- Thread starter
- #21
hueleweki mkuu. Kinachofanya aonekane msaliti ni kuchapishwa kwa picha hiyo au ni yeye kucheka na mh rais? Maana picha au gazeti linareport event tu!
Lakini kubwa ni kwa nini unaamini si sawa kwa zitto kuongea na kucheka na rais. Tuliona karibu viongozi wote wa cdm walipoenda pale magogoni na kupewa chai wote walionesha tabasabu/kufurahi tu. Sasa hili la zitto ni kwa nini lionekane kuwa ni tatizo? Na kwa gazeti kuchapisha picha hiyo ni kwa nini unaona vibaya...mimi naona kama vile inamjenga zitto kisiasa kwa sababu inaonesha anavyokubalika hata na wapinzani wake (ccm).
Kama utakumbuka hili la kukubalika na wapinzani liliwapa taabu sana washabiki wa jk pale ilipokuwa inaonekana kama vile dr slaa hamkubali, anamkwepa etc. Ilivyotokea mwanya wa dr slaa na jk kukutana sote tunajua picha hizo zilivyopewa umuhimu hata na magazeti ya ccm au pro ccm. Well hili la zitto pengine lipo tofauti kidogo lakini kimsingi sioni tatizo kwa picha hizo kuchapishwa gazeting kama kweli hiyo event ilitokea.
Kama unadhani kuna hoja/agenda nyingine labda utuambie.
maneno yaliotumika tu mkuu