ya bure ilikwisha na utawala wa Mwalimu, wakati huo wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu walikuwa hawajai kiganjanjani.Leo vyuo vikuu tele, na wanafunzi tele na wote wanataka kusomeshwa na kodi ya wananchi.
Sioni hilo likitendeka leo au kesho.
Tatizo la serikali ni kutolifafanua hili kuwa kuwasomesha watu bure kumefikia mwisho, wawe ni watoto wa wa mkulima ,mafanyakazi au kibopa.
Sasa hivi kinachofanyika ni ujanja ujanja tu wa wanafunzi wengine wapewe mikopo na wengine wakose.Sera ya kuwa kila mwanafunzi lazima alipie karo ianzishwe na muundo wa mikopo usioeleweka sasa usitishwe.Nchi nyingine kuna mtindo wa scholarship kwa category fulani ya wanafunzi waliofanya vizuri sana na ambao serikali inaona umuhimu wa kuwa retain kwa kuwalipia ili wawe wataalam/viongozi wa nchi.
Hapa criteria ni performance tu na hii inaongeza ushindani katika elimu.

Exactly my sentiments!!!! Na ndio mfumo uliokuwa unatumika miaka yote mpaka ilipokuja hii bodi ya mikopo na mambo shaghalabaghala ya 40%, 60% and 100%.

Criteria ya kutoa udhamini kwa mwanafunzi dunia nzima ni moja tu, kufaulu vizuri! Serikali itoe mikopo na udhamini kwa wanafunzi waliofaulu vizuri bila kujali mtoto wa mkulima au wa tajiri. Haiingii akilini eti kwa sababu mimi baba yangu ana uwezo wa kifedha halafu nimefaulu vizuri ninyimwe mkopo kisa nilisoma Academy.

Hapo bodi ya mikopo inajiongezea kazi ya kufanya mchakato wa nani alipiwe na nani aachwe. Ni vigumu sana kuchanganua vipato vya Watanzania!

Serikali isomeshe wanafunzi kwa 100% kwa kuzingati viwango vyao vya kufaulu mpaka pale uwezo wake unapoishia!
 
Ndugu yangu, watanzania walio wengi wanamaisha duni, kipato chini ya dola moja...ukiangalia kwa makini suala hili tunataka kujenga tabaka la masikini na wenye nacho, serikali haishindwi kuwalipia hao wasio na uwezo, angalia ni kiasi gani tunateketeza pato la taifa kwa mambo yasiyo na msingi? Ufisadi ? chaguzi? the list is very wrong...wenye uwezo sawa wachangie wale akina Kayumba nao???

Ushirombo mimi sikatai kuwepo kwa masikini, lakini ninakuhitaji na wewe utambue tofauti zilizopo. Kama uko Tanzania ukipata muda nenda kakae mtoni kwa aziz ali pembeni ya barabara. Angalia magari yanayopita na watu walioyapanda. Halafu nenda sarenda bridge, angalia magari na waliomo kwenye magari hayo. Labda hii itakusaidia kutambua kuwa kugoma ili kila mwanafunzi akopeshwa asilimia 100 kwa madai kuwa watanzania ni masikini sio jambo la busara.
 
Siku zote ukiwa na uongozi wa DARUSO usiokuwa makini lazima kutokee migomo....

Wale waliosoma wakati SWEKE kutoka Engineering na KITILA MKUMBO kutoka science kama sikosei wakiwa maraisi wa DARUSO... watakubaliana na mimi kwamba makubwa yalifanyika bila kuwa na migomo isiyokuwa na kichwa wala miguu...

Kwa mfano nilisikitishwa sana na wanafunzi kugoma kwa sababu ya cost sharing policy...I support the policy kwa 100%...Tatizo lao lilikuwa ufanisi wa Board ya Mikopo kutambua nani tajiri na nani maskini hilo ndio tatizo tu... hakuna lingine ... cost sharing must be there... kwa kuwa hata kwenye afya na maji ipo pia.

Board ya mikopo pia inashindwa kujua nani tajiri nani maskini kwa sababu watanzania hawawezi ku-be-identified.. yaaani hawana vitambulisho vya kitaifa (National Identity Card) ambavyo vinginetunza database, ingekuwa rahisi kujua baba yako anafanya kazi gani? analipa kodi kiasi gani, na pato lake la mwaka kiasi gani? Bila hilo hata board ya mikopo inalaumia kijinga tu.

Kibaya solution za wasomi ziko kama za watu ambao hawajaona hata darasa moja na kwa namna wanavyofanya kweli mlimani hakukaliki na wala sio nchi haikaliki.
 
Kichwangumu unaongea theory nyngi lakini practice iko tofauti na hizo theory. Ukimleta mwanafunzi aliyepeleka hati ya nyumba bodi ya mikopo mlete hapa. Hakuna mtu anayelazimishwa kupeleka hati ya nyumba ili apewe mkopo. wala hakuna collateral yoyote inayohitajika ili kuidhinisha mkopo.
Wanafunzi hawa hawapingi utekelezaji, wanapinga sera. wao wanataka flat rate 100% kwa wanafunzi wote na sera haisemi hivyo.

Jibu hoja nzima don jump to what you believe. Huo nimetoa kama mfano tu nothing to do with preparation before implementation of the policy
 
Hao waliolipa na kurudi chuoni wametoka wapi? Je wao sio watanzania? Unapaswa kelewa kuwa kuna watanzania wa uwezo tofauti tofauti na msimamo wa serikali ni kuwasaidia wale wanaoshindwa, kama wewe ulivyoshindwa na ikakusaidia. Ninachopinga mimi ni kulazimishana kuamini kuwa watanzania wote hawawezi kujlipia.

Kwahiyo ambao hawajalipa ni masikini na ambao wamelipa wanauwezo hivyo basi serikali itawapa asilimia 100% hawa ambao hawajalipa?

Jamani tunapochangia tuwe tunapambanua tofauti ya maisha ya watanzania (ya juu, ya kati, ya chini, na ya chini zaidi) na yako wewe unaechangia maada hii. Unaweza ukawa unaandika kwa kujiangalia wewe, bila wewe kujijuwa kuwa unajiangalia wewe (Favored alternative)
 
Exactly my sentiments!!!! Na ndio mfumo uliokuwa unatumika miaka yote mpaka ilipokuja hii bodi ya mikopo na mambo shaghalabaghala ya 40%, 60% and 100%.

Criteria ya kutoa udhamini kwa mwanafunzi dunia nzima ni moja tu, kufaulu vizuri! Serikali itoe mikopo na udhamini kwa wanafunzi waliofaulu vizuri bila kujali mtoto wa mkulima au wa tajiri. Haiingii akilini eti kwa sababu mimi baba yangu ana uwezo wa kifedha halafu nimefaulu vizuri ninyimwe mkopo kisa nilisoma Academy.

Serikali isomeshe wanafunzi kwa 100% kwa kuzingati viwango vyao vya kufaulu mpaka pale uwezo wake unapoishia!

Umesahau kuwa kabla ya kuja kwa Bodi ya mikopo wanafunzi waliosoma kwenye vyuo binafsi kama Tumaini na vingine hawakupewa msaada wowote na serikali.Unadhani ni sahihi kwa serikali kutowasaidia wanafunzi wa Tumaini, SAUT, MUM, IMTU, Kairuki etc. ? Au unadhani walioenroll kwenye hivyo vyuo hawajafaulu???
 
Njia muafaka kabisa ya kumtawala mtu ni kumnyima elimu na kuziba midomo ya wanaotetea wanyonge. Bado tunaona tatizo kwenye jamii yetu, wale wanaostahili kukamatwa na kuzuiliwa na polisi(mafisadi wa EPA na Richmond) wapo wanapeta, lakini wanafunzi wa chuo waliojaribu kupigania maendelea ya elimu ya watanzania wanyonge na wasio watoto wa vigogo ndio wako chini ya ulinzi wa FFU. Hii ni TZ.
 
