Tanzania earning 1.9 in mines!

Hivi mnajua mgodi wa Barrick North mara tokea mwaka 2001 hadi oct 2006 walikuwa wamezalisha 1million Ounces za dhahabu ambazo kwa hesabu ya haraka ni sawa na USD 480million au Tshs 570Billion!!! Je ktk uzalishaji huu sisi watanzania tumepata faida gani!! zaidi ya kubaki na mashimo (pits) na uharibifu wa mazingira????
Hakika kwa mtindo huu hatuwezi kuendelea hata kidogo... hii nchi inahitaji marekebisho makubwa sana ktk siasa ili tuendelee!!!
 
hii nchi inahitaji marekebisho makubwa sana ktk siasa ili tuendelee!!!

Litakuwa ni tatizo la kisiasa sio? Oh, I have to join em politicians then! Halafu hiyo info umeleta inani-shock. Let me read btn the lines
 
Hivi mnajua mgodi wa Barrick North mara tokea mwaka 2001 hadi oct 2006 walikuwa wamezalisha 1million Ounces za dhahabu ambazo kwa hesabu ya haraka ni sawa na USD 480million au Tshs 570Billion!!! Je ktk uzalishaji huu sisi watanzania tumepata faida gani!! zaidi ya kubaki na mashimo (pits) na uharibifu wa mazingira????
Hakika kwa mtindo huu hatuwezi kuendelea hata kidogo... hii nchi inahitaji marekebisho makubwa sana ktk siasa ili tuendelee!!!
Waulize wafanya kazi wa Geita Gold mine wakati wa enzi za CEO Harry Michael.Watakuambia alisema nini kuhusu siasa za Tz!
Ni bahati walau tunapata hiyo 1.9% ilikuwa tuambulie mashimo tu
 
Waulize wafanya kazi wa Geita Gold mine wakati wa enzi za CEO Harry Michael.Watakuambia alisema nini kuhusu siasa za Tz! Ni bahati walau tunapata hiyo 1.9% ilikuwa tuambulie mashimo tu

Mzee unaposema tuambulie mashimo inabidi uwe makini, kuna baadhi ya watu ambao akaunti zao huko Uswisi zinatuna, kwa kuna baadhi wanaonufaika sana na wengi ndio tutaambulia mashimo.
 
Rev,

Kuna wengine wamesema 1.9% it is ok......................labda pengine siijui nchi yangu vizuri........lakini hiyo figure mmhhh...............yaani kweli tumekubali kupata 1.9% toka ktk madini yetu!!!

Tatizo hapa, mpaka sasa hakuna aliyesema 1.9% ni kiasi gani!!! statistics zozote usipokuwa makini nazo lazima utafsiri kila kitu kama unavyotaka....

Let be serious,,,, Uchumi wa Amerika haukui zaidi ya 3%, wa Tanzania unakuwa kwa 7%, wa Angola 20%,,, hauwezi kusema kwa kutumia hizo statistics hapo ati Tanzania au Angola ina uchumi Mkubwa...

mfano mwingine,,, Uchumi wa Kenya ukikua kwa 5%,,, ni mkubwa kuliko wa Tanzania ukikua kwa 8%....

So kwa sasa mnajadili hewa... poleni...

mfano wa mwisho:
A. 1.9% ya 1,000 = 19
B. 1.9% ya 1,000,000,000 = 19,000,000

Au ndio tatizo/kensa ya hisabati wandugu inaendelea kutumaliza?!!!!
 
Bado ni kiasi kidogo mno. Ukitilia maanani sasa hivi bei ya dhahabu ni $824 wakati katika mkataba bei inaonyesha ni $238. TUNAIBIWA MCHANA MCHANA!
 
Huhitaji rocket sayansi kujua kwamba kila shillingi mia moja wewe unaambulia shillingi moja na senti tisini.

Au kwa maneno mengine kila dola mia moja unaambulia dollar moja na senti tisini. kweli kama mtu haelewi hili aeleweshwe vipi?
 
Dua, Babu anataka Kusema,

Rais alisema madini yanachangia 1.9% ya Uchumi wa nchi, sijui ndio GDP au GNP,,,sasa naomba jibu 1.9% ya GDP ni kiasi gani? alafu tuanzie hapo, mpaka sasa hakuna... kwa hiyo mimi sijui ni kubwa au ndogo!

Mahesabu mnayoleta hapo huu, walahi kama ndio mahesabu yangukuwa yanafanywa hivyo, kusingekuwa na haja ya Certification za CPA, au Degree za Hesabu...
 
Kama ni 1.9 ya bilioni moja, au ni 1.9 ya trilioni moja hakuna tofauti. Tofauti hapo ni kuwa tumenyewa asilimia 1.9 ni sawa na bure, lakini najua kuwa wanaonufaika na mgodi huo(wenye akaunti zao huko Uswisi) bila shaka wana namna ya kuitetea.
 
Bado ni kiasi kidogo mno. Ukitilia maanani sasa hivi bei ya dhahabu ni $824 wakati katika mkataba bei inaonyesha ni $238. TUNAIBIWA MCHANA MCHANA!

Nilishawahi kusema mawazo mengi ya wataalamu wetu yako static,,, pale ambapo hutakiwi ku-fix bei wao wana-fix... sasa mambo yenyewe ndiyo hayoo!!! badaya ya kusema bei ya soko la dunia, wanasema x$... anyway again kensa ya Hisabati inatumaliza... too much vyuo vya sheria wakati hakuna uchumi wa kuwachukua hao wanasheria,,, we need more scientists
 
Huhitaji rocket sayansi kujua kwamba kila shillingi mia moja wewe unaambulia shillingi moja na senti tisini.

Au kwa maneno mengine kila dola mia moja unaambulia dollar moja na senti tisini. kweli kama mtu haelewi hili aeleweshwe vipi?

Dua nadhani wewe ndio umebeba mambo juu juu!!!... Rais amesema madini yanachangia pato la taifa kwa 1.9% kwa maana kilimo kinachangia takribani 30%... Viwanda 10-20%, then utalii sijui 10-18% sorry tarakimu hizo sio actuall...

Akasema tena, pamoja na kwamba madini yanachangia zaidi ya 50% ya FOREX lakini mchango wake kwa uchumi wa nchi bado ni mdogo hivyo tuangalie namna gani itachangia zaidi!!!

Sasa hii ni tofauti na wewe unavyotaka ku-represent hapo juu! Kumbuka kama kilimo kikishuka kwenye pato la taifa, na/au viwanda vikishusha uzalishaji, automatically madini yatapanda kwenye contribution yake katika pato la taifa hata kama uzalishaji utabaki pale pale... Okay!!!

Interpretation yake sio rahisi kama unavyotaka kusema,,, kama nilivyosema tukiwa wavivu tu, na viwanda vikashusha uzalishaji, madini yatapanda contribution kwenye mizania hata kama hakuna lolote...

Another thing; Ndio maana hata kwenye pato la foreign currency, wapinzani akiwepo Zitto walikuwa wakisema contribution ya 50% kwenye foreign curreny inayotoka na Madini sio jambo la kujivunia,,, inabidi kuwe na mizania,,, kwa maana sekta moja isiwe na kiwango kikubwa kwa sababu kukiwa na tatizo tu kwenye hiyo sekta nchi itayumba,,, mifano unayo ya SHABA ya Zambia, Karafuu ya Zanzibar etc...
 
Dua, Babu anataka Kusema,

Rais alisema madini yanachangia 1.9% ya Uchumi wa nchi, sijui ndio GDP au GNP,,,sasa naomba jibu 1.9% ya GDP ni kiasi gani? alafu tuanzie hapo, mpaka sasa hakuna... kwa hiyo mimi sijui ni kubwa au ndogo!

Mahesabu mnayoleta hapo huu, walahi kama ndio mahesabu yangukuwa yanafanywa hivyo, kusingekuwa na haja ya Certification za CPA, au Degree za Hesabu...

GDP ya Tanzania ni $21 580 000 000 kama hii website iko up to date. Kutokana na mikataba mibovu ya madini ambako tunaambulia 3% utaona mchango wake kwa GDP umekuwa mdogo kiasi hicho cha 1.9%. Kama tungekubaliana na makampuni haya ya madini na kuwa na angalau 50-50% joint venture machango wake ndio kweli ungeinua maisha ya walio wengi. Mifano iko mingi kuanzia Botswana, Angola na hata Nigeria wanaanza kubadili mikataba mibovu kutokana na sokomoko la Niger delta.

Tungekuwa waangalifu na kuwa na 50-50% mchango wake kwenye GDP ungekuwa 31.67%.
 
..whatever the case tumeliwa tuu hapo wajomba na mkataba tulisha sign,dawa ni kuwa punish waliotuingiza hapo kwa kuwanyima kura lakini at the end of the day hata Ditopile akigombea atashinda tuu...inakatisha tamaa sana!
 
Kilitime,

hakuna anayekataa hiyo fact unayoitetea....................suala linalotuumiza kichwa hapa ni kuwa je hiyo 1.9% ndio kweli uwe urithi wa madini yetu (Tanzania ni nchi ya 3 afrika nafikiri kwa utoaji Dhahabu pekee)........achilia mbali kuna almasi, tanzanite and the like....something is wrong with us............1.9%!!!.................hii sio figure ya kuifurahia au kuanza kutupa mifano ambayo ni nonsense (im sorry)

unapoanza kulinganisha kukua kwa uchumi wa nchi..........thats a different story.

The ishu is 1.9% madini kwa Pato la Taifa.................does it make sense to you!!....if it does then lets continue na majadiliano mengine......

wengine tupo hapa JF kuwaonyesha/kuwashtua viongozi wetu.......if there is something wrong...................in short mikataba ya madini haitusaidii chochote mbali ya kutuachia mashimo at the end of the day.
 
Dua, Babu anataka Kusema,

Rais alisema madini yanachangia 1.9% ya Uchumi wa nchi, sijui ndio GDP au GNP,,,sasa naomba jibu 1.9% ya GDP ni kiasi gani? alafu tuanzie hapo, mpaka sasa hakuna... kwa hiyo mimi sijui ni kubwa au ndogo!

Mahesabu mnayoleta hapo huu, walahi kama ndio mahesabu yangukuwa yanafanywa hivyo, kusingekuwa na haja ya Certification za CPA, au Degree za Hesabu...

Yeyote anayejua hesabu hahitaji kuwa Certfied Public Accountant (CPA) ili kujua 1.9% ni kitu kidogo sana. Huna mantiki yeyote katika kutetea hiyo 1.9% siku zote utabisha for the sake ya ubishi tu hata kama huna point ya kussuport your arguments!

Sasa hivi madini yanaingiza pesa nyingi Tanzania kuliko hata kilimo hasa ukitilia maanani ongezeko la bei ya dhahabu kufikia $824, hivyo kuendelea kuchangia 1.9% ya pato la Taifa ni kichekesho na aibu kubwa kwa nchi yetu.
 
Bajameni,

Mimi si mchumi, bali mbwabwajaji. Sasa if madini ambayo ni 1.9% ya GDP ya Taifa yanaingiza 50% ya forex, then something is wrong on this picture. It means kuwa hizo 98.1% ya GDP hazina nguvu za kutuleta japo 98.1% ya Forex?

Naomba mwenye proper break down ya exports zetu aiweke hapa, na zaidi hii GDP yetu ni kutokana na uzalishaji mali na mauzo bila "misaada"?

bado sielewi kwa nini Madini ambayo ni tosha kuchukua japo 30% ya GDP yawe ni kiwango kidogo hivyo.

If barrick can earn Billions of dollars, from Gold of tanzania, why are getting a mere hundred thousand or a million? does this make sense to anyone? Kwa nini Serikali isitumie zile pesa walizobwaga Meremeta, Tangold, Mwananchi na Deep Green wakaitumia Stamico kuwa at least 40% owners wa Uzalishaji madini ili tupate japo 40% ya earnings?

Kwani Ardhi na Watu si wetu? mtaji pesa na Mitambo ndio vya Barrick (60%)?
 
Rev.Kishoka,
majuzi Mohamed Dewji ameandika makala akutusihi Watanzania tusiilaumu serikali kutokana na mfumuko wa bei. Mohamed Dewji alielekeza kwamba mambo mengi yanayosababisha mfumuko wa bei yako nje ya uwezo wake.

sasa Dewji alieleza kwamba kupanda kwa bei ya mafuta ni sababu mojawapo. lingine akaeleza ni kupanda kwa "comodity prices." sasa wanaposema "comodity" wanazungumzia pamoja na mazao ya kilimo mfano ngano, mahindi etc etc.

sasa mimi nimefadhaishwa sana. kama bei za mazao ya kilimo zinapanda kwanini Watanzania wasifaidike na kupata nafuu.

Kama anayoyasema Mohamed Dewji ni ya kweli basi tuna tatizo kubwa sana. Hivi ni nani aliyeifikisha Tanzania hapa tulipo. Hawa viongozi wetu toka tupate uhuru wamekuwa wakifanya nini?
 
Angalieni mapato na faida ya Barrick inavyoongozeka toka mwaka 2004 hadi 2006 kutokana na ongezeko la bei ya dhahabu katika soko la dunia. Sisi kichwa cha mwendawazimu hatuambulii chochote.
http://www.barrick.com/Investors/InvestorFactSheet/default.aspx

...babu hawa jamaa wanalipa tax nyingi US kuliko kwetu wanapoitoa hiyo gold,kweli ng'ombe wa fukara hazai hata iweje,hivi tatizo letu ni nini hasa ? maana hata tulichopewa bure hakitusaidii,nina uhakika hata mafuta leo yakipatikana Tanzania nzima umaskini ni ule ule tuu
 
Net profit ya Barrick mwaka 2004 ilikuwa $248,000,000 mwaka 2005 iliongezeka na kufikia $401,000,000 mwaka jana ilizidi kuongezeka na kufikia $1,506,000,000. Je, Tanzania katika ongezeko la bei ya dhahabu katika soko la dunia ambayo imeongeza faida ya kampuni hiyo mara 7 katika mwaka 2006 ukilinganisha na 2004, imeambulia nini!?-ZERO! unatamani kulia lakini ndio ukweli wa mambo! Wenye mali hatufaidiki na dhahabu yetu lakini 'wachukuaji' alias 'wawekezaji' na shareholders wao ndio wanaofaidika na dhahabu yetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom