Tanzania earning 1.9 in mines!

Bajameni,

Mimi si mchumi, bali mbwabwajaji. Sasa if madini ambayo ni 1.9% ya GDP ya Taifa yanaingiza 50% ya forex, then something is wrong on this picture. It means kuwa hizo 98.1% ya GDP hazina nguvu za kutuleta japo 98.1% ya Forex?

bado sielewi kwa nini Madini ambayo ni tosha kuchukua japo 30% ya GDP yawe ni kiwango kidogo hivyo.

Binafsi ningependa Madini yaweze kuwa na contribution kubwa kwenye GDP, hata hivyo nisingependa sekta kama hiyo ichukue 30%! Kwanini nasema hivyo Jibu ni kwamba Lazima Sekta zinazoajiri watu wengi, sekta zenye risk ndogo ndio zishike uchumi wa nchi nazo ni Kilimo,,, Leo hii sekta ya madini ikichangia sema 50% kwa mfano siku madini ya namna fulani yakishuka bei tumeliwa!!! Ndio maana nimesema hiyo percentage inadepend sekta zingine zinafanya nini!!!

Leo sekta ya madini kwa mfano ikichangia 90% ya GDP maana yake Watanzania hatufanyi kazi tunategemea sekta moja na ambayo umiliki wa wenyewe wa hiyo migodi sio wetu... hivyo kuliweka taifa kwenye risk.
 
wakaitumia Stamico kuwa at least 40% owners wa Uzalishaji madini ili tupate japo 40% ya earnings?

Kwani Ardhi na Watu si wetu? mtaji pesa na Mitambo ndio vya Barrick (60%)?

Jee, hiyo ardhi, watu na STAMICO havikuwapo miaka zaidi ya 40 tokea enzi za ujamaa? Au unafikiri mradi wa migodi na kuchimba mafuta ni masihara? Unajua si vitu vingi Watanzania wanaweza kufanya na vikafanikiwa zaidi ya ku-organize vikao vya michango ya harusi na mikutano ya CCM Dodoma.
 
Binafsi ningependa Madini yaweze kuwa na contribution kubwa kwenye GDP, hata hivyo nisingependa sekta kama hiyo ichukue 30%! Kwanini nasema hivyo Jibu ni kwamba Lazima Sekta zinazoajiri watu wengi, sekta zenye risk ndogo ndio zishike uchumi wa nchi nazo ni Kilimo,,, Leo hii sekta ya madini ikichangia sema 50% kwa mfano siku madini ya namna fulani yakishuka bei tumeliwa!!! Ndio maana nimesema hiyo percentage inadepend sekta zingine zinafanya nini!!!

Leo sekta ya madini kwa mfano ikichangia 90% ya GDP maana yake Watanzania hatufanyi kazi tunategemea sekta moja na ambayo umiliki wa wenyewe wa hiyo migodi sio wetu... hivyo kuliweka taifa kwenye risk.

Kwa hiyo hata kama bei ya dhahabu duniani ikiongezeka na kufikia $2,000 kwa ounce moja bado unataka tuendelee kupata 1.9%! Wewe ni nani hasa katika serikali ya Tanzania mpaka uamue sekta ya madini ichangie kiasi gani katika pato la Taifa? :confused:
Usiangalie sekta inaajiri watu wangapi bali ni lazima uangalie pia kwamba dhahabu inaongezeka bei kwa kasi sana.
 
Madini ndiyo kimojawapo kati ya tulivyojaliwa.Hivyo inatakiwa tutokee hapo hapo maana hatuwezi vingine vingi.Kwa taarifa yako madini kama gold kushuka bei siyo rahisi,ila innazidi kupanda.Mfano mdogo ni nchi kama ujerumani hazina yao wameiweka kama gold reserves, siyo manoti.Hivyo katika central benki yao huko Frankfurt ni magold tuuu!!Kumbuka hilo ni taifa la tatu tajiri duniani linalomiliki 2/3 ya uchumi wa ulaya yote.
 
Binafsi ningependa Madini yaweze kuwa na contribution kubwa kwenye GDP, hata hivyo nisingependa sekta kama hiyo ichukue 30%! Kwanini nasema hivyo Jibu ni kwamba Lazima Sekta zinazoajiri watu wengi, sekta zenye risk ndogo ndio zishike uchumi wa nchi nazo ni Kilimo,,, Leo hii sekta ya madini ikichangia sema 50% kwa mfano siku madini ya namna fulani yakishuka bei tumeliwa!!! Ndio maana nimesema hiyo percentage inadepend sekta zingine zinafanya nini!!!

Leo sekta ya madini kwa mfano ikichangia 90% ya GDP maana yake Watanzania hatufanyi kazi tunategemea sekta moja na ambayo umiliki wa wenyewe wa hiyo migodi sio wetu... hivyo kuliweka taifa kwenye risk.

Trinidad and Tobago walikuwa wazalishaji wakubwa sana wa sukari na uchumi wao ulikuwa unategemea zao hilo pamoja na Utalii...................hivi sasa wana mafuta.........sasa wee nenda Trinidad ukaone yale mashamba ya miwa na vile viwanda vya sukari viko ktk hali gani ambavyo vilikuwa vikiajiri wa-Trinbagonians.........in thousands......i mean....noo!! give me a break.....Kilitime there are levels of risks to be determined with time and quantity of natural resources kama madini ambayo tunayo.

makampuni yanayochimba mafuta ni kutoka US, Canada na UK na ni local wachache sana wanaonufaika na ajira ktk hayo makampuni...................sasa check mikataba yao ilivyo....halafu wala sio siri kama ambavyo sisi huku Tanzania.

Kilitime hebu angalia hizi nchi vizuri ambazo binafsi nimepata kuishi huko japo kwa vipindi si virefu sana
Trinidad and Tobago
Venezuella
Singapore
South Korea
Botswana
Angola

angalia chumi zao zinavyokua........................halafu linganisha na

Tanzania
Zambia
Congo DR
Nigeria

then talk about the risks

Yes, uchangiaji wa sekta ktk uchumi unategemea sana sekta zingine zinazalisha/zinaingiza vipi........however kigezo chako cha RISKS kisitufanye ku-play LOW na kusaini mikataba ya KIFISADI...............there is no reason whatsoever WHY WE SHOULD NOT BENEFIT SIGNIFICANTLY FROM OUR NATURAL RESOURCES
 
Bajameni,

Mimi si mchumi, bali mbwabwajaji. Sasa if madini ambayo ni 1.9% ya GDP ya Taifa yanaingiza 50% ya forex, then something is wrong on this picture. It means kuwa hizo 98.1% ya GDP hazina nguvu za kutuleta japo 98.1% ya Forex?

Naomba mwenye proper break down ya exports zetu aiweke hapa, na zaidi hii GDP yetu ni kutokana na uzalishaji mali na mauzo bila "misaada"?

bado sielewi kwa nini Madini ambayo ni tosha kuchukua japo 30% ya GDP yawe ni kiwango kidogo hivyo.

If barrick can earn Billions of dollars, from Gold of tanzania, why are getting a mere hundred thousand or a million? does this make sense to anyone? Kwa nini Serikali isitumie zile pesa walizobwaga Meremeta, Tangold, Mwananchi na Deep Green wakaitumia Stamico kuwa at least 40% owners wa Uzalishaji madini ili tupate japo 40% ya earnings?

Kwani Ardhi na Watu si wetu? mtaji pesa na Mitambo ndio vya Barrick (60%)?

Kutoka wikipedia GDP: The most common approach to measuring and understanding GDP is the expenditure method:
GDP = consumption + investment + (government spending) + (exports − imports), or, GDP = C + I + G + (X-M)
"Gross" means depreciation of capital stock is not included. With depreciation, with net investment instead of gross investment, it is the net domestic product. Consumption and investment in this equation are the expenditure on final goods and services. The exports minus imports part of the equation (often called cumulative exports) then adjusts this by subtracting the part of this expenditure not produced domestically (the imports), and adding back in domestic area (the exports).

Google wikipedia kupata definition zaidi kama unapenda.

Hii hapa chini kutoka Shirika la Ujasusi la Marekani:

GDP (purchasing power parity) $ 29.64 billion (2006 est.)
GDP (official exchange rate) $ 13.14 billion (2006 est.)

GDP real growth 5.9% (2006est.)

GDP per capita (PPP) $ 800 (2006 est.)

GDP composition by sector:

Agriculture: 43.2%
Industry: 18.1%
Services: 38.7% (2006 est.)
Labour force by sector Agriculture 80%
Industry and services 20%

Population below poverty line 36%

Exports $ 1.798 billion FOB (2006 est.)
(gold, coffe, cashew nuts, manufactures, cotton.)

Exports partners China 9%, India 8.9%, Netherland 6.3%, Japan 5.4%, UAE 4.3%, Germany 4.3% (2006 est.)

Imports $ 4.369 billion FOB (2006 est.)
Import commodities: consumer goods, machinery and transportation equipment, industrial raw materials, crude oil.

Imports partners: South Africa 9.7%, China 9.3%, Kenya 7.8%, India 6.7%, UAE 5.9%, Zambia 5.7% (2006)

Economic aid recipient $ 1.2 billion (2001) I don't know recent figures.
Reserve Foreign exchange and gold $ 2.281 billion (2006 est.)

Debt external $ 4.786 billion (2006 est.)
 
Binafsi ningependa Madini yaweze kuwa na contribution kubwa kwenye GDP, hata hivyo nisingependa sekta kama hiyo ichukue 30%! Kwanini nasema hivyo Jibu ni kwamba Lazima Sekta zinazoajiri watu wengi, sekta zenye risk ndogo ndio zishike uchumi wa nchi nazo ni Kilimo,,, Leo hii sekta ya madini ikichangia sema 50% kwa mfano siku madini ya namna fulani yakishuka bei tumeliwa!!! Ndio maana nimesema hiyo percentage inadepend sekta zingine zinafanya nini!!!

Leo sekta ya madini kwa mfano ikichangia 90% ya GDP maana yake Watanzania hatufanyi kazi tunategemea sekta moja na ambayo umiliki wa wenyewe wa hiyo migodi sio wetu... hivyo kuliweka taifa kwenye risk.

Kweli kabisa mkuu.
Madini yakiachiwa asilimia kubwa sana ya uchumi kutakuwa na matatizo iwapo madini hayo yatashuka thamani katika soko la dunia. Tukumbuke jinsi shaba ilivyoutesa na kuuporomosha uchumi wa Zambia baada ya kukosa bei nzuri katika soko la dunia miaka kadhaa hapo nyuma. Tusifike huku.
 
Uchumi unabadilika kila leo. Leo mazao ya biashara kama kahawa,, pamba n.k. yanaweza yakawa yameshuka bei katika soko la dunia na wakati huo huo bei ya dhahabu imeongezeka kwa kiwango kikubwa sana. Hivyo siyo siri kwamba mchango wa dhahabu katika pato la Taifa unatakiwa nao pia uongezeke ukilinganisha na kilimo. Ni kweli bei ya dhahabu inapanda na kushuka, na hiyo ni nje ya uwezo wa nchi zenye dhahabu. Kama bei y dhahabu inapanda basi hakuna cha ajabu chochote kuona dhahabu inachangia hata asilimia 50% ya pato la Taifa. Ndio uchumi ulivyo! na ni kichekesho kusema kwamba dhahabu isichangie asilimia kubwa ya pato la Taifa kwa sababu ikishuka bei kutakuwa na matatizo! :confused:
 
wazee mbona trade balance deficit ni kubwa sana hapo(Export-import)? vitu kama hivi ndio vinatufanya tunazidi maskini na shilling yetu kushuka bila break!
 
Uchumi unabadilika kila leo. Leo mazao ya biashara kama kahawa,, pamba n.k. yanaweza yakawa yameshuka bei katika soko la dunia na wakati huo huo bei ya dhahabu imeongezeka kwa kiwango kikubwa sana. Hivyo siyo siri kwamba mchango wa dhahabu katika pato la Taifa unatakiwa nao pia uongezeke ukilinganisha na kilimo. Ni kweli bei ya dhahabu inapanda na kushuka, na hiyo ni nje ya uwezo wa nchi zenye dhahabu. Kama bei y dhahabu inapanda basi hakuna cha ajabu chochote kuona dhahabu inachangia hata asilimia 50% ya pato la Taifa. Ndio uchumi ulivyo! na ni kichekesho kusema kwamba dhahabu isichangie asilimia kubwa ya pato la Taifa kwa sababu ikishuka bei kutakuwa na matatizo! :confused:

exactly!!...........kwa kweli ni kichekesho...............yaani napata picha ya kwamba.............kuna watu wanatoa baraka ya kwamba mchango wa madini kwa pato la Taifa usiszidi certain percentage............in a way una-allow some %ges kufisadiwa!!!! simply because you see only 1.9% ndio halali yetu
 
Waswahili walikwisha sema tangu zamani kwamba limbukeni hana siri. Unawezaje kuwa na nyumba nzuri ya ghorofa na kila kitu ndani yake na usitake kwenda kulala huko (au kuitumia) kwa kuogopa kwamba likitokea tetemeko nyumba hiyo inaweza kuanguka.
 
Binafsi ningependa Madini yaweze kuwa na contribution kubwa kwenye GDP, hata hivyo nisingependa sekta kama hiyo ichukue 30%! Kwanini nasema hivyo Jibu ni kwamba Lazima Sekta zinazoajiri watu wengi, sekta zenye risk ndogo ndio zishike uchumi wa nchi nazo ni Kilimo,,, Leo hii sekta ya madini ikichangia sema 50% kwa mfano siku madini ya namna fulani yakishuka bei tumeliwa!!! Ndio maana nimesema hiyo percentage inadepend sekta zingine zinafanya nini!!!

Leo sekta ya madini kwa mfano ikichangia 90% ya GDP maana yake Watanzania hatufanyi kazi tunategemea sekta moja na ambayo umiliki wa wenyewe wa hiyo migodi sio wetu... hivyo kuliweka taifa kwenye risk.

I agree with you with the fear of price fluctuation and risks involved. However the good years of getting 30-50% contibution from Mining could help with other developments that will create suitable environment for country progression. We should use the neema out mapato ya madini (as capital) kuboresha huduma za jamii, kujenga mitandao bora (barabara, reli,umeme, simu, maji) na kufungua milango ya maendeleo ambayo itazalisha ajira na kukuza uzalishaji mali mwingine kama Kilimo, Ufugaji nk.
 
Jee, hiyo ardhi, watu na STAMICO havikuwapo miaka zaidi ya 40 tokea enzi za ujamaa? Au unafikiri mradi wa migodi na kuchimba mafuta ni masihara? Unajua si vitu vingi Watanzania wanaweza kufanya na vikafanikiwa zaidi ya ku-organize vikao vya michango ya harusi na mikutano ya CCM Dodoma.

If Angola, Botswana, Chile, Venezuela can do it, why not Tanzania? why are you giving in that you are incompetent to run an efficient economy and industries and you give up?

A little bit of inferiority complex out of bitter dosage ya ukoloni?
 
Canada now dominate the world, currently Canadian dollar is higher than USD. One of the reason is Gold and Oil. Tanzania should ask for Gold and not dollars, USD is decreasing while Gold value is increasing.
 
Kilitime,
Binafsi ksikuwepo hapa toka majuzi lna nimejaribu kupitia baadhi ya hoja huko nyuma lakini kazi yake imekuwa kubwa sana.... Ila nachotaka kuchagia hapa ni kwamba ni lazima tume wakweli na hali halisi pia tuwe wazi kutambua mchango wa kitu ktk maisha yetu. Tulitazame swala hili kwa undani zaidi na kutoa maoni yetu ambayo yataweza kuwa funuo kwa wengine.

Sasa basi, labda kwa uharaka itabidi nizungumzie sehemu mbili, kwanza ni hii ya mchango wa madini ktk GDP. Binafsi na tukilitaza swala hili kitaalam haiwezi kuwa mbaya ikiwa madini yatachangia asilimia 30, 50 ama 70 kwa sababu madini hayatoi ajira kubwa kiasi kwamba yakija kwisha wananchi wengi watakuwa hawana kazi. Ila Kinachotakiwa kwetu ni kuhakikihsa mchango wa madini ktk mfuko wa taifa ni mkubwa sana faida yake kubwa kiasi kwamba tupo radhi kuchukua risk ya kuachiwa mashimo, kesho tutajenga subway (underground train).

Tatizo ndio kama hivyo ulivyoona ni asilimi 1.9 tu inayochangia mfuko wetu wajomba wanaondoka na kila senti..
Pili nimeona mahala uki question hiyo 1.9 ni kiasi gani na kuwa yawezekana kuwa na fedha nyingi sana tena basi ukafikia kuzunguzia habari za Ukuaji uchumi..

Hapa mjomba kidogo ulitoka nje ya swala muhimu mezani nalo ni huo mchango wa 1.9 kwa sababu kama utataka kujua kiasi chake basi bora pia utafute kujua ile 98.1 ni kiasi gani?..Kwa hiyo mchango huu na ukuaji wa uchumi ni vitu viwili tofauti kabisa..

Mchango wa mfuko wetu ni ujazo wa mali safi ktk gunia letu moja, wakati Ukuaji wa uchumi huwekwa magunia yote pamoja na pumba zke ktk mzani na kutazama tofauti ya uzito wa gunia (ongezeko ama pungufu) hilo na lile la mwaka jana no matter what's inside!

Mjomba, hata kama hiyo 1.9 iwe Usd billioni 10 ukasema sii mnaona nyingi sana hizi, lakini usije sahau tu kuwa mchango wa vitu vingine ni Usd billioni 98.1!.. hapa kinachotupa sifa ni hiyo 98.1 ya vitu ambavyo havipo kabisa ktk akili zetu. Ndio maana nikasema huko nyuma kuwa sioni faida ya madini hata kidogo na bora tubakie na hivyo vinavyoingiza hiyo asilimia 98.1 fo any amount kuliko kuuza miili yetu kama vile sisi ni ma Changudoa, Umalaya usokuwa na hadhi wala faida.
 
Na Buzwagi uliosainiwa juzi juzi baada ya kelele chungu nzima za Watanzania mbona bado mlisaini mkataba bomu!?

Posted Date::11/19/2007
Masha adai wawekezaji wa madini waligoma

Na Frederick Katulanda, Mwanza
Mwananchi

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha amesema wawekezaji katika sekta ya madini nchini waligoma kubadilisha mikataba yao kwa madia ni makubaliano hali yaliyokuwa yamekwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini.

Mashaalisema hayo, wakati akijibu hoja mbalimbali zilizoibuka katika kongamamo la kuadhimisha Siku ya Wananfunzi Duniani katiika Chuo Kikuu cha Matakatifu Augustino (SAUT).

Alisema kosa lilifanyika awali wakati wa kuandaasheria ambapo sheria hiyo iliwekwa kwa lengo la kuwavutia wawekezaji wa sekta ya madini.

Masha alisema sheria iliyokosewa katika kukaribisha wawekezaji hao wa madini ni kuwekwa kwa sheria iliyoruhusu mwekezaji kusamehewa kulipa kodi kiasi cha asilimia 15 ya mtaji wake (15 % addition capital allowance).Mimi nikiwa Naibu Waziri wa Madini na Nishati nilikuwa miongoni mwa

wajumbe waTume ya kwanza ya kupitia sheria hiyo, tulikwenda kwa wawekezaji lakini waligoma wakidai kuwa tulishaingia mikataba nao na kutisha kwamba watatutangaza kuwa sisi ni wababaishaji na vigeugeu,� alieleza.

Alieleza kuwa tatizo la madini katika nchi kutoinufaisha nchi yetu lipo katika sheria na wala siyo viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuongeza kuwa sheria hiyo ndiyo inayosababisha nchi hii kutonufaika na madini na kudai kuwa kuibadili ni jambo gumu kutokana na mikataba kufungwa toka zamani.

Alifahamisha kuwa katika kamati yao ambayo iliundwa na rais walikuwa wakipitia mikataba ya migodi yote ipatayo sita na kwamba katika hiyo mgodi uliokubali ni wa Barrick na wengine waligoma na kudai kuwa wataishitaki nchi yetu.

Masha alisema katika kamati yao walifanikiwa kuwashawishi baadhi ya wawekezaji na kisha kuufuta sheria hiyo kwa mgodi wa Barrick na kudai kuwa migodi hiyo pia ilikubali kulipa kodi na kwamba kamati iliyoundwa sasa ni muendelezo wa kamati yao ambayo ilivunjika baada ya rais kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

Alisema kwa sasa watu wamekuwa wakipiga kelele kutokana na hisia na siyo hali halisi, hivyo kuwataka wasomi wa chuo hicho kutopenda kuzungumzia mambo bila kufanya utafiti.
 
Waachwe waondoke na watutangaze kwamba sisi ni wababaishaji na sisi tutawatangaza kwamba wao ni WEZI siyo investors. Na dunia yote itakuwa nyuma yetu wakishajua details za mikataba hiyo with exception ya mafisadi, wala rushwa na waroho wa utajiri wa haraka haraka.
 
[COLOR="Blue" said:
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha amesema wawekezaji katika sekta ya madini nchini waligoma kubadilisha mikataba yao kwa madia ni makubaliano hali yaliyokuwa yamekwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini[/COLOR][/size]

Kwa kweli waende zao tu..watuachie madini yetu!! hatuwezi kuingia mikataba ya kijinga sababu kuogopa kuonekana sisi ni wababishaji. Mwal Nyerere aliliona hilo....Hawa akina Mkapa na Mwenzake Muungwana wanatupeleka ambako wajukuu wa watoto zetu watakuja kuchapa bakora makaburi yetu, kwa kuruhusu maliasili yetu kuporwa na wajinga wachache
 
...mnaongea tuu na hamko serious hapo ni blah blah tuu ambayo ndio hiyo hiyo ilitufanya tukasign mikataba hiyo hiyo ndio mnaileta hapa,badala ya kuwa wakweli mnataka kuleta masifa tuu yasiyo na maana...eti waondoke watuachie madini yetu? vipi na nyie mtawarudishia mabilioni yao waliyowekeza kwenye hiyo miradi au? kwa ufupi hatuna huo uwezo na hatuwezi labda kama tuko tayari kulipa price kubwa kuliko hayo madini na alichosema Masha ndio ukweli ambao JK alitakiwa aseme kutoka mwanzoni kuliko spin zake ambazo hazina maana...kumbukeni tuu kampuni maskni kama IPTL tena na mkataba wake wa rushwa walivyotushinda na tunaendelea kulipa mabilioni ndio iwe Barrick tena wamesign mkataba kwa sheria zetu wenyewe naona mntaka kurudishwa stone age na hao wazungu na ukizingatia 40% ya budget ni kwao
 
...mnaongea tuu na hamko serious hapo ni blah blah tuu ambayo ndio hiyo hiyo ilitufanya tukasign mikataba hiyo hiyo ndio mnaileta hapa,badala ya kuwa wakweli mnataka kuleta masifa tuu yasiyo na maana...eti waondoke watuachie madini yetu?

Koba nini kifanyike???? kwa kuwa makosa yameishafanyika tuache hivyo hivyo sababu 40% ya budget inatoka kwao? hii sikuelewi fafanua mazee
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom