Kuna haja Dua ziongozwe na Kasisi mmoja kuwakilisha Wakristo na Imam mmoja kuwakilisha Waislam wakisha maliza wanatoka nje ya Bunge na wabunge kuendelea na kazi yao. Hii itawafanya wawe na adabu kuheshimu uwepo wa Mwenyezi Mungu hapo Bungeni.
Nasema watashika adabu kwa sababu sasa hivi hakuna hiyo kitu kwani huyu anayejifanya kuongoza dua jana alikuwa nje ya maadili leo wanamuona akiongoza dua ndani ya bunge hawawezi kutilia maanani uzito wa dua na kikao cha bunge lenyewe, tufanye mabadiliko hayo ili kutenganisha dini na siasa kwa vitendo.
Nimeiona hii kwenye gazeti la Mwanachi la leo linalohusu 'Dua ya kuombea Bunge inayosomwa kama kasuku.
Dua hii inasema kama hivi:
Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu,Muumba wa Mbingu na Dunia,umeweka katika dunia Serikali za Wanadamu na Mabunge ya Mataifa ili haki ya itendeke.Twakuomba uibariki nchi yetu idumishe uhuru,umoja.haki na amani,umjalie rais wetu hekima,afya njema,na maisha marefu ili pamoja na wanaomshauri,wadumishe utawala bora.Utuongezee hekima na busara sisi wabunge wa Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utupe uwezo wa jujadili kwa dhati mambo yatakayoletwa mbele yetu leo,ili tufanye maamuzi sahihi yenye manufaa kwa watu wote na utsawi wa nchi yetu.Amina"
Kwenye sala/dua hii ni nzuri siwezi kukataa wala kupinga,lakini nina maswali kadhaa kuhusu hili:
1.Je Bunge letu linaitendea haki sala au dua hii.
2.Kwanini dua hii isisomwe na wabunge wote ili kila mmoja aweze kuifanyia tafakuri ya kina pale anapoomba au kusali dua/sala hii asubuhi wafunguapo Bunge.
3.Na kwanini sala/dua hii husomwa kwa haraka sana kama vile kuna muda unapotea,yaani kwanini dua hii sifanywe kwa tafakuri ya kina pale inaposaliwa?
Inawezekana hoja hii ilishawahi kuletwa hapa na sikuiona basi naomba mnisamehe,ila ningependa tuitafakari dua hii na kuiomba serikali yetu au Bunge letu liichulie DUA hii kwa moyo na kila mtu ndani ya Bunge awe anaisoma na kuitafakari,ninadhani itabadilisha dhana nzima ya uchangiaji usiona tija,uchangiaji wa mipasho na matusi kwa wabunge wa pande zote mbili.
Karibuni nyote tuijadili.
Hapo ushatoa jibu sio swali tena mdau.Hizo dua wanazoanza nazo ipo siku sitawarudia wao wapige meza wee tutajua mwisho wao tuu.kuna uhusiano wowote wa dua ktk kuombea bunge la katiba na yale matendo ambayo yanafanywa na wajumbewa katiba hasa ukizingatia manung'uniko mengi yamekuwa yakitolewa na wananch juu ya uwezekano wa baadh ya wajumbe kuchakachua katiba ambayo kiukweli ni maoni ya wananchi wa jamhuri ya muungano wa tz.je kunaweza kukawa na athari kubwa kwa maana kwamba ni kumdhihaki mwenyezi mungu?
Mungu hana upendeleo kwa mtu yeyote na pia Mwenyezi Mungu hachoki kusamehe dhambi zetu ndio maana hamna mtu mkamilifu hapa duniani, kama dhambi kila moja ana dhambi.
dua ni nzuri ila anaeisoma dua hiyo si mtu mwemakuna uhusiano wowote wa dua ktk kuombea bunge la katiba na yale matendo ambayo yanafanywa na wajumbewa katiba hasa ukizingatia manung'uniko mengi yamekuwa yakitolewa na wananch juu ya uwezekano wa baadh ya wajumbe kuchakachua katiba ambayo kiukweli ni maoni ya wananchi wa jamhuri ya muungano wa tz.je kunaweza kukawa na athari kubwa kwa maana kwamba ni kumdhihaki mwenyezi mungu?
kuna uhusiano wowote wa dua ktk kuombea bunge la katiba na yale matendo ambayo yanafanywa na wajumbewa katiba hasa ukizingatia manung'uniko mengi yamekuwa yakitolewa na wananch juu ya uwezekano wa baadh ya wajumbe kuchakachua katiba ambayo kiukweli ni maoni ya wananchi wa jamhuri ya muungano wa tz.je kunaweza kukawa na athari kubwa kwa maana kwamba ni kumdhihaki mwenyezi mungu?