Kwahiyo ambao hawajalipa ni masikini na ambao wamelipa wanauwezo hivyo basi serikali itawapa asilimia 100% hawa ambao hawajalipa?

Hilo limeelezewa wazi na waziri. Wale wote walioshindwa kulipa wapeleke appeal wizarani for reassessment. Assessment hiyo ndio itatoa jibu kama walipiwe 100% au la. Sera kama ilivyo inamconsider kila mtanzania. wanaofanya utekelezaji uwe mgumu ni wanafunzi wanaotoa taarifa zisizo sahihi. Hivyo basi adui wa mwanafunzi masikini ni mwanafunzi mwenye uwezo aliyedanganya kuwa hana uwezo.Tatizo si sera.
 
Umesahau kuwa kabla ya kuja kwa Bodi ya mikopo wanafunzi waliosoma kwenye vyuo binafsi kama Tumaini na vingine hawakupewa msaada wowote na serikali.Unadhani ni sahihi kwa serikali kutowasaidia wanafunzi wa Tumaini, SAUT, MUM, IMTU, Kairuki etc. ? Au unadhani walioenroll kwenye hivyo vyuo hawajafaulu???

Hoja yangu ya hapa ni kufaulu na kupata admission kwenye Chuo chochote kile kinachotambilika, kiwe cha serikali ya cha binafsi. Ila viwango vya kufaulu ndicho kiwe kigezo cha kumpa mwanafunzi mkopo na si kipato chake! Hayo mambo ya kutathmini uwezo wa kifedha wa mzazi/mlezi wa mwanafunzi ili kujua anaweza kuchangia kiasi gani yanatuletea matatizo makubwa.

Kumbuka wakati bodi inaanza, critea zilikuwa wazi mno.

1. Div I - wavulana
2. Div i and II - wasichana
3. Wote waliopata admission ya kusomea ualimu kwenye vyuo vikuu na vingine vya elimu ya juu
4. Wote waliopata admission ya kusomea udaktari kwenye vyuo vyote vikuu.
5. Wote waliopata admission ya kusomea Kilimo (SUA wote wanapata mikopo)
6. Wote waliopata admission ya kusomea masomo ya Sayansi Asilia (sio ya jamii au siasa).

Vigezo hivi vikizingatiwa na serikali ikatoa mikopo kwa asilimia 100% migogoro yote hii itaisha! Ila tu warekebishe kipengele cha kufaulu kwa wavulana na kuweka usawa, wote wenye Div one and two kwa wavulana na wasichana wadhaminiwe na serikali kwa njia ya mikopo. FULL STOP!!!
 
Hoja yangu ya hapa ni kufaulu na kupata admission kwenye Chuo chochote kile kinachotambilika, kiwe cha serikali ya cha binafsi. Ila viwango vya kufaulu ndicho kiwe kigezo cha kumpa mwanafunzi mkopo na si kipato chake! Hayo mambo ya kutathmini uwezo wa kifedha wa mzazi/mlezi wa mwanafunzi ili kujua anaweza kuchangia kiasi gani yanatuletea matatizo makubwa.

Mkopo sio zawadi. Lengo la mkopo ni kuwawezesha wale wasiafford kujilia waweze kusoma. Unaposema mkopo utolewe based on exams results utakuwa sahihi iwapo tu waliofaulu wote watashindwa kujilipia. Iwapo mtu amefaulu na anauwezo wa kujilipia kwa nini umkopeshe. Kumbuka huu ni mkopo sio zawadi.
 
Hilo limeelezewa wazi na waziri. Wale wote walioshindwa kulipa wapeleke appeal wizarani for reassessment. Assessment hiyo ndio itatoa jibu kama walipiwe 100% au la. Sera kama ilivyo inamconsider kila mtanzania. wanaofanya utekelezaji uwe mgumu ni wanafunzi wanaotoa taarifa zisizo sahihi. Hivyo basi adui wa mwanafunzi masikini ni mwanafunzi mwenye uwezo aliyedanganya kuwa hana uwezo.Tatizo si sera.

Hiyo Wizara na huyo Waziri wanoongea kwenye vyombo vya habari ili kujikosha unawaamini sana eeeeh?

Watasota hapo Wizarani na majibu yake kila siku yatakuwa "suala lenu bado linashughulikiwa"!
Mtu katoka Bukoba na Dar hana ndugu unategemea aishije?

Ama kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa!
 
Yes, serikali uwezo wake mdogo sana.
Mashangingi ya bei mbaya 700 kwa mwaka mmoja. Kukodisha ndege mbovu za ATCL, zilizopelekwa Kiwira kimya kimya, za safari, za vikao, washa, seminar, kongamano................ Kweli serikali uwezo wake mdogo, AMEN!!

na ni serikali hiyohiyo inayojenga barabara nchini kote, inajipinda kupeleka maji na umeme vijijini, imejenga shule kila kata, inatarajia kujenga zahanati kila kata huku ikipambana na wakwepa kodi... AMEN
 
Hilo limeelezewa wazi na waziri. Wale wote walioshindwa kulipa wapeleke appeal wizarani for reassessment. Assessment hiyo ndio itatoa jibu kama walipiwe 100% au la. Sera kama ilivyo inamconsider kila mtanzania. wanaofanya utekelezaji uwe mgumu ni wanafunzi wanaotoa taarifa zisizo sahihi. Hivyo basi adui wa mwanafunzi masikini ni mwanafunzi mwenye uwezo aliyedanganya kuwa hana uwezo.Tatizo si sera.

Nani mwenye wajibu wa kusema huyu kadanganya au hajadanganya? Mimi au wewe au serikali(bodi)?
 
Mkopo sio zawadi. Lengo la mkopo ni kuwawezesha wale wasiafford kujilia waweze kusoma. Unaposema mkopo utolewe based on exams results utakuwa sahihi iwapo tu waliofaulu wote watashindwa kujilipia. Iwapo mtu amefaulu na anauwezo wa kujilipia kwa nini umkopeshe. Kumbuka huu ni mkopo sio zawadi.

Tatizo ni jinsi ya kumjua aliyefaulu na hana uwezo wa kujilipia na yule aliyefaulu na ana uwezo wa kujilipia. Ukitaka kufanya zoezi hilo kwa ufanisi unahitaji nyenzo za kisasa na wataalamu walibobea ambao bodi hawana!

Pia gharama zake zinaweza kuwa kubwa, na tatu inaongeza administrative issues kwa bodi. Ili bodi ifanye kazi kwa ufanisi, inatakiwa kuweka vigezo vilivyo rahisi na ambavyo viko straight forward ili kuondokana na matatizo kama haya ya sasa hivi!
 
Serikali na Chuo wanatumia vigezo gani kujua kina nani wana uwezo na kina nani hawana uwezo?

kuna form ambayo hujazwa na wanafunzi. form ina vipengele vinavouliza in detail kuhusu hali ya uchumi. Hii form inatakiwa kuwa endorsed na uongozi wa mtaa anaoishi mwombaji then kata na mahakama. Bodi, theoretically, inahakiki usahihi wa taarifa hizo.
 
Board ya mikopo pia inashindwa kujua nani tajiri nani maskini kwa sababu watanzania hawawezi ku-be-identified.. yaaani hawana vitambulisho vya kitaifa (National Identity Card) ambavyo vinginetunza database, ingekuwa rahisi kujua baba yako anafanya kazi gani? analipa kodi kiasi gani, na pato lake la mwaka kiasi gani? Bila hilo hata board ya mikopo inalaumia kijinga tu.

Hapa ndo pakuanzia pia ziwe na connection with any bank infos, land owership, fixed and mobile assets.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom