Tanzania haina udhuru kuwa maskini; haielewi - Balozi wa Ujerumani

swali gumu sana hili....kwani hata jk alishaulizwa
na mwandishi wa habari bbc...sehemu ya maongezi ni hii
mwandishi. unafikiri kwa nini tanzania ni maskani?
jey key . hata mimi sijui ni kwa nini!
 
Kwa sababu tunaimport hadi toothpicks, nchi inakua tajiri kwa kuongeza uzalishaji wa kilimo na viwanda kwa export,na hii inaletwa na elimu bora pamoja na uongozi imara.
 
Ili tuondokane na umaskini tunahitaji vitu vinne uongozi bora, WATU, siasa safi na ARDHI...kwa mtazamo wangu hatuna viongozi bora. Tatizo ni mfumo wa kupata viongozi kubinafsishwa. Tumepata genge la Wahuni ambalo linapanga safu za uongozi. Matokeo ni kuwa na wajinga katika uongozi na kwakua wajinga ndio waliwao tuko maskini kwa kuliwa.
 
Katuni%2BAgost%2B24.jpg
 
WATANGANYIKA nipeni mimi niwaongozeeni, kila Raia atakuwa na nyumba nzuri ya kuishi, watoto wote kwenda shule, Mahospitali yatakuwepo,Mabarabara mazuri, nitaitokomeza Rushwa,mafisadi wote hawatakuwepo, hakuna ubinafsi katika kupeana vyeo atapata mtu cheo aliyesoma kila mtu atakuwa na kazi kutokana na elimu yake haya tena nipeni Nchi niwaongoze ...
 
Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne; WATU, ARDHI, SIASA SAFI na UONGOZI BORA.
WATUuuuuuuuuuuuu tupo.
ARDHIiiiiiiiiiii ya kumwaga.
SIASA safi, pumbafu kabisa .........
Uongozi bora ...... hakunaga!
 
Hebu tujadiliane inakuwaje tanzania nchi yenye rasilimali nyingi za kipekee lakini bado ni masikini na wananchi wake wanaishi maisha duni?
 
tulitupilia mbali siasa ya ujamaa na kujitegemea tukakumbatia siasa za kimagharibi hapo ndipo tulipopotea turudi kwenye siasa yetu kwanza.
 
Kwa sababu munatumia muda wenu kufanya mambo ya kijinga mfano mmoja wapo ni jinsi mulivyorundikana kwenye msiba wa Kanumba
 
Serikali ya CCM haina sera Inayoonyesha Dira ya taifa na kama inayo basi haiitekelezi. Rushwa na viongozi kutokuwa na utaifa nalo ni tatizo kwani mikataba yote mibovu imepitishwa kwa sababu ya rushwa na kutokujali utaifa wetu.
 
Hebu tujadiliane inakuwaje tanzania nchi yenye rasilimali nyingi za kipekee lakini bado ni masikini na wananchi wake wanaishi maisha duni?

tunahitaji viongozi na si watawala,tunahitaji siasa safi na si siasa shwari,tunahitaji viongozi watakao jitolea kwa maslahi ya nchi na watu wake na si kwa maslahi ya kikundi na familia zao

hakika hayo tukiyapata basi upo uwezekano wa kuwa juu ya USA kwa rasimali tulizo nazo
 
Back
Top Bottom