Tanzania Government to probe alleged secret CDM party financing

Swali moja tu hivi mnaotetea huo ufadhili wa nje ni wajinga au mna maslahi binafsi?
Si wajinga wala wabinafsi lakini kwa kuwa tunajua hakuna na ni dhahiri hakuna ufadhili wowote kutoka nje kwenda kwa CDM zaidi ya propaganda za ccm. Lengo ni kutufanya watanzania tuichukie CDM wakati tunajua aliyoongea Nape ni propaganda za kutuziba macho watanzania ili fedha zilizowekwa nje na mafisadi wa ccm zifichwe kilaini.
Kwahiyo ni kwamba sisi ni werevu kuliko propaganda za ccm na Nape wake. Hakuna ushahidi wowote alionao Nape, wala hakuna uchunguzi wowote utakaofanywa na Mizengo pinda na serikali yao kwa kuwa wanajua hata wakichunguza wataumbuka wenyewe. Hizo zote ni propaganda zilizopangwa kuanza na Nape, mbunge kuuliza swali kisha waziri mkuu kujibu kufanya uchunguzi. Lakini hatudanganyiki ng'o. Bila shaka Ecoli sasa unajua uko kwenye kundi gani wajinga ua werevu? Kama mpenzi wa magamba sikushangai lakini ujue watanzania wa sasa ni zaidi ya fikra hizi fupi za ccm.
 
Ndio tatizo la nchi kuongozwa na watu wenye matatizo ya akili, kama hizo pesa zimeingia nchini na kunazinazotoka tena trilions of money watu hawachukuliwi hatua,,,,,,,,,,,,,,,, kunamatatizo makubwa hapa . Bado madi, arith za wananchi inapolwa na maliasili nyingi tu huibwa bila kuchukua hatua kweli viongozi wa serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania ni dhaifu kwelikweli.
 
Kwani hivi CCM na Serikali si kitu kimoja? sasa UChunguzi wa nini wakati nape Ninauye Anao tayari wauchukue na kuishitaki CHAdema Kama ni kweli...

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kwani hivi CCM na
Serikali si kitu kimoja? sasa UChunguzi wa nini wakati nape Ninauye Anao
tayari wauchukue na kuishitaki CHAdema Kama ni kweli...

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

uchunguzi ni mzuri. ila usishangae wakikaa kimya baada ya kukosa ushahidi!
 
Nilichojifunza kwenye baraza hili ni kwamba wajumbe wa baraza hawataki chadema ichunguzwe. Nitamtafuta Pasco (a.k.a mzee wa inside stories)nimuulize kama anajua sababu ya wajumbe wa baraza kupinga uchunguzi.
 
Last edited by a moderator:
Nilichojifunza kwenye
baraza hili ni kwamba wajumbe wa baraza hawataki chadema ichunguzwe.
Nitamtafuta Pasco (a.k.a mzee wa inside
stories)nimuulize kama anajua sababu ya wajumbe wa baraza kupinga
uchunguzi.

wangapi ccm wamechunguzwa?
 
Last edited by a moderator:
Hayo mabilioni yalikuja kama dollar au Tsh?Kama ni USD basi mabenk yatakuwa na dollar ambazo serikali itayatumia kununulia vitu nje.Kama ni hela za madafu lazima ziwe fake ili ziweze toka kwa hao donors.Otherwise kubadili hayo mabilioni si rahisi kaa wanavyoaka tuaminisha.Kubadili Dollar kuanzia millioni ndio zitaanza ingia katika Tsh billion+Na huwezi wapa wafanyabiashara kirahisi wakupe tsh.Kwani huwa dollar zinabanwa sana kila nchi katik dunia ya leo na kiasi hicho ni soo.

Ila isijekuwa hela za wabongo walio nje alizochonga ndizo tunataka lishwa *****?
 
Hela chafu? EPA, change ya RADA, Deep Green, Meremeta, Kagoda, mabilioni Uswiss na sasa Dangote!

Hata hivyo Pinda asipate shida sana, Nape alidai anayo majina ya nchi zinazotoa hela "chafu" kwa makubaliano maalum.

Jamani nashindwa hata niseme nini. Inakuwaje hawa CCM wanakuwa na tabia za ajabu hivi? Nape ni nani? Ama kweli serikali hii ni kichekesho. Inapewa amri na watu walio nje ya serikali ilimradi ni kada wa CCM na inakwenda kichwa kichwa? Huu ni uwenda wazumu wa aina yake. Masuala mazito mengi hayajatolewa majibu wanahangaika na such things?
Wanahaha mwisho unakaribia!!!
 
Nilichojifunza kwenye baraza hili ni kwamba wajumbe wa baraza hawataki chadema ichunguzwe. Nitamtafuta Pasco (a.k.a mzee wa inside stories)nimuulize kama anajua sababu ya wajumbe wa baraza kupinga uchunguzi.
Hao wajumbe wa baraza ni akina nani?
Chadema ndio waliwaambia serikali ya Magamba iwataje hao wanaoipa hizo fedha hadharani, isiwe na kigugumizi na wakaenda mbali zaidi wakamwandikia msajili wa vyama vya siasa kuchunguza na kumchukulia hatua Nape ikijulikana amesema uongo na wakaomba vyama vyote vikaguliwe na CAG na ripoti iwekwe wazi.
wangapi ccm wamechunguzwa?

Kwani hivi CCM na Serikali si kitu kimoja? sasa UChunguzi wa nini wakati nape Ninauye Anao tayari wauchukue na kuishitaki CHAdema Kama ni kweli...

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Tunajua kazi ya Nape ni ama ametumwa ama ameropoka. Ila sasa tunahitaji waseme ukweli waweke wazi, fedha zozote zile zikiingia nchini lazima mabenki ama ya hapa ama ya nje yajue. Haiwezekani cdm wakaingiza fedha serikali ikakaa kimya wakati fedha hizo zitawaletea madhara ya kuwatoa madarakani. Kila mtu anajua wenye fedha chafu ni CCM.

Huu mchezo ni ahadi ya Wasira kuimaliza CDM in one year. Walianza na Zitto kumwita mla Rushwa naona hilo linawashinda sasa wanahamia kwenye chama. CCM wanapumua kwa taabu sana ila siku zao zinahesabika.
 
Kaka hebu tumegee kuhsu hlo sakata tulielewe vyema kaka.

Kuhusu uuzaji wa silaha kufadhili mgogoro wa DRC. Kama unakumbuka kuna tume ya uchunguzi iliundwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa na mwaka 2008 ilitoa taarifa ya awali kuwa Tz inahusika na ku-supply silaha maziwa makuu. Tena kuna baadhi ya figures walitajwa. Namkumbuka Maj. Gen Mdolwa aliyekuwa mwambata Burundi (alikuwa ana-link) na vigogo wa chama tawala alidaiwa kuhusika. Ndiposa mh. Membe aliijia juu UN kutaka Tz tuombwe radhi kwa kuchafuliwa lakini UN ikajibu kuwa hiyo ni dondoo tu ya yaliyomo lakini ripoti kamili haijakabidhiwa UN hivyo hawana cha kujibu. Nakumbuka ile tume iliongezewa muda wa uchunguzi, sasa sijui baada ya hapo mambo yaliishia wapi.
 
Ni lini chama tawala kiliwatangazia wanachama wake kwamba kimepokea msaada wa fedha kutoka nje? Au akijawahi kupewa msaada wowote. Je, ni kosa kwa chama cha siasa kupokea msaada wa fedha kutoka nchi za nje?

Benki kuu imekauka? Wao wanachukua huko.
 
Back
Top Bottom