Tanzania haina sababu ya kuwa na Bunge; madiwani wanatosha

Papa D

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
753
182
Jamani kwa Mambo yanayoendelea bungeni hakuna haja ya kuendelea kuwa na Wabunge. Wanapoteza/wanafuja rasilimali za taifa bila Tija. Ni busara Mabaraza ya madiwani yakaimarishwa.
jamani hili mnaliona aje?
 
Kweli kwani Wabunge zaidi ya Mia mbili wa Ccm hawana wanalofanya bora 48 wa Cdm wanauchungu na rasilimali za nchi.
 
Hujajua tatizo bado uko mwepesi, tatizo ni wabunge wa sisiem na spika wao. Kila mahali wanakwamisha utadhani mwamezaliwa na mama mmoja wote hawana akili zaidi ya kutegemea za Makamba (baba) sio mtoto, maana at least mtoto anaongea point.
 
kwa kweli mimi kinachonishangaza pale mbunge anapochangia hoja kwanza kabla ya kuchangia anasema anaunga mkono hoja kwa 100% sasa sijui anachangia nini si bora akae tuu aache wenye hoja wachangie.
naunga mkono hoja bora wabunge 48 wa chadema kuliko 200 wa ccm
 
Hilo ndio bunge la kumi la JMT, tusubiri zaidi ya tuyaonayo sasa.
 
Jamani kwa Mambo yanayoendelea bungeni hakuna haja ya kuendelea kuwa na Wabunge. Wanapoteza/wanafuja rasilimali za taifa bila Tija. Ni busara Mabaraza ya madiwani yakaimarishwa.
jamani hili mnaliona aje?

Pendekezo lako ni zuri lakini halina chanzo...au sababu ya kufikiria hivyo...

Bunge ni kuubwa mno hasa viti maalum...
hakuna hoja bali ni vijembe kama club za mpira
Je ni vibaya kupendekeza wabunge wa kuchaguliwa wawe japo na ka degree kamoja?(maana ndio watunga sheria wetu na wapitishaji mikataba hawa!) ukizingatia hata lugha ya mikataba ni ya kigeni!
hao wa kuteuliwa wanaowakilisha makundi maalumu ndio wasiwe na mipaka ya kiwango cha elimu
 
Tena hawa wabunge wa viti maalumu ndio wanaharibu kabisa umakini wa bunge, bora viti hivi vifutwe!!
 
Ni bunge la kufurahisha kwani hata wanaozama kwenye maombi wameanza mapema.
 
kwa kweli mimi kinachonishangaza pale mbunge anapochangia hoja kwanza kabla ya kuchangia anasema anaunga mkono hoja kwa 100% sasa sijui anachangia nini si bora akae tuu aache wenye hoja wachangie.
naunga mkono hoja bora wabunge 48 wa chadema kuliko 200 wa ccm

Hesabu ni tatizo la kitaifa nchi hii ndugu yangu. Inabidi hawa jamaa waelimishwe maana ya asilimia 100. Yaani kama unaunga mkono kwa asilimia mia moja ina maana hoja haina mawaa na haihitaji kuongezwa wala kupunguzwa.
 
Hapa umeona mbali sana. Mimi naona ni bora kuwa na baraza la wazee kwani hawa walishaasi nchi yetu na sasa wamekaa pale kama makapi tu. Hawana maana yoyote, mfano katika bunge hili siku tano zimetumika kwa salamu tu hii ina maanisha kwamba ccm wametumia suku nne na robo tatu kusalimiana. Hii ni hasara kubwa sana. Pia ni kukosea adabu fedha ya Watanzania waliz:thinkingoitafuta kwa kulima juani, kusukuma mikokoteni juani, kufundisha kwenye vumbi, kupiga kwata juani, n.k.
Mimi nasema hakuna haja ya kuwa na bunge la waasi.:thinking:
 
Wabunge nadhani tunapaswa kuwa nao ila wa namna gani? kama ndo hao wanaotetea ufisadi bora wasiwepo. Kubwa zaidi nadhani kuna haja ya kuwapiga chini viti maalum na wale wa kuchaguliwa manake kubwa ni kuvaa vikuku tu mjengoni!
 
Jamani kwa Mambo yanayoendelea bungeni hakuna haja ya kuendelea kuwa na Wabunge. Wanapoteza/wanafuja rasilimali za taifa bila Tija. Ni busara Mabaraza ya madiwani yakaimarishwa.
jamani hili mnaliona aje?
Hilo nalo neno.
 
kume umeliona hilo, hawa jamaa wanaonekana kufanya vitu kwa kukariri na kuzoelea sana:coffee:
bora liende
Hesabu ni tatizo la kitaifa nchi hii ndugu yangu. Inabidi hawa jamaa waelimishwe maana ya asilimia 100. Yaani kama unaunga mkono kwa asilimia mia moja ina maana hoja haina mawaa na haihitaji kuongezwa wala kupunguzwa.
 
Pendekezo lako ni zuri lakini halina chanzo...au sababu ya kufikiria hivyo...

Chanzo ni tathmini ya michango yao na matokeo ya hiyo michango;
Au wewe kwa maoni yako mpaka niseme chanzo ni ofisi ya Bunge, wizara ya Fedha, usalama wa Taifa n.k!; Kwa mtu anayefuatilia mabunge au mabalaza ya uwakilishi hawezi kusema Wabunge wa Tanzania ni wanawakilisha Watanzania. Mbunge makini hawezi kutumia au kumsikiliza waziri akitumia dakika kumi kushukuru binamu zake waliokaa kwenye viti vya wageni huku taifa likiwa gizani kwa kukosa umeme [for about twenty years now]. Bunge makini haliwezi kumtuma makamba aende mtera kuangalia kina cha maji kisha aje na mapendekezo ilhali master plan ipo tangu enzi za mkoloni. Nyerere alianza kuitekeleza. matokeo yake wote tunajua kipindi chake hatukuwahi kusikia upungufu wa umeme. HAYO NI KWA UCHACHE TU WA YALE YANAYOFANYA BUNGE LIPOTEZE CREDIBILITY YAKE!!!

DO YOU WANT MORE?
 
Hivi mafanikio kwenye deliverables za mbunge yanaweza kupimwa kwa vigezo vipi?

Kwa kweli hii ni moja ya sababu zinazonishawishi kuamini kuwa uwepo wa bunge TZ ni useless!!! nashukuru umeliona hili pia!! labda pia tupendekeze vigezo vya ufanisi wa mbunge!!
 
Back
Top Bottom