Tanzania Daima lauzwa kama njugu siku hizi

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Wadau, kwa taarifa tu, leo asubuhi kutokana na udhuru nyumbani nilichelewa kwenda kazini hadi saa 6 hivi mchana. Nilipotoka nikakumbuka magazeti, nikasema nitanunua Kariakoo. Nilishangaa sana kuanzia Congo Street hadi Mnazi MMoja gazeti la Tanzania Daima sikulipata, kila muuzaji asema ameishiwa.

Hatimaye nilikuja kulipata Jamhuri Street karibu na NBC. Wauzaji waliniambia siku hizi gazeti hilo huisha mapema sana na baadhi yao wanashangaa kwa nini wamiliki hawachapishi nakala nyingi.
 
inawezekana zinatolewa kopi chache kwa siku hivyo zinaisha fasta...........
 
Mkuu Nyunyu inawezekana umehit penyewe kabisaa, mwaka huu chama cha majizi na mafisadi watatumia kila njia na gharama yoyote ile ujumbe usifike kwa walengwa na kupotosha ukweli. Lakini yana mwisho haya, iko siku! Wananchi watasema hatudanganyiki!
 
Mkuu Nyunyu inawezekana umehit penyewe kabisaa, mwaka huu chama cha majizi na mafisadi watatumia kila njia na gharama yoyote ile ujumbe usifike kwa walengwa na kupotosha ukweli. Lakini yana mwisho haya, iko siku! Wananchi watasema hatudanganyiki!

Wakuu haya ndo mambo inabidi CHADEMA wafikirie sana. Pamoja na ilani nzuri pia kuna hizi hila za hili monster. It can even eliminate the threat to its way. Please they should think of all huge and minor tactics.

CCM ni balaa wewe...
 
:mad2:Hata mi nahisi hao vichaa hununua nakala nyingi na kuzichoma ili zisiwafikie wadau. Mwisho wao upo.
 
Dawa ni redio. CHADEMA ina redio station inayowaunga mkono? Kama haina itabidi iwe inanua time sana kwenye redio.
 
Hivi mnakumbuka Mwalimu Nyerere alivyotoa kitabu kilichomchambua Malecela naMarehemu Kolimba kuwa kitabu hicho hakikuonekana mitani kwani watu wa kazi walikinunua na kukichoma moto ili kisiwafikie wengi? Basi ndiyo kinachofanyika kwa Tanzania Daima na mwana halisi. Mafisadi wako kazini masaa 24, si hata hapa JF wapo na wanahaha kama mbwa mwitu.
 
NI kweli hili gazeti sasa hivi ni adimu sana. Sehemu nyingi utasikia limeisha. Lakini habari njema ni kwamba: watu wengi wanalipenda. Nikiwa kwenye basi la Abood Moro-Dar (frequent traveller), hili gazeti huonekana kwa wasomaji wengi, kama inavyokuwa kwa gazeti la Mwananchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom