Tanzania haifai kuendelea kuwa Jamhuri

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Hakuna sababu ya kuendelea na Taifa la Tanzania kama Jamhuri (ya muungano au vinginevyo). Tanzania ni nchi dhaifu, maskini, dunia ya tatu, ambayo haiwezi kabisa kupambana na nchi za magharibi.

Nchi jirani zetu -- Uganda, Burundi, Rwanda na Kenya zina shida kubwa ya Ardhi. Ukiziunganisha nchi hizo zote, bado hazifikii Tanzania kwa ukubwa wa Ardhi. Tanzania ni nchi ya 31 kwa ukubwa wa ardhi duniani. Matokeo yake majirani zetu wanauana kwa vile tu msongamano wa watu umekuwa mkubwa.

Hatuwezi kuwaaangalia hivihivi wenzetu wanapata taabu, wakati sisi tunayo ardhi ya bwelele. Kwa kuanzia tutafuta mipaka kati yetu na wao, ili waweze kuja kujihomolea sehemu ya nchi yetu wanavyopenda! Hii ndio tunaloita soko la pamoja. Tanzania itabaki na taasisi muhimu -- Rais anayesindikizwa na misafara, anayekaa Ikulu, na akienda nje ya nchi, anapigiwa mizinga 21. Wabunge wanaofanya vikao, na wataendelea kuitwa Waheshimiwa. Vyama vya siasa 'vya upinzani' vitaendelea kuwepo, na kutambuliwa na mabalozi wa nje ya nchi. Jeshi letu tukufu litaendelea kusubiri adui aje na vifaru na mizinga kuchukua nchi. Hao ambao tunawagawia, ni kwa hiari yetu, si kwamba wametushinda vitani, hata kama wapo watakotuona sisi ni mazuzu kwa kufanya hivyo. Huo ni ufinyu wao wa kufikiri. Sisi tutaendelea kupata sifa duniani kwamba 'hata Waafrika tunaweza kuungana'. Baada ya miaka miwili mitatu, hata madaraka ya kisiasa tutayaunganisha, wasije wakadhani tunawaogopa.

Halafu wapo baadhi ya Watanzania vidomidomi wanaong'ang'ania mawazo ya kizamani kwamba tuendelee kuwa na taifa letu wenyewe. Wanaabudu mipaka bandia iliyowekwa na wakoloni. Wanataka Tanzania iendelee kuwa Jamhuri huru. Kuthibitisha kwamba sisi ni 'advanced' tunaifuta hiyo mipaka hata kama wananchi hawataki.

Siyo tu hivyo, tunaandaa wizara nzima, tunayoitengea bajeti, kuhakikisha Tanzania inafutwa kikwelikweli pasi na uwezo wa kurudi tena.

Kwa kuanzia, mipaka ya Tanzania tutaifuta Julai 01 mwaka huu 2010, isije ikawa mambo ya uchaguzi Tanzania ukaja utawala mwingine utakaozinduka na kubadili mawazo. Ofkozi hiyo ni mpaka Bunge lipitishe makubaliano ambayo Rais Kikwete keshayasaini -- bunge la nani litakalothubutu kukataa?

Miaka ya zamani Watanzania walikuwa 'brainwashed' kuwa tayari hata kutoa maisha yao kulinda mipaka, uhuru, umoja na ardhi ya Tanzania. Hivyo pale Iddi Amin alipotaka kuchukua 'ardhi kidogo tu' ikawa vita! Watu walijitolea kwa hiari na kwa lazima kumng'oa 'nduli' mvamizi. Lakini leo tunaigawa nchi nzimanzima, tunafuta hiyo mipaka ambayo watu walijitolea muhanga kuilinda. Tukiwa wazima, hatukunywa, wala hatukulewa. Nchi tunaigawa kwa watu wengine watokao mbali, kwa nini isiwe Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi?

Lazima tuwaonee huruma. Wao wako kwenye ile Jumuia Nyingine ya Afrika Mashariki - Igad. Lakini kule watachukua ardhi ya wapi? Somalia? Jibuti? Ethiopia? Jumuia yao ni kubwa, ya zamani, na ina malengo yote sawa na EAC. Lakini kule bado suala la msingi linabaki kuwa ni ardhi. Siyo ardhi ya jangwa, ardhi ya kilimo! Kilimo kwanza! Hata wale wengineo wako kwenye jumuia ile nyingine. Lakini lazima tuonyeshe sisi hatuogopi kupoteza uhuru wetu, mradi tu unaenda kwa wenzetu wenye ngozi nyeusi kama sisi.

Ni kweli walisherehekea pale EAC ilipovunjika mwaka 1977 kwa vile walijua tutapata taabu, lakini sasa hivi tunawapatia nchi nzima, pasipo na uwezo wa kusema 'ajua' kama ya 1977.

Tanzania mwisho Julai 01 2010, Viva Afrika Mashariki!
 
Kwa kuanzia, ifikapo Julai mosi mwaka huu, Wakenya, Wanyarwanda, Warundi na Waganda watakuwa na haki zifuatazo Tanzania:

1. Haki ya kwenda popote Tanzania
2. Haki ya kufanya kazi ya ajira au isiyo ya ajira yoyote Tanzania
3. Haki ya kufungua biashara yoyote na kufanya chochote Tanzania
4. Haki ya kumiliki ardhi na kujipatia makaazi (hii itafanya Tanzania isiwe na Wakimbizi toka EAC kwa vile watakuwa na haki sawa tu (na labda kuzidi) za Mtanzania. Huoni itakuwa sifa?)
5. Haki ya kuhamisha faida au mtaji toka Tanzania.

Hizo haki zote zitalindwa na sheria na makubaliano haya hapa ambayo Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania keshayasaini. Bado Bunge tu...
 
Kwa vile hayo yameandikwa kwa Kimombo, ingekuwa vyema mtu hapa akatutafsiria kwa Kiswahili fasaha maana yake nini hasa.

Baada ya hayo, nchi za Magharibi hazitatuweza!
 
Pana hiki kitabu kinasema kwamba mataifa yote ni bandia, jamii za [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Imagined_communities"]kufikirika [/ame]tu. Mataifa kama Tanzania yakifutika, ni vema kabisa. Hasa pale watawala wenyewe wanapokuwa mstari wa mbele kuvunja himaya zao!
 
Chonde mkuu ya zimbabwe ni somo tosha kwetu.pplation ya rwanda na burundi ongeza na uganda haifui dafu.umimi wako uweke kando kuna watakaozaliwa baada ya wajukuu zako watapata wapi ardhi? Kama kuna aliyegawa kagawa eneo la shamba lake.NYERERE alishasema madini yaacheni yabakie ardhini hata baada ya miaka mia wajukuu watapata uwezo wa kuyavuna watayavuna. Mkampuuza ki wapi leo?mwabakiziwa mahandaki mwajivuna nayo. Wewe kiranga hicho umekipata wapi the great thinker
 
Wabunge wanaangalia matumbo yao wala hawasomi yale wanayotakiwa kusoma. Inasikitisha, kuchagua rais kichaka ndio athari zake na sasa tunayaona. Asiyesikia la mama yake walimwengu watamfunza. Subirini tu kama yale yanayotokea Congo, Zimbabwe sio mafunzo Watanzania wana haki ya kusubiri wataona nini kitatokea.
 
Draft Protocol.11009 Some Exerpts from the protocol (emphasis may be added)


2.3 The Common Market shall be managed in accordance with the relevant laws of the Community.

[Maana yake sheria za Tanzania ziko chini ya mamlaka ya EAC]


3.1 The Common Market shall be guided by the fundamental and operational principles of the Community as enshrined in Articles 6 and 7 of the Treaty.


3.2 (a) observe the principle of non‐discrimination of nationals of other Partner States on grounds of nationality;

[Wakitaka kuchimba dhahabu, kuchimba mafuta, kuchimba gesi, kulima mashamba, kumiliki majengo, kumiliki misitu, mbuga za wanyama, milima na mabonde... kuwa madereva teksi, makonda, masuka wa daladala, ...wasizuiwe kwa vile tu si Watanzania]



5.2
(b) ease cross‐border movement of persons and eventually adopt an integrated border management system;
[Tunakuwa na idara moja ya uhamiaji... ]



(c) remove restrictions on movement of labour, harmonise labour policies, programs, legislation, social services, provide for social security benefits and establish common standards and measures for association of workers and employers, establish employment promotion centres and eventually adopt a common employment policy;

(d) remove restrictions on the right of establishment and residence of nationals of other Partner States in their territory in accordance with the provisions of this Protocol;

[Hakuna kumzuia mtu kuishi Tanzania kwa vile tu si Mtanzania...]



(e) remove measures that restrict movement of services and service suppliers, harmonise standards to ensure acceptability of services traded; and

(f) eliminate restrictions on free movement of capital; ensure convertibility of currencies; promote investments in capital markets (stock exchange) eventually leading to an integrated financial system.

[Kuhamisha mitaji... raia wasio Watanzania wakishavuna 'chao', wasizuiwe kukihamishia 'kwao kabisa'...]


5.3 (h) integrate environmental and natural resources management principles in the activities relating to the Common Market;
[Serengeti, Ngorongoro, Manyara.... Bingo! Mlima Kilimakyaro... Pwani ya Bahari ya Hindi -- vyote si vya Tanzania pekee tena...]


6.2In addition to the Customs Law of the Community, the free movement of goods shall be governed by:

(a) the East African Community Protocol on Standardisation, Quality Assurance, Metrology and Testing;

[Mwisho wa TBS]


(b) the East African Community Standardisation, Quality Assurance, Metrology and Testing Act, 2006;

(c) the provisions of this Protocol;
[Sheria za Bongo zitawabana tu Wabongo....]


7.2

(a) the entry of citizens of the other Partner States into the territory of the Partner State without a visa;



(b) free movement of persons who are citizens of the other Partner States within the territory of the Partner State;

(c) that the citizens of the other Partner States are allowed to stay in the territory of the Partner State; and



[Hakuna tena mambo ya vibali vya makaazi]


(d) that the citizens of the other Partner States are allowed to exit the territory of the Partner State without restrictions.


7.9 The implementation of this Article shall be in accordance with the East African Community Common Market (Free Movement of Persons) Regulations, specified in Annex I to this Protocol.



10.1 The Partner States hereby guarantee the free movement of workers, who are citizens of the other Partner States, within their territories.
[Hakuna mambo ya vibali vya kazi... wao tu na roho zao!]


2. For the purposes of paragraph 1, the Partner States shall ensure non discrimination of the workers of the other Partner States, based on their nationalities, in relation to employment, remuneration and other conditions of work and employment.
[Kwa hiyo ni jukumu la serikali ya Tanzania kuhakikisha haiwapendelei Watanzania kwenye ajira...]


13. (a) a national of a Partner State to:
(i) take up and pursue economic activities as a self employed person; and



[Jua kali, waongoza watalii, mama lishe, wang'arisha viatu, walimu, madaktari, wavuvi, warina asali... wowote wale, ruksa!]



(ii) set up and manage economic undertakings,
in the territory of another Partner State;
[Kufungua mgodi wa Tanzanite, kujenga bandari, viwanja vya ndege, kulima, kufuga, ...kufanya chochote...]



13.4 The rights applicable to a spouse, child and dependant of a worker under Article 10 of this Protocol shall apply to the spouse, child and dependant of a self employed person.

[Ukoo mzima una haki hizo...]

14.
1. The Partner States hereby guarantee the right of residence to the citizens of the other Partner States who have been admitted in their territories in accordance with Articles 10 and 13 of this Protocol.

[Kwa hiyo makabila mazimamazima yanaruhusiwa kuja kuanzisha makaazi yao mapya TZ]

2. The right of residence guaranteed under paragraph 1, shall apply to the spouse, child and a dependant of a worker or self‐employed person entitled to rights provided in Articles 10 and 13 of this Protocol.
 
Hata kwenye SADC hatuna makubaliano kama haya. Kumbe tulipigania uhuru wa nini? Je kwa nini tulimfukuza nduli wakati sisi ni tutusa tu?
 
Mlenge sijaona bado unachekelea nini wakati ulichokizungumzia ni "Draft Protocol" na sio Protocol iliyopitishwa na Wakuu wa nchi husika. Na hakuna mahali popote ambapo pameonyeshwa kwamba mipaka haitakuwepo kama ulivyoanza kueleza hapo juu. Nilichoona ni kwamba "some restrictions" zitaondolewa na hakuna mahali popote ambapo Sheria za "Territory" nyingine zitakuwa non-functional! After all unanipa mashaka kama wewe kweli ni Mtanzania hasa pale "unapoona huruma" eti kwa wasomali, wanyarwanda, etc na kutokuona huruma kwa watanzania watakaokosa ardhi ambayo inaweza kuvamiwa na wageni!
 
Buchanan

Rais amekwisha sign hiyo protocol, kinachosubiriwa ni wabunge tu kulipitisha. Kuanzia Juni mosi utaanza kukumbana na Nyang'aus, banyamulenga with equal rights kama Watanzania wengine, naona kama hili lilikupita.
 
Buchanan

Rais amekwisha sign hiyo protocol, kinachosubiriwa ni wabunge tu kulipitisha. Kuanzia Juni mosi utaanza kukumbana na Nyang'aus, banyamulenga with equal rights kama Watanzania wengine, naona kama hili lilikupita.

Kwani ikisainiwa na Rais ndio inaacha kuitwa "Draft Protocol?" Na huko kumiliki mali patakuja overnight? Mbona sheria za uwekezaji, umiliki ardhi, uhamiaji, etc bado hazijabadilishwa? Na kama zikibadilishwa hatujui zitachukua sura gani! Hebu soma paragraph zifuatazo:
4. The free movement of persons shall not exempt from prosecution or extradition, a national of a Partner State who commits a crime in another Partner State.

5. The free movement of persons shall be subject to limitations imposed by the host Partner State on grounds of public policy, public security or public health.

6. A Partner State imposing a limitation under paragraph 5, shall notify the other Partner States accordingly.
 
Kwani ikisainiwa na Rais ndio inaacha kuitwa "Draft Protocol?" Na huko kumiliki mali patakuja overnight? Mbona sheria za uwekezaji, umiliki ardhi, uhamiaji, etc bado hazijabadilishwa? Na kama zikibadilishwa hatujui zitachukua sura gani! Hebu soma paragraph zifuatazo:
4. The free movement of persons shall not exempt from prosecution or extradition, a national of a Partner State who commits a crime in another Partner State.

5. The free movement of persons shall be subject to limitations imposed by the host Partner State on grounds of public policy, public security or public health.

6. A Partner State imposing a limitation under paragraph 5, shall notify the other Partner States accordingly.

1. Je, ni lini itaachwa kuitwa 'Draft protocol'?

2. Je, sheria zipi ambazo zimerekebishwa kukidhi hiyo protocal?

3. Je, Tanzania itafaidika vipi kwa kuingia nchini wahamiaji wengi kutoka Rwanda/Burundi ambako kuna uhaba wa ardhi? Kenya ambao wameuza literally ardhi yao yote kwa wageni?

4. Kauli mbiu ya CCM ya ajira itafanikiwa vipi wakati nafasi zilizopo zitakuwa kwa raia wote wa EAC nchini Tanzania?

5. Sio siri kutakuwa na mafuriko ya wahamiaji kutoka nchi jirani kuanzia Julai, Kenya tayari wamejiandaa kuwaleta raia wao nchini Tanzania kwa wingi inavyotakiwa, Je Tanzania imejiandaa vipi na hili wimbi la wageni?
 
Sheria za Tanzania ni chini ya sheria za EAC:


[FONT=IGKDLD+Calibri]2.3 The Common Market shall be managed in accordance with the [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]relevant laws of the Community[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri].[/FONT]

[FONT=IGKDLD+Calibri]Which means, Bunge la Tanzania ni chini ya lile la EAC. Haiwezekani kwa Bunge la Tanzania kubadili maamuzi ya EAC: nafasi ya mwisho ya Wabunge kubaki na madaraka yao ni Tanzania kujitoa EAC.[/FONT]

[FONT=IGKDLD+Calibri]2.5 The establishment of the Common Market [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]shall[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri], notwithstanding paragraph 1, [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]be progressive[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri].[/FONT]

[FONT=IGKDLD+Calibri]Documenti itabadilishwa kadiri EAC inavyopenda huko baadaye.[/FONT]

[FONT=IGKDLD+Calibri]Mkataba upi ambao watawala wa Tanzania wamesaini ambao sisi Watanzania tumewazidi kete wale wengine? Mikataba mingapi ambayo watawala wa Tanzania wamesaini ambayo sisi Watanzania tumezidiwa kete?[/FONT]

[FONT=IGKDLD+Calibri]5.1 The provisions of this Protocol shall apply to [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]any[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] activity undertaken in cooperation by the Partner States to achieve the free movement of goods, persons, labour, services and capital and to ensure the enjoyment of the rights of establishment and residence of their nationals within the Community.[/FONT]


[FONT=IGKDLD+Calibri]10.9[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] The national laws[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] and administrative procedures of a Partner State[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] shall not appl[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]y[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] where the principal aim or effect is to deny citizens of other Partner States the employment that has been offered.[/FONT]

[FONT=IGKDLD+Calibri]Kwa hiyo kule Dodoma watakuwa wanacheza mchezo wa kuigiza tu, kama bado hawajaanza...[/FONT]


[FONT=IGKDLD+Calibri]13.5 The Partner States shall [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]ensure[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] that [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]all[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] restrictions[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] on the [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]right[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] of establishment based on the nationality of companies, firms and self employed persons of the Partner States [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]are removed[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri], and [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]shall not introduce any new restrictions[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] on the right of establishment in their territories, [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]save as otherwise provided in this Protocol[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri].

[/FONT]​
[FONT=IGKDLD+Calibri]Kiswahili kingine, hizo sheria zenu zilizotungwa na bunge-toto hazina nafasi pale sheria hizi za Bunge lenyewe EAC zinapohusika. Na hata kama watatunga sheria nyingine, zitakuwa ni kujifurahisha tu, jambo ambalo ni haki yao ya kikatiba...


[/FONT]​
[FONT=IGKDLD+Calibri]13.7 For the purposes of undertaking [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]any[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] economic activity[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] in accordance with the provisions of this Article, the Partner States shall mutually [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]recognize[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] the relevant experience obtained, requirements met, [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]licenses[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri] and certificates granted to a company or firm [/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri]in the other Partner States[/FONT][FONT=IGKDLD+Calibri].[/FONT]​

[FONT=IGKDLD+Calibri]Mwisho wa BRELA... Mtu anaingia na ‘kipande' chake toka kwao, ambacho kinaonyesha ana kampuni, ana leseni, mwisho wa reli. Vijisheria vyenu havina nafasi. Anapeta tu...[/FONT]
 
Wacha1:

1. Je, ni lini itaachwa kuitwa 'Draft protocol'?

2. Je, sheria zipi ambazo zimerekebishwa kukidhi hiyo protocal?

3. Je, Tanzania itafaidika vipi kwa kuingia nchini wahamiaji wengi kutoka Rwanda/Burundi ambako kuna uhaba wa ardhi? Kenya ambao wameuza literally ardhi yao yote kwa wageni?

4. Kauli mbiu ya CCM ya ajira itafanikiwa vipi wakati nafasi zilizopo zitakuwa kwa raia wote wa EAC nchini Tanzania?

5. Sio siri kutakuwa na mafuriko ya wahamiaji kutoka nchi jirani kuanzia Julai, Kenya tayari wamejiandaa kuwaleta raia wao nchini Tanzania kwa wingi inavyotakiwa, Je Tanzania imejiandaa vipi na hili wimbi la wageni?

1. Iliacha kuwa Draft pale Rais alipoisaini.

2. Kwa nini wabadilishe sheria, ikiwa wanaridhia mkataba huu?

3. Huo ndio utakuwa mwisho wa Jamhuri ya Tanzania... ni jambo la kusikitisha, lakini wanaopembejea mambo haya wanadhani wao hayatawagusa...

4. CCM itakuwa 'redundant' kwa vile maneno yote yatakuwa EAC.

5. Hamna njia yoyote ya kuzuia madhara ya EAC, isipokuwa kwa Tanzania kujitoa. "Nyie Burundi, Rwanda, Kenya, na Uganda si mko wanne, sisi tunajitoa kwa muda ili tushughulikie matatizo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Pindi tukiyamaliza tu tutajiunga nanyi..."
 
Buchanan,

Unakumbuka lile shairi la "Kwetu ni kwao kwa nini?"; kama yupo mtu anajidanganya kwamba mkataba huo utatekelezwa sawa hizo nchi nyingine kama ambavyo utatekelezwa Tanzania, atakuwa anajidanganya.

Vipengele hivyo vipo kuhakikisha kwamba Watanzania tutakapokuwa tumetimuliwa nchini mwetu hatutaweza kwenda kwao.
 
Mlenge sijaona bado unachekelea nini wakati ulichokizungumzia ni "Draft Protocol" na sio Protocol iliyopitishwa na Wakuu wa nchi husika. Na hakuna mahali popote ambapo pameonyeshwa kwamba mipaka haitakuwepo kama ulivyoanza kueleza hapo juu. Nilichoona ni kwamba "some restrictions" zitaondolewa na hakuna mahali popote ambapo Sheria za "Territory" nyingine zitakuwa non-functional! After all unanipa mashaka kama wewe kweli ni Mtanzania hasa pale "unapoona huruma" eti kwa wasomali, wanyarwanda, etc na kutokuona huruma kwa watanzania watakaokosa ardhi ambayo inaweza kuvamiwa na wageni!

Buchanan,

Tusipobakia kwenye EAC, hata kama ikiwa ni ujuha mtupu kwa Tanzania kuendelea kuwepo, hatuwezi kuacha, kwa vile itaonekana "ni waoga", "tunakimbia ushindani", "hatukusoma", halafu tutakosa sifa duniani za kuonyesha "na sisi Waafrika tunaweza kuungana!".

Halafu baadhi ya watu 'machizi' wanasema kwamba watawala wetu wanachukulia EAC kuwa ni sehemu nyingine 'ya ulaji', kwa hiyo kujitoa EAC kutasababisha 'wabanane' majimboni...

Halafu makao makuu ya EAC yapo Arusha, japo manufaa yake kwa wananchi ni suala la mjadala, huoni ni sifa Arusha inapoandikwa na mashirika ya habari ya kimataifa kama vile Reuters?
 
Ladies and Gentlemen,

With regard to the East African Community, I would rightly brag that things are on course. We have made remarkable progress so far and the prospects for the future look very promising.
As you know, in 1996, we started with cooperation among the three partner states of Kenya, Tanzania and Uganda. There were some few sectors which were designated for that purpose. Three years later in 1999 a bold decision was taken to go for integration. It was agreed on the stages to follow with the Customs Union being the entry point to be followed by the Common Market, then the Monetary Union and Political Federation being the ultimate.
Since January, 2005 the East African Community member states have implemented the Customs Union phase with great success. Next year, the Customs Union will reach maturity when goods from Kenya will enjoy the no-tariff facility on export to other member states. But, as the Customs Union matures, we are surely going to graduate on to the next phase of the Common Market. The negotiations are almost complete. What is now being awaited is the Summit of Heads of States of the EAC for conclusion and endorsement.

So far the community has worked well for Tanzania. We have witnessed phenomenon increase in our trade within the East African Region to the extent that we have a trade surplus with Kenya. This is something which almost looked unimaginable when we were negotiating the Community Treaty before 1999. It has demonstrated in real terms that nothing is impossible. I firmly believe that the East African Community offers great potential for Tanzania to benefit even more in the years ahead.

-- Jakaya Kikwete, November 5 2009 (emphasis added). http://mawasilianoikulu.blogspot.com/2009/11/presidents-adress-at-economist.html

Huree!

Tanzania sasa ina surplus kwenye balance ya trade na Kenya! Bring'Em on!

I rest my case!
 
Kwani ikisainiwa na Rais ndio inaacha kuitwa "Draft Protocol?" Na huko kumiliki mali patakuja overnight? Mbona sheria za uwekezaji, umiliki ardhi, uhamiaji, etc bado hazijabadilishwa? Na kama zikibadilishwa hatujui zitachukua sura gani! Hebu soma paragraph zifuatazo:
4. The free movement of persons shall not exempt from prosecution or extradition, a national of a Partner State who commits a crime in another Partner State.

5. The free movement of persons shall be subject to limitations imposed by the host Partner State on grounds of public policy, public security or public health.

6. A Partner State imposing a limitation under paragraph 5, shall notify the other Partner States accordingly.
Sasa huu ndiyo tunaita ubishi
The president of the Republic has already signed. That is one step; big step towards approval. You know very well our pariliament is a corrupt rubber stamp "agency"; wewe uoni kuwa tayari tumekwisha na sasa we have been put into a doubtfu atmosphere?
Kwanza ungejiuliza kitu kimoja; why we need all this shit? Sisi tunazoadvantage zote ambazo hatuhitaji nchi nyingine. Na chi hizi ambazo tunataka kuungana nazo hazina kitu cha kutusaidia. Ardhi yetu ni kubwa, watu kwetu ni wengi, tuna bahari, arable land, waterways, rails and a very United popuplation.
Mie naunga mkono kabisa kuwa watawala wetu lazima hawana akili zuri. WE have to negotiate a better deal than this because we are a better place than others.

"----- Wepesi wepesi"
 
Hivi suala la ardhi kuna clause yeyote inayoelezea inshu itakuwaje? Maana hapo so far naona ishu ni ukazi, kukaa sio kumiliki ardhi. Au?
 
Abdulhalim,

Mtu atakuwa ni resident bila kukaa kwenye ardhi?

Ona habari hii:

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala, amewatahadharisha wageni kuwa ardhi ya Tanzania haitatolewa kwao kinyemela, isipokuwa kwa wale wenye mipango madhubuti na ya kweli ya uwekezaji.

Akizungumza katika mkutano wa wafanyabiashara wa Rwanda na Tanzania mjini Kigali Dk. Kamala, alisema Serikali ya Tanzania iko makini mno katika suala la ardhi, lakini hiyo haina maana kwamba itawazuia watu wenye nia ya kweli, kwenda kuwekeza nchini humo.

``Ardhi tunayo kubwa na nzuri, kama mgeni anataka kuwekeza katika kilimo au ujenzi wa nyumba, aje, suala kubwa ni kwamba aje na mpango ulio wazi na ulio makini.

``Kama anakuja akitaka ardhi tu kwa ajili ya kukamata ardhi, huyo hawezi kuipata, ardhi ni mali ya Serikali na inatolewa kwa wawekezaji makini wenye nia ya kweli ya kuwekeza,`` alisema.

Habari kamili ipo hapa.

******************

Kwa hiyo Abdulhalim, akija mwekezaji anayetaka kulima au Kujenga Nyumba, ni yeye tu na roho yake!

Kulima inaweza kuwa analima pori, au majani ya ng'ombe, macho yenu tu yanaona hajafanya chochote; kujenga anaweza kujenga nyumba ya makuti, mradi tu amewekeza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom