Tanzania Haikopesheki!!

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,422
1,790
katika kipindi cha BBC kilichorushwa jana jioni (20-02-2012), kuna taarifa ya kuwa Tanzania imewekwa katika orodha ya BLACKLIST na hivyo HAIKOPESHEKI, NA UWEKEZAJI NI MGUMU. Kwa maelezo yaliyotolewa ni kwamba nchi ikifikia kuwekwa katika BLACKLIST ina maana ni ngumu kwa nchi wahisani kuikopesha Tanzania kwa hofu ya kutolipwa deni, na pia Wawekezaji wataogopa kuwekeza Tanzania kwa hofu ya kibiashara.

Tanzania inafikia hatua ya kuingia katika orodha ya BLACKLIST kutokana na kukithiri kwa matumizi ya PESA CHAFU (MONEY LAUNDARING) ambazo husababishwa na kukithiri upatikanaji na matumizi ya pesa Haramu.

Je, wadau uchumi wetu miaka mitatu ijayo tutakuwa wapi???

Au ndio Tanzania nayo inakaribia kutangazwa imefilisika?


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
We deserve kuwa kwa iyo list ndo maana serikali inakopa benki za ndani maana nje issue.
Sasa naona na bank za ndani nazo zimeanza kuchoka sijui itakuwaje
 
Ajabu kuna siku Mh. Zitto Kabwe alitoa kauli Bungeni kuwa " Serikali ya Tanzania Imefilisika"

Yaani alipingwa vikali mno kwamba kauli yake ni ya uongo. Sasa sijui leo tutasemaje.

Na hii pia inasababishwa na pesa kuwa mikononi mwa watu wachache na kuiacha Serikali ikiwa haina kitu.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Ndicho walichotaka viongozi wetu tuliowapa dhamani ya kutuongoza na kuapa wakiwa wameshikilia biblia na quraani mkono na kusema watailinda na kuitetea katiba yetu
 
Back
Top Bottom