Tanzania Daima mnajua athari kwa UKAWA kwa mlichokiandika kuhusu Mtatiro?

Huey freeman

JF-Expert Member
Sep 20, 2013
593
247
"SABABU ZA MTATIRO KUNG'OKA CUF" -

Sababu za Mtatiro kung'oka CUFSIRI ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba kufanya mabadiliko kwenye kurugenzi zake kwa kumng'oa Julius Mtatiro kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, imefichuka.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya chama hicho, vinadai kuwa sababu ya kwanza imetokana na viongozi wakuu wa chama hicho taifa kumtaka Mtatiro asigombee nafasi yoyote.

Inaelezwa kwamba Mtatiro aliandaliwa kisaikolojia kwamba hatarudi kwenye nafasi yake kwa madai ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Sababu ya pili ambayo inatajwa na baadhi ya viongozi wa CUF ni kwamba kiongozi huyo kijana, anadaiwa kujihusisha na matumizi mabaya ya fedha hasa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga.

Kwa mujibu wa habari hizo, sababu ya tatu inaelezwa kuwa Mtatiro alikuwa akifanya siasa za kitoto (siasa nyepesi), zilizokuwa zinawakera baadhi ya viongozi wa juu wa CUF.

"Mtatiro sio kama amependa mwenyewe kuacha nafasi hiyo la hasha, ukweli ni kwamba aliandaliwa kisaikolojia kuwa nafasi hiyo hatoshi na inamlazimu atoke ampishe Sakaya ambaye anaweza akasukuma gurudumu hilo la chama," kilieleza chanzo cha habari hizo.

CUF imefanya mkutano mkuu na kuwachagua wajumbe wapya wa Baraza Kuu pamoja na kurugenzi.

Katika mabadiliko hayo, nafasi ya Mtatiro inachukuliwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya.

Nafasi ya Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, imeshikiliwa na Joran Bashange, Mkurugenzi wa Haki na Binadamu na Sheria imeshikiliwa na Mbunge wa Viti Maalumu Rufiji, Rukia Mchuchuli huku nafasi ya Kurugenzi ya Mipango na Uchaguzi imeenda kwa Shaweji Mketo.

Wapinga mabadiliko

Baada ya kufanya mabadiliko hayo, baadhi ya wanachama wamejitokeza kupinga uteuzi huo na leo wanatarajia kufanya maandamano ya amani kwa lengo la kuonana na kuzungumza na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba kueleza sababu za kutoridhishwa na baadhi ya viongozi.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Ibrahimu Nanga, ambaye ni mmoja wa wanachama wanaopinga uteuzi wa baadhi ya viongozi, alisema watakwenda kuwataka viongozi kuwapa fursa ya kueleza dukuduku lao.

"Lengo si maandamano bali ni kutaka kukutaka na mwenyekiti. Tunapinga uteuzi wa Shaweji Mketo na wengine waliorejeshwa wakati kipindi kilichopita hawakukisaidia chama," alisema Nanga.

Chanzo: Tanzania Daima
_____________________________________________

MTATIRO KASEMA HAYA.

Hii habari imenishangaza sana.Tanzania Daima nalo limegeuka kuwa gazeti la kuandika habari za kubahatisha namna hii kwani hamna vyanzo vya habari sahihi?

Nilitegemea UHURU ndio wahangaike kuandika habari zisizo na kichwa wala miguu.Tusubiri tena kesho watakuja sijui na sababu zipi.

KUPUMZIKA KWANGU WADHIFA WA JUU NDANI YA CUF KUMEGEUZWA KUWA DEAL.

Nigawieni basi MGAO wangu mkishauza magazeti kwa habari za Uzushi!

TANZANIA DAIMA MMLIKI WAKE NI FREEMAN MBOWE MMOJA WA VIONGOZI WA UKAWA. INATOA HABARI ZA UCHONGANISHI KATI YA KATIBU MKUU UKAWA NA CHAMA KINACHOUNDA UKAWA.


JE CCM WATAACHA KUTUSHINDA WKT TUKO CARELES HIVI.
 
Sasa UKAWA hapo itaingia vipi? Japo sioni mantiki ya habari kama ambavyo sioni mantiki ya sensational headline yako ........
 
Tanzania Daima huwa linatoka kila wiki kama UWAZI la Shigongo ama kila siku ?
 
Polepole ndiyo mwendo mengi sana yatajitokeza cuf wameliwa wameingizwa mkenge na hawa ukawa halafu watapotelea humohumo.
 
Kwani nyie mnadhani tanzania daima nalo gazeti la maana lakini mtatiro kweli alikuwa anafanya siasa za kitoto sana hana mipango ya kisiasa kabisa.
 
"SABABU ZA MTATIRO KUNG’OKA CUF" - Hii
nimeinasa Tanzania Daima…………Inasema;
SIRI ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi
(CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba kufanya
mabadiliko kwenye kurugenzi zake kwa
kumng’oa Julius Mtatiro kwenye nafasi ya
Naibu Katibu Mkuu Bara, imefichuka.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya chama
hicho, vinadai kuwa sababu ya kwanza
imetokana na viongozi wakuu wa chama
hicho taifa kumtaka Mtatiro asigombee nafasi
yoyote.
Inaelezwa kwamba Mtatiro aliandaliwa
kisaikolojia kwamba hatarudi kwenye nafasi
yake kwa madai ya kutoridhishwa na utendaji
wake.
Sababu ya pili ambayo inatajwa na baadhi ya
viongozi wa CUF ni kwamba kiongozi huyo
kijana, anadaiwa kujihusisha na matumizi
mabaya ya fedha hasa wakati wa kampeni za
uchaguzi mdogo wa Igunga.
Kwa mujibu wa habari hizo, sababu ya tatu
inaelezwa kuwa Mtatiro alikuwa akifanya
siasa za kitoto (siasa nyepesi), zilizokuwa
zinawakera baadhi ya viongozi wa juu wa
CUF.
“Mtatiro sio kama amependa mwenyewe
kuacha nafasi hiyo la hasha, ukweli ni
kwamba aliandaliwa kisaikolojia kuwa nafasi
hiyo hatoshi na inamlazimu atoke ampishe
Sakaya ambaye anaweza akasukuma
gurudumu hilo la chama,” kilieleza chanzo
cha habari hizo.
_____________________________________________
_________
MTATIRO KASEMA HAYA.
Hii habari imenishangaza sana….Tanzania
Daima nalo limegeuka kuwa gazeti la
kuandika habari za kubahatisha namna hii…
kwani hamna vyanzo vya habari sahihi????
nilitegemea UHURU ndo wahangaike kuandika
habari zisizo na kichwa wala miguu
….tusubiri tena kesho watakuja sijui na
sababu zipi. KUPUMZIKA KWANGU WADHIFA
WA JUU NDANI YA CUF KUMEGEUZWA KUWA
DEAL…..Nigawieni basi MGAO wangu
mkishauza magazeti kwa habari za Uzushi!!!!!

TANZANIA DAIMA MMLIKI WAKE NI FREEMAN MBOWE MMOJA WA VIONGOZI WA UKAWA. INATOA HABARI ZA UCHONGANISHI KATI YA KATIBU MKUU UKAWA NA CHAMA KINACHOUNDA UKAWA.

JE CCM WATAACHA KUTUSHINDA WKT TUKO CARELES HIVI.

Siasa za maji machafu
 
Mi Naona Mtatiro Palikuwa Hapamtoshi Pale, Siasa Hajui Vzr Ni Kama Nape
 
Ukimuona mtu amenunua Tanzania Daima kwa madai anatafuta issue muhimu ujui maisha yamemuendea kombo, anatafuta kisingizio cha ugumu wa maisha yake.
Fanya kazi wenzio wanapiga hela oooh!
 
Lakn Tz Daima Wamekosea Kuripot Hivo, Wangeandika Sababu Za Mbowe Kugombea Tena Uenyekiti Chadema
 
Ukimuona mtu amenunua Tanzania Daima kwa madai anatafuta issue muhimu ujui maisha yamemuendea kombo, anatafuta kisingizio cha ugumu wa maisha yake.
Fanya kazi wenzio wanapiga hela oooh!
Hivi Tanzania Daima ni gazeti la kusomwa na watu wenye akili? Mie najua linaandaliwa kwa ajili ya misukule na watu wanaosubiri kupelekwa Mirembe!
 
Lakn Tz Daima Wamekosea Kuripot Hivo, Wangeandika Sababu Za Mbowe Kugombea Tena Uenyekiti Chadema
Si sababu za Mbowe kugombea tena uenyekiti wa CHADEMA bali sababu za Mbowe kutumia fedha nyingi za umma kwenda kufanya uzinifu huko Dubai
 
Ukimuona mtu amenunua Tanzania Daima kwa madai anatafuta issue muhimu ujui maisha yamemuendea kombo, anatafuta kisingizio cha ugumu wa maisha yake.
Fanya kazi wenzio wanapiga hela oooh!

Ni Kama Ilivyo Uhuru, Yakijinga Sana
 
Si sababu za Mbowe kugombea tena uenyekiti wa CHADEMA bali sababu za Mbowe kutumia fedha nyingi za umma kwenda kufanya uzinifu huko Dubai

Kweli bwana! Safari za msingi ni kama hizi ambazo hata wenyeji hawana habari na ujio wako
ImageUploadedByJamiiForums1404207281.245257.jpg


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Back
Top Bottom