''...Tanzania haitakalika''

Sera ya nchi ni kwamba masikini watasaidiwa kwa kupewa asilimia ya mkopo wanayohitaji na tajiri atajilipia mwenyewe. Hiki ndio wanachokipinga hawa wanafunzi kwa madai kwamba watanzania wote ni maskini hivyo wote wapewe asilimia 100 ya mkopo. sasa anaposema wanaorudishwa ni matajiri anajichanganya mwenyewe, kama anajua kuna matajiri kwa nini aliongoza mgomo wa kutaka wanafunzi wote wapewe mkopo asilimi 100%? Hiyo maana ulizoweka hapo ni yako wewe, angetaka ieleweke hivyo angeelezea explicitly.

ZeMarco,
Nyerere aliposhambuliwa kuwa enzi zake alikuwa anaweza mawaziri wote kwenye baraza lake la Mawaziri wa dhehebu la Kikristo, unajua alijibu vipi?
"....... wanasema mimi nilikuwa naweza WAKATOLIKI wenzangu kwenye baraza la mawaziri. Wakati huo Wakatoliki tuko watatu, mimi .... na ..... (jina nimesahau) na mwisho ni George Kahama ambaye alikuwa na wake 2.......".
Nafikiri DARUSO hawakuwa wajinga kugoma halafu leo hii walalamike kuwa hii system inasaidia tu wale walionazo. Jana nimesoma kuwa wale wasio na uwezo waandike barua kwa Waziri. Sasa barua ya nini wakati mambo ni mazuri kabisa kama wewe unavyoidai? Mbona umekaa na mambo ya kulazimisha tuamini jambo lenye utata? Duuu, Makatibu kata wengi dunia hii....
 
1. Hakuna elimu ya juu ya bure na hizi sii enzi za ujamaa..ambapo wanafunzi vyou vikuu walikuwa wachache sana na serikali iliweza kuwagharamia bure!
2. Ni jukumu la jamii kuwa na mikakati kuwasomesha watu wake..mbona pesa ya arusi tunaweza kuchanga mamilioni?
3. Ukiangalia Kenya mfano- wanaopewa mikopo ni asilimia ndogo sana..wengi ni wazazi au michango ya harambee inawasomesha hata tena Ulaya!
4. Mimi naona Tz tutazoea tu taratibu...it will take time...ila huo ndiyo ukweli!
5. Tanzania sii nchi maskini kuwasomesha watoto wetu tuliowazaa wenyewe...tunakosa tu vision na we dont keep our priorities right!
 
Ameongea ukweli kwani nchi haijatulia kabisa
Wazee wastaafu wa EAC waligoma hadi wakazuia barabara
Walimu nao waligoma
Wanafuzi nyuo vya juu karibu vyote vimefungwa
Kuna wananchi walivamia mgodi hivi karibuni
Jamaa wa mafuta waligoma kushusha bei ya mafuta

Kwa matukio kama hayo we unaona nchi iko salama?
 
Hawa-appreciate the fact kwamba serikali, kwa kuona uwezo wake mdogo wa kugharamia elimu, imeamua kuwaangalia waanafunzi wasio na uwezo kupitia sera hiyo, ili wale wenye uwezo watoe nafasi kwa wasio na uwezo kulipiwa na serikali. Huu ni ubaguzi wa aina gani? Je, kutaka matajiri na masikini wote walipiwe 100% huko si kuwanyanyasa wasio na uwezo?
Mkuu wangu,

Kauli za "Serikali haina uwezo" nadhani ni za kufutwa vichwani mwetu. Tusikubali kumeza tu! Uwezo wa kuwasomesha tunao... Tena sana tu.

Mkuu wangu nakumbuka mwaka 2000 yalinikuta haya. YES, yawezekana kiakili nilikuwa sijakomaa lakini kamwe sijilaumu kujiingiza katika mgomo ule!

Kuna mapungufu ya vijana wetu ambayo nakiri ni elimu wanayopewa ambayo aidha inawakosesha uzalendo au haikidhi mahitaji ya jamii yetu lakini kusema kuwa serikali haina uwezo wa kuwasomesha vijana wake elimu ya Juu bado kwangu naona si sahihi. Serikali inaweza, ikiangalia sehemu zinazostahili vipaumbele na kuzipa haki yake.
 
Ameongea ukweli kwani nchi haijatulia kabisa
Wazee wastaafu wa EAC waligoma hadi wakazuia barabara
Walimu nao waligoma
Wanafuzi nyuo vya juu karibu vyote vimefungwa
Kuna wananchi walivamia mgodi hivi karibuni
Jamaa wa mafuta waligoma kushusha bei ya mafuta

Kwa matukio kama hayo we unaona nchi iko salama?
Uvumilivu wa wananchi umepungua kwa kiasi kikubwa
 
Kwa tathmini yangu ni kwamba hawa vijana wanatumiwa na watu fulani, ambao wameweza kuwamanipulate kutokana na kutokukomaa kwa wanafunzi hawa kifikra. Ndio maana migomo ya UD siku zote ni ya undergraduate students. Ingekuwa ni migomo genuine mature postgraduate students nao wangekuwa wanagoma.

Ni bahati mbaya sana hata watawala wanaamini kwamba vijana wanatumiwa lakini infact migomo hii haikuanza leo, na hata hiyo sera ya uchangiaji haikuanzishwa mwaka jana wala mwaka huu. It's something of way back in the 90's. Well unaposema wanatumiwa una amini wao binafsi hawawezi kufikiri na kuact au? ZeMrcopolo kwa comments zako nnadhani hujawahi kuwepo UDSM. Culture iliyopo pale ni kwamba bila mgomo serikali na utawala wa chuo huwa wanakuwa so slow kuact. Enzi zetu kuna wakati ile NBC mlimani iliwahi kufunguliwa jpili something that was totaly strange into those ages. Lakini ilikuwa ni baada ya kugoma. Na hili la kwamba mbona postgraduate hawagomi inanidhihirishia hufahamu tofauti ya UG's na PG' pale mlimani.

All in all serikali na watawala wote wamechemsha, na kichekesho wanafikiri kufuta Daruso ndio suluhisho wkt infact this is one of the shameful decision to be done in 2009. Kwa mtizamo huu tusijeshangaa hata chama cha walimu tukaambiwa kimefutwa eti kwa sababu ya mgomo.

Who feels it knows it!!!!!!
 
Naamini panapofuka moshi pana moto...tatizo la msingi lipo kwenye namna mikopo inavyotolewa elimu ya juu. Serikali ina sera za kutoa mikopo, lakini implementaion inaleta matatizo kwasababu so far imekuwa ngumu kujua nani ni maskini wa kweli mwenye kuhitaji 100% na nanani siye. Cha msingi ni kuazima busara na kutafuta njia muafaka ya kulitatua. Kitu kibaya sana badala ya wahusika kuendesha suala zima kama ni ishu of national interest linageuzwa ni suala la kisiasa zaidi. Kauli za machibya siyo sahihi...ila condemning the claim about problems related to how loans are being given for higher learning students is also not realistic.
We should all seek to understand before being understood. Otherwise migomo itakuwa inaendelea kila kukicha kwasababu ya ku handle everything with arrogance
 
Last edited:
Machibya aache sera potofu, ni majuzi tu Waziri wa Elimu ameeleza wazi kabisa kuwa ambaye atashindwa kabisa kulipia akate rufaa kwake. Sasa hii fujo mpya tena ina msukumo wa nani? Angetakiwa awahamasishe watoto wa maskini kukata rufaa kwa waziri haraka iwezekanavyo kuliko kupoteza muda wa kuendekeza migomo ambayo mwisho wake yeye ndiye atakayepoteza. wanaomtuma hebu na wamshauri vizuri.
 
Hawa wanafunzi wanatapatapa na si muda muafaka wa kuwalaumu. Cha msingi Serikali ichukue hatua kumaliza matatizo ya wanafunzi wa elimu ya juu si kutumia mabavu.

Nadhani pia tatizo lipo kwa hao walimu na viongozi wa vyuo vikuu (UDSM & SUA), hawa wana matatizo makubwa kwani wanajaribu kuendekeza mashindano na wanafunzi wakitegemea vyombo vya Dola. Hauwezi kuongoza kwa namna hii.

Hawa wangeenda kujifunza chuo kikuu cha Mzumbe (MU) waone jinsi wao wanavyoweza ku manage matatizo kama haya.

Tatizo la UDSM na SUA ni uzembe wa Viongozi (VCs et al) pamoja na Bodi ya mikono and not otherwise. Na kwa upand e wa Bodi ya mikopo ni ufisadi mtupu.
 
2. Ni jukumu la jamii kuwa na mikakati kuwasomesha watu wake..mbona pesa ya arusi tunaweza kuchanga mamilioni?
Mkuu usilinganishe Kenya na Tz...!

Bado nadhani unakubaliana nami kuwa serikali yetu INAWEZA kuwasomesha vijana wake elimu ya Juu BURE.

Halafu, sijui hiyo jamii unayoilaumu kwa kuchangia harusi kama unaitendea haki... Jamii hii hii ndiyo inayokamuliwa vibaya na serikali yao na pesa hiyo ndiyo Jamii hiyo ina-demand itumike kuwasomesha vijana wake.

Fuatilia makato ya kodi wanayokumbana nayo watanzania, kila sehemu bei za vitu ziko juu ajili ya makato ya serikali (kitu ambacho naamini kila kukicha serikali yetu inajivunia kukifanikisha kwa umakini mkubwa na maana yake kuwa inajiingizia kipato kizuri sana tu).

I stand to be corrected
 
Yes, serikali uwezo wake mdogo sana.
Mashangingi ya bei mbaya 700 kwa mwaka mmoja. Kukodisha ndege mbovu za ATCL, zilizopelekwa Kiwira kimya kimya, za safari, za vikao, washa, seminar, kongamano................ Kweli serikali uwezo wake mdogo, AMEN!!

Excellent Sikonge, umejibu wale wasemao serikali uwezo wake mdogo sana.
 
... hili la kwamba mbona postgraduate hawagomi inanidhihirishia hufahamu tofauti ya UG's na PG' pale mlimani.


Who feels it knows it!!!!!!

Tafadhali nifafanulie hiyo tofauti iliyopo kati ya UGs na PGs wa UDSM.
 
Sera ya nchi ni kwamba masikini watasaidiwa kwa kupewa asilimia ya mkopo wanayohitaji na tajiri atajilipia mwenyewe. Hiki ndio wanachokipinga hawa wanafunzi kwa madai kwamba watanzania wote ni maskini hivyo wote wapewe asilimia 100 ya mkopo. sasa anaposema wanaorudishwa ni matajiri anajichanganya mwenyewe, kama anajua kuna matajiri kwa nini aliongoza mgomo wa kutaka wanafunzi wote wapewe mkopo asilimi 100%? Hiyo maana ulizoweka hapo ni yako wewe, angetaka ieleweke hivyo angeelezea explicitly


Naamini panapofuka moshi pana moto...tatizo la msingi lipo kwenye namna mikopo inavyotolewa elimu ya juu. Serikali ina sera za kutoa mikopo, lakini implementaion inaleta matatizo kwasababu so far imekuwa ngumu kujua nani ni maskini wa kweli mwenye kuhitaji 100% na nanani siye. Cha msingi ni kuazima busara na kutafuta njia muafaka ya kulitatua. Kitu kibaya sana badala ya wahusika kuendesha suala zima kama ni ishu of national interest linageuzwa ni suala la kisiasa zaidi. Kauli za machibya siyo sahihi...ila condemning the claim about problems related to how loans are being given for higher learning students is also not realistic.
We should all seek to understand before being understood. Otherwise migomo itakuwa inaendelea kila kukicha kwasababu ya ku handle everything with arrogance

Mkuu unajua tatizo letu sisi watz ni kwamba siku zote tu waoga au wavivu kukomfront reality. Hebu imagine mojawapo ya kigezo kwamba ulipiwe asilimia ngapi ni shule ulizosoma sekondary kama kuna any of the so called "academia" hupati mkopo say ulisoma form six St Mary's au Feza basi wewe mkopo sahau lakini tunashindwa kuelewa kwamba mtu anaweza kuwa amelipiwa huko na wasamaria wema na ambao waliamini kwa namna iliyokuwepo baada ya kumaliza hiyo form VI basi kijana itabidi ajitegemee. Mama Lwakatare anasomesha yatima kwenye shule zake ina maana vjana hao hawapewi mkopo eti tu kwa sababu wamesomshwa St. Mary's.

Pamoja na kwamba ni ngumu sana kwa nchi masikini na corrupt kama hii kupambanua nani maskini na nani tajiri, lakini something has to be done kupata data za kueleweka na za kuaminika.
 
Hongereni kwa kutimiza lile mlilokusudia mana CCM wanasema bila hata kutenda. Tupo pamoja kwenye hili japokuwa sio kimwili. I wish i could go back. Ni watanzania wachache wenye ujasiri kama wenu. Plz kama kuna mtu ana mawasiliano nao waambie huku kijijini tunaelewa kazi wanayoifanya.

Our understanding huku kijijini

Hatukatai hii sera ila wakati wake bado, watu hawajawa tayari. Nchi hii haina kuaminiana hata chembe. Haiwezekani utumie computer kuangalia nani apewe asilimia gani. Watu wamedanganya i have a evidence on this na sitanii. Hiki ndicho kinachonifanya nione kuwa hapa pana kamchezo. DARUSO hapa ndo mahala pa ku komaa napo mana hawa hawa mafisadi ukishafika chuo kwa private sponsor wanakusaidiia kupata mkopo.

Maandalizi ya hapa lazima tuanze kupanga uzazi kuliko kuamini kuwa kila mtoto atakuja na riziki yake mwisho ni WIZI MTUPU. Nyumbani mpaka ughaibuni.
 
Ze marcopolo na Shy Mngekuwa ndio watu wa Daraja la chini haya maneno ya Machibya mngeyaaelewa lakini kwakuwa mambo yenu yapo shwari lazima mumuone kama Mzushi tu kwani kwenu hakuna Effect na inawezekana nyi e ndio mliosoma bure Wasaliti wakubwa na wanene, nadhani mnashindwa kusoma alama za nyakati !!!!!!
 
Our understanding huku kijijini

Hatukatai hii sera ila wakati wake bado, watu hawajawa tayari. Nchi hii haina kuaminiana hata chembe. Haiwezekani utumie computer kuangalia nani apewe asilimia gani. Watu wamedanganya i have a evidence on this na sitanii. Hiki ndicho kinachonifanya nione kuwa hapa pana kamchezo. DARUSO hapa ndo mahala pa ku komaa napo mana hawa hawa mafisadi ukishafika chuo kwa private sponsor wanakusaidiia kupata mkopo.

Maandalizi ya hapa lazima tuanze kupanga uzazi kuliko kuamini kuwa kila mtoto atakuja na riziki yake mwisho ni WIZI MTUPU. Nyumbani mpaka ughaibuni.


Sasa kama baadhi ya wanafunzi wamedanganya ili kuwadhurumu wenzao kwa nini tunailaumu sera ya serikali? Kwa nini DARUSO kama chama cha wanafunzi -badala ya kugoma na kutaka flat rate ambayo ni nonsense- isibuni utaratibu wa kuijulisha bodi juu ya hali za uchumi za wanafunzi? DARUSO na vyama vingine vya wanafunzi vilikuwa na nafasi nzuri kwenye hili kwa sababu wao wanawajua wanafunzi wote na wanaona their dat to day life. Ingemake sense iwapo DARUSO wangeomba fungu la kuwawezesha kutafuta report za hali za uchumi wa wanafunzi na kuanalyse uwezo wao wa kujilipia kuliko jinsi wanavyoact irresponsibly!!!
 
Jiweke kwenye position ya mtanzania mwanafunzi wa UDSM asiyeweza kutimiza masharti hayo ya readmission kabla ya kulaumu hizo lugha 'zisizo na busara' aliyotumia.

Jee sote tukijiweka katika hali za utatanishi tulizonazo na kuamua kama huyu wa chuo kikuu unadhani ingekuwaje?

Tanzania hii watu wana tabu nyingi kuanzia makazini, shuleni na hata mitaani na vijijini ha ikiwa sote sote tutajipa haki a kutumia nguvu basi kweli hapatakaLIKA.
 
Daruso ilishafutwa sijui alikuwa anaongea kwa niaba ya nani kauli kama hizo hazitakiwi haswa kwa nchi yetu ya tanzania tuliozoea amani , uhuru na upendo maisha yetu yote hatuko tayari kuacha vijana hao watishie maisha wengine

Inasikitisha sana kuona watu mnaweka siasa kwenye mambo ya kitaifa. Yaani wanafunzi wa Chuo Kikuu kudai haki zao linafanywa kwamba ni jambo la kisiasa!

Malipo ni hapa hapa duniani.....!!!! Ipo siku!
 
UGs = Undergraduate students na PGs = Post graduate students nadhani niko sahihi...


Uko sahihi, lakini nilichouliza ni tofauti inayofanya PGs wasishiriki katika migomo wakati UGs kila muhula lazima wabuni sababu ya kugoma.
 
Back
Top Bottom