Tanzania haina udhuru kuwa maskini; haielewi - Balozi wa Ujerumani

Wengi kiasi gani? Kati ya milioni 40 ni wangapi wanaofaidika na maliasili zetu?

Sina takwimu. Ninazo anecdotal data tuu. Kwa ninao wajua mimi ni wengi. Lakini ukiniuliza ni wengi kiasi gani kati ya milioni 40 hapo kwa ukweli siwezi kukupa jibu. Labda serikali ianze kukusanya takwimu hizi tuzione.
 
Kaangalie hospitali zetu na shule ndio usema hivyo. Quality of life inaanzia hapo. Watu wanakula vizuri, wanasoma vizuri na wanapata matibabu mazuri.

Hao watu wanaokula vizuri, wanaosoma vizuri na wanaopata matibabu mazuri mbona wapo? Tena wala si vigogo. Ni watu baki tuu wanakula neema. Kama unataka nchi nzima ile, isome na itibiwe vizuri basi hapo sijui kama itawezekana. Maana hiyo ni utopia unayoiongelea.
 
1. Tanzania inaendelea kuwa maskini kwa sababu viongozi wanasema hadharani kuwa hawajui kwa nini nchi na wananchi ni maskini lakini walipenda kuwa viongozi wa maskini hao.

2. Kama nchi na kama wananchi tumeshindwa "kuishi kimjini mjini".

3. Watanzania tumenusishwa "ugolo" wa amani,mshikamano na utulivu.

4. Ubinafsi usio kikomo, rushwa na ufisadi ndio vitu vinaendesha mfumo wetu wa kijamii na serikali na hilo limesimika mfumo wa chukua chako mapema.

5. Kama wananchi na viongozi tumejenga mawazo/fikra za kufadhiliwa/ kusubiri msaada wa kufanya yale yaliyo muhimu.

6. Viongozi wetu kukosa uzalendo,kupenda ufahari/ kutanua (ubadhirifu wa mali za umma) huku wakijua kuwa wananchi hawana uthubutu wa kuwawajibisha au kuwaadhibu.

7. Kila kitu/ jambo linafanywa kuwa ni siasa hata pale unapohitajika taaluma maalum/ utaalamu. Hili limepelekea wasomi na wanataaluma kukimbilia kwenye siasa kuendeleza unafiki wa kimfumo.

8. Wananchi hawajui haki zao na hakuna anayewaelimisha kuzijua haki hizo.Wanalipa kodi lakini siku zote wanaambiwa serikali haina fedha na hawahoji hela zimekwenda wapi.

9. Serikali zina mipango ya nguvu za soda/ zimamoto na kuwahadaa wananchi kwa ahadi hewa. Hakuna mipango endelvu na ya muda mrefu.

10. Mfumo wa uongozi umejengeka juu ya msingi wa kulindana hata mmoja anapoboronga.

11. Nimalizie kusema kuwa wananchi au umma wa Tanzania ni lege lege na hilo linajinesha kwenye viongozi tunaowachagua au wanaojichagua katika nafasi nyeti.

Sababu ni nyingi sana lakini kubwa ni kuwa kama nchi bado hatujataka kuondokana na umaskini tulionao mbali na neema ya raslimali tulizonazo. Tukiamua kuendelea basi ni kupindua/ kugeuza hayo niliyaandika hapo juu.
 
Hao watu wanaokula vizuri, wanaosoma vizuri na wanaopata matibabu mazuri mbona wapo? Tena wala si vigogo. Ni watu baki tuu wanakula neema. Kama unataka nchi nzima ile, isome na itibiwe vizuri basi hapo sijui kama itawezekana. Maana hiyo ni utopia unayoiongelea.
Inawezekana. Katika nchi yenye maliasili nyingi kama Tanzania tunaweza kutengeneza utopia ambako watoto wetu watakuwa wanasoma shule nzuri, mama zetu waja wazito wanapata huduma kwenye hospitali zenye vitanda vizuri, madaktari, manesi wa kutosha na kila mtu anapata zaidi ya mlo mmoja kwa siku. Inawezekana kabisa.
 
Sina takwimu. Ninazo anecdotal data tuu. Kwa ninao wajua mimi ni wengi. Lakini ukiniuliza ni wengi kiasi gani kati ya milioni 40 hapo kwa ukweli siwezi kukupa jibu. Labda serikali ianze kukusanya takwimu hizi tuzione.
Hapo umesema ukweli wako. We can and we should do better.
 
Jk alisema hata yeye haelewi........nafikiri ni kati ya milinganyo migumu sana kuielewa....lol
 
Utaona mara nyingi watu wanasema Tanzania ni tajiri lakini watu wake ni maskini, tanzania kuna abundant natural resources. Sina pingamizi na kuwa Tanzania tunarasilimali nyingi tu za kuweza kuwafanya watanzania waishi tofauti na ilivyosasa. Tatizo kubwa ninaloliona na kuamini ni kuwa suala siyo wingi wa rasilimali bali suala kubwa ni watanzania wanaelewa nini kuhusu rasilimali zilizopo na watazitumiaje ili kubadilisha maisha. Tatizo kubwa watanzania tunapenda kulalamikia serikali, ndiyo kuna mapungufu ya serikali na siyo ya Tanzania tu ni serikali zote ulimwenguni. Ili kuondokana na hali iliyopo ni lazima sisi wenyewe kama wananchi tubadilike kifikra na mitazamo ili kutumia rasilimali zilizopo kubadilisha maisha yetu. Hilo haliwezi kufanywa na serikali bali sisi wenyewe.

Ikumbukwe kuwa huenda ikawa matatizo na mfumo uliopo umetengenezwa na serikali na matatizo tunayoyaona wakati mwingine yanainufaisha serikali, hivyo hatutarajii serikali kuyaondoa matatizo hayo endapo inanufaika nayo. Kwa maana hiyo kwa kuwa kuibadili serikali ni suala gumu sana, ni vyema sisi wenyewe kama wananchi tukabadilika, badala ya kuilaumu serikali na kukaa bila kufikiri tufikirie kwa kujua kuwa serikali imeshindwa kutusaidia na kuangalia namna ambavyo tunaweza kujiletea maisha bora bila kutegemea serikali. Elewa fursa zilizopo na kuzitumia.
 
Tatizo letu ni siasa zimetujaa wananchi!Tunapiga domo tuko busy na siasa za CHADEMA na CCM huku uzalishaji zero,unategemea nini hapo?
 
Is the system of governance a problem or we have been cursed?



This thread is very important but some of JF members will be discussing it without taking into account its weight.

in my opinion i would prefer to say that Tanzania is not poor rather it has poor economy becauseof the following reasons:

1. The country has no specific vision on economy whether it is capitalist or socialist.
2. The country has leaders with no practical responsibility and accountability .
3. Most of the leaders of the Country are overtaken by age and proper skills that match with the modern development challenges.
4. Tanzania has educated youth who believe that politics is the avenue for their success.
 
Suala la msingi unapaswa ufahamu,mbio si za wenye kasi,na mapambano si kwa wenye nguvu.japan ni kisiwa ambapo hawana madini,natural resources kama mbuga,highest mountains,gas,rivers,lakes etc.nchi ya phillipines ama wanajiita tigers ni kati ya nchi zinazokua kwa kasi asia but 25 yrs ago ilikuwa ni nchi masikini kama tz.ni nini basi kilifanyika?na nani alileta mabadiliko?ni waziri wao mkuu aliyekuwa madarakani kwa miaka 25 aliweza kuitoa kutoka third world to be among the developed countries.rwanda,ingawa bado haijakuwa developed lakini ndio inapoelekea ni nini hasa kimechangia?uongozi wa rais Kagame,,najua watu watasema oohh ni nchi ndogo ntawajibu sawa je zanzibar ni kubwa?madagascar je?UONGOZI,UONGOZI,UONGOZI,,KUNA KIJANA mmoja alitengeneza caterpillar kwa kutumia chuma,guess what?sijui yupo wapi sa hv?na kuna kiongozi hadi alimsifia..tunaua vipaji,tunajali matumbo ambayo ukila kilimanjaro hotel kitaenda chooni,utanunua gari baada ya miaka 10 ni scrapper.tunataka viongozi wasio na uchu wa mali,,maana kuna chama kinasema UCHU WA MADARAKA,hata kagame alikuwa nao kwa ajili ya kuleta maendeleo ya nchi yake.SASA TUNATAKA MTU MWENYE UCHU WA MADARAKA KWA AJILI YA KULETA MABADILIKO.Sio mtu akipewa cha juu anakuwa kimya.
 
As Economics student, teacher i think one of the reason is that our leaders decide to make us poor and the second is that lack of political willingness because the decision of what to produce?when to produce?how to produce and who gets whats depends on the political economics since most of decision depending on normative economics

i.e kind of economy where by disagreement can be settled through voting, e.g in the parliament because majority have no political willingness(CCM)probably the questions above wilL not get solutions.Thanks
 
Culture of poverty is prevalent and widespread in this beautiful country. We are lazy and ignorant, and when there is an opportunity to do more we often do less.

Hoping government will come to the rescue. The ever present faces of people complaining about this or that to the govt-serikali inabidi itusaidie hili au lile, why did you build kinyume na taratibu za serikali za mitaa? damn it. Maendeleo yataletwa vipi na this kind of thinking?

All those people at the coast who think kusoma ni majaliwa na siyo lazima.

All the the lack of entrepreneurship in our youths, who out of school think of getting employed only.

All the men out there who after increase income, only go on to get another wife and eventually invest less in their retirement and their children's future.

All the young girls who are discouraged to pursue more education despite all its obvious advantages in the struggle to eradicate poverty.

All that fatalistic view of life that tells us we dont need to question authority and kua makondoo hadi kwenye haki zetu za kimsingi.

All the money that is channelled by the few rich to the mosques and churches across the country instead of direct charitable contributions of social or economic nature i.e kununua vifaa vya mahospitali yetu, kujenga maabara za elimu ya juu, kuweka kwenye utafiti wa magonjwa na sayansi nyingine, kurudisha watoto wa mabarabarani shule NK.


Sisi ni maskini kitamaduni kwa hii ndiyo maana na serikali na taifa kwa ujumla ni maskini....Government alone should not be crucified for all our economic and social problems. Its is basically our fault as mush it is theirs too.


mharakati,
 
Kiukweli inasikitisha sana na inaleta uchungu. Hasa kwa wanaobahatika kwenda kwa hao wazungu wananyanyasa na wanadharau sana ukiuliza ni maskini. Haya yote tunasababishiwa na hao wanaojiita VIONGOZI. Kila siku mambo kuzidi magumu uongozi unabadilishwa lkn hakuna kitu zaidi maneno mengi saaaaana! TUNABAGULIWA SANA ULAYA NA KUDHARAULIWA KWA UJINGA WETU. Ni hao hao mabalozi na watu wao ndiyo wanapeleka taarifa za nchi zetu na kuonekana sisi ni wajinga lakini kwa hakika sisi tunauwezo kuliko wao ni UMASKINI unaosababishwa na wachache. HATA kuboresha Hospitals, Elimu na Makazi pamoja na miundo mbinu ni vitu muhimu lkn hakuna anayewajibika TUTAPONA? Tumebakia kelele za UDINI na kwa ujinga wetu wengi wananchi tunaamini,wao wanalala na makafiri na kuzaa nao hawaoni udini, Ni kupumbazwa tu!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom