Tanzania Daima: Kama CHADEMA ni Wachagga, CCM ya Waislamu?

CCM ni chama cha Kitaifa na kimataifa..kisera na hata kiuongozi (mpangilio nk)

Chadema ni chama cha kidini (ukristo) na kichagga kisera na hata kiuongozi (mpangilio nk)

Utaratibu wa kupata viongozi wa juu unaratibiwa na kanisa..kwahiyo waislamu watawekwawekwa tena wachumia tumbo e.g. Prof. Safari, Yule makamu wa darasa saba (kama vile wamekosa educated muslims) wanafanya kiini macho....

Chadema ki-utaratibu kinahakikisha maslahi ya kifedha yanafaidisha wachaga..tafuta watunza fedha na watumiaji fedha wengi wanatokea huko..wengine mtachujwa na kuzushiwa kashfa mpaka muondoke...

Waislamu wenye uwezo wamebinywa kwa maelekezo ya kanisa katoliki (hidden) mfano Zitto will go no where??, jambo hili linaratibiwa katika jumuia za kanisa katoliki mitaani....

Wanaweza kujivua gamba wakidhamiria kweli..lakini wanakoelekea wataimba sana kupata nchi kwakuwa ni wabaguzi wengi wa washabiki wao ni "christian fundamentlist"

Nembo ya chama ni msalaba (mistari meusi) wakipata nchi wanakamisha...

wamejificha lakini wanaonekana wazi kwa tabia, nyendo zao...
Una story nzuri kwa wajukuu.
 
Duka analouza mpemba(sijasema CUF) hukosi gazeti la AN-NUUR, na duka analouza mchaga hukosi gazeti la tanzania Daima(sijasemaCHADEMA)
 
You have said it all MKJJ wakubali wasikubali hiyo si kazi yako check this para........big up MKJJ.
Katika suala la uhuru wa maoni kuna kanuni moja ambayo pale Marekani huwa wanaitumia sana kuzuia maoni yenye kuhatarisha usalama wa watu. Kwamba "huwezi kupiga kelele za 'Moto Moto' kwenye ukumbi uliojaa watu" wakati hakuna moto wowote na ukiulizwa useme ati "nilikuwa natumia haki yangu ya maoni". Wale wanaotuambia "ukabila ukabila, udini na udini" kama hawamaanishi hicho na kama hakuna ushahidi wanachezea mchezo wa "moto moto".
 
Duka analouza mpemba(sijasema CUF) hukosi gazeti la AN-NUUR, na duka analouza mchaga hukosi gazeti la tanzania Daima(sijasemaCHADEMA)

Ah! Wapi huko magazeti yanauzwa madukani? Tanzania Daima hata uongozi wake simwoni Mchagga. Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo mhariri mtendaji na naibu wote sio Wachagga! Jamaa wanaandika kwa uhuru ambao magazeti mengi hayana.
 
Ah! Wapi huko magazeti yanauzwa madukani? Tanzania Daima hata uongozi wake simwoni Mchagga. Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo mhariri mtendaji na naibu wote sio Wachagga! Jamaa wanaandika kwa uhuru ambao magazeti mengi hayana.

Sasa kinachokuliza nini?Maana unalalamika sana.
 
Mkuu MMJ
binafsi nashukuru kwa hili darasa la leo.
Nimesoma notes nikaelewa.
Kwa Mtanzania yeyote atakayepitia hii shule na kubakia kichwa ngumu atakuwa amelaaniwa!
 
M.M Mwanakijiji kachemka vibaya na hiyo hoja yake regerege, uwezi kafananisha Dini na kabila, Uislam ni zaidi ya uchaga, sababu kasema Rais wa Jf inaonekana hoja ya msingi, Mwanakijiji vipi Waislam ambao wapo Chadema unawaweka wapi?

Vipi Wakistro waliopo CCM unawaweka wapi?
 
Kama CHADEMA ni Wachagga, CCM ya Waislamu?
ban.kijiji.jpg


M. M. Mwanakijiji

amka2.gif

NIVUNJE mwiko, nisivunje? Nimeamua kujitolea kuvunja mwiko hata kama hamtaki nivunje.
CHADEMA ni chama cha Wachagga na CCM ni chama cha Waislamu. Huwezi kukubali moja ya hilo na ukakataa jingine. Vigezo vinavyotumiwa na baadhi ya watu kuitaja CHADEMA kuwa ni chama cha Wachagga tukivikubali bila kutumia uwezo tuliojaliwa na Mwenyezi Mungu kuvihoji basi vinatusukuma kama mkokoteni ulioachiliwa kwenye mteremko na shehena ya madafu kufikia hitimisho kuwa CCM nayo yaweza kabisa kutajwa kuwa ni chama cha Waislamu.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilipoanzishwa viongozi wake wengi wa awali walikuwa ni Wachagga. Na hata leo baadhi ya viongozi wake wengi ni Wachagga hata wale waliostaafu.
Kutokana na historia hii baadhi ya watu (hasa wana Chama Cha Mapinduzi na wapinzani wengine) wamekitaja CHADEMA kuwa ni Chama “Cha Wachagga”. Na ni kutokana na hilo wamehitimisha pasipo kuonyesha uwezo wa kutumia mantiki kuwa CHADEMA ni chama cha kikabila. Kama kuna Wachagga wengi – wanasema, basi kuna ukabila.
Baadhi ya viongozi wa kwanza wa Chama hicho ni pamoja na mzee Edwin Mtei, Freeman Mbowe, na Philemon Ndesamburo.
Hawa watatu licha ya kuwa ni viongozi maarufu vile vile ni wafanyabiashara wakubwa nchini. Kwa vile uanzishwaji wa CHADEMA unahusishwa moja kwa moja na Edwin Mtei mtu wa Kilimanjaro na chama hicho kikavutia watu wengi wakiwemo baadhi ya hao wafanyabiashara basi kimekuwa kikitajwa tangu mwanzo kuwa ni chama cha Wachagga.
Hivyo tunaweza kuona kwa urahisi kabisa kuwa tuhuma za Uchagga wa CHADEMA zinatokana na mambo makubwa matatu: uasisi wake, uongozi wake na nafasi za wanachama wake maarufu wanatoka maeneo gani ya nchi. Tukumbuke kuwa kinachoangaliwa katika “ukabila” huu ni kile kinachoonekana ni “wingi” au idadi ya Wachagga ndani ya CHADEMA na nafasi zao kubwa za kisiasa.
Chama Cha Mapinduzi kilipoasisiwa (wakati huo kikiitwa TANU na ASP) viongozi wake wengi walikuwa ni Waislamu. Hili siyo siri. Kwa upande wa TANU viongozi waanzilishi wake kabla hata Mwalimu Nyerere hajahamia Jijini Dar na kuanza shughuli za kisiasa rasmi walikuwa ni Waislamu maarufu wa Jiji la Dar ambao majina yao yalikuwa yakijulikana wakati huo.
Miongoni mwao tunaowakumbuka leo hii ni familia ya Sykes (maarufu kati yao akiwa ni Abdulwahid Sykes na kaka zake Ali na Abbas), masheikh maarufu wa Jiji la Dar es Salaam kama kina Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Chaurembo na mzungumzaji maarufu, Sheikh Suleiman Takadir.
Kwa madhumuni ya hoja yangu siwahesabu Wakristu kama John Rupia, Vedasto Kyaruzi au Stephen Mhando ambao nao ni waasisi wa TANU kama vile ambavyo sitawahesabu watu wengine ambao hawakuwa Wachagga lakini walishiriki katika uasisi wa CHADEMA kama kina mzee Brown Ngwilulupi, Jacob Nkomola na Bob Makani. Tukiwaingiza hao wengine hoja yetu haitanoga.
Ni Waislamu hata hivyo waliokuwa na nguvu zaidi ndani ya TANU kutokana na nafasi zao na uwezo wao wa kifedha katika Jiji la Dar. Walitumia mali na nafasi zao kuweza kukijenga chama na wengine walitoa hata nyumba zao kwa ajili ya matumizi ya TANU.
Kitabu cha Mohammed Said cha Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968): Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati Za Waislam Dhidi Ya Ukoloni Wa Waingereza Katika Tanganyika kinaelezea kwa kina jinsi Waislamu walivyokuwa na nafasi ya pekee katika kuanzishwa kwa TANU kiasi kwamba sehemu mojawapo Said anatangaza pasipo shaka wala kujiuma meno kuwa “Kimsingi Chama cha TANU kilikuwa ni chama cha Waislamu”.
Lakini siyo kutokana na uasisi wake tu ndio maana TANU ilikuwa ni chama cha Waislamu bali pia eneo lake ambapo kilikuwa na nguvu sana. Kama CHADEMA kuwa na nguvu kwa muda mrefu mikoa ya Kaskazini kutokana na kukubalika zaidi maeneo hayo TANU nayo ilikuwa na nguvu sana katika maeneo ya Pwani na maeneo ambayo yalikuwa na Waislamu wengi kama Tabora, Tanga na Dar yenyewe.
Hivyo, kilikuwa ni chama cha Waislamu siyo kutokana na uasisi wake tu bali pia kutokana na maeneo yake ambayo kilikuwa kimekubalika zaidi kwani hata katika maeneo hayo mengine ni viongozi wengi wa Kiislamu waliokuwa wakijitokeza kukiunga mkono.
Vile vile CCM baada ya kuundwa kufuatia kuunganishwa kwa ASP na TANU kilijikuta kimepokea viongozi wengi ambao ni Waislamu kutoka Zanzibar na matokeo yake hadi leo hii ni rahisi kuona kuwa Kamati Kuu inachukua wajumbe wengi kutoka Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya CCM kitu ambacho kinasababisha chama hicho kuwa na Waislamu wengi kwenye Kamati Kuu kutoka na wingi wa Waislamu wanaotoka Zanzibar.
Hivyo basi tunalazimika kufikia mahitimisho yafuatayo tunapoviangalia vyama hivi viwili:
CHADEMA ni chama cha Wachagga kwa sababu:
  • Kiliasisiwa na Wachagga wakiwa na nafasi za pekee.
  • Kilikubalika zaidi katika maeneo ya Kilimanjaro na Kaskazini (Moshi mjini na maeneo mengine).
  • Viongozi wake wameendelea kuwepo kuwa ni Wachagga.
Kama Uchagga ni haya mambo matatu na watu wenye akili timamu wanakubali kuwa ni haya yanayofanya chama hicho kuwa cha “Kichagga” au cha “kikabila” basi ni kweli CHADEMA ni chama cha Wachagga na ni chama cha kikabila.
CCM ni chama cha Waislamu kwa sababu:
  • Kiliasisiwa na Waislamu wakiwa na nafasi za pekee (Baraza la Wazee la TANU ilipoundwa liliundwa na Waislamu watupu).
  • Kilikubalika kwenye maeneo yenye Waislamu wengi
  • Viongozi wake wengi wameendelea kuwa ni Waislamu.
Hivyo basi tunaweza kuona kitu kingine cha pekee ambacho kimefichika na huwa tunadokezwa nacho katika hizi tuhuma. Wachagga wengi ni Wakristu! Hivyo, kwa namna moja au nyingine tunaona kuwa tuhuma za “CHADEMA ni chama cha Wakristu” zinatokana na hilo vile vile na hivyo wale ambao wanakishambulia kuwa ni Chama cha Wakristu hufanya hivyo kwa sababu ile ile kwamba ni chama cha Wachagga.
Matokeo yake tunalazimishwa kuiangalia CHADEMA aidha ni kama chama cha Wakristu au chama cha Wachagga kwa sababu mantiki inayopendekezwa mbele zetu haitupi uchaguzi mwingine wowote.
Na tukifuata mlolongo huo huo wa mantiki tunajikuta tunaangalia CCM vile vile kama chama cha Waislamu na ukishaliona hili utaelewa ni kwanini baadhi ya Waislamu ambao walikuwa na tatizo na CCM miaka kadhaa huko nyuma leo hawana tatizo nayo kwa sababu wanaona kuwa kinaongozwa na “Waislamu”. Na matokeo yake utaona kundi la Waislamu hawa hawawezi kuona kosa au tatizo lolote lile la serikali kwani kwa kufanya hivyo itabidi wakubali matatizo ya “Muislamu” mwenzao au “Waislamu wenzao”.
Ndugu zangu, hapa ndipo tulipofikishwa na watawala wetu walioshindwa; hapa ndipo tulipopigishwa magoti na kuambiwa tuabudu; naam, hapa ndipo tunalazimishwa kuangalia na kuangaliana kwa misingi ya dini na kabila.
Na wapo baadhi ya watu kati yetu ambao wanaangalia Tanzania kwa misingi hiyo. Viongozi wengine, wakuu wa taasisi za umma ambao wakiona jina la Kichagga wanafikiria ni jinsi gani hawatompa mtu huyo nafasi.
Kuna mifano ambayo siku moja ikiitwa wazi tutaona haya kwani baadhi ya watu wanaotukuzwa kwa “uongozi bora wa mashirika ya umma” ni wabaguzi wa kikabila waliokubuhu ambao wanastahili tuzo mbovu ya ufisadi wa kidini!
Naam, wapo na wengine wanaochukulia hali iliyopo sasa na kuamini kabisa kuwa tatizo ni kikundi cha Waislamu na hivyo nao wanapoona jina la Muislamu wanaanza kufikiria wafanye nini naye au watumie mbinu gani kutokumtendea haki kwa sababu tu ni Mwislamu.
Ndugu zangu, chuki ya kidini na kikabila ambayo inaenezwa na watawala walioko madarakani ni lazima ikataliwe na kila Mtanzania ambaye anakumbuka tunu za taifa letu.
Chuki hizi zinapandikizwa kiujanja na wanasiasa walioshindwa hoja na hupepewa kama cherezi cha ubani na harufu yake mbovu hukumbatiwa na watu ambao hawataki kufikiri kwa kutumia chembe za ubongo walizojaliwa na Muumbaji wao.
Leo hii tunawasikia wanasiasa wakubwa wa CCM wakizungumza bila haya wala kupepesa macho kuwa “CHADEMA ni cha Wachagga” na chama chao hata kuwakemewa hakithubutu na wanasiasa wapo ambao hueneza sumu hii ili kuwatisha Watanzania wengine. Kinachoniudhi mimi zaidi ni kuwa serikali ya CCM ndio imeshika madaraka na ndiyo inatakiwa kusimamia sheria zetu.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo Rais Kikwete, Rashid Othman, Waziri Mkuu Pinda, IGP, DPP, Mwanasheria Mkuu, majaji na viongozi wote wa kisiasa nchini wameapa kuilinda inasema hivi katika Ibara ya 20:2(a) kuwa hakuna chama chochote cha kisiasa (au kikundi) nchini ambacho kitaandikishwa chenye misingi au malengo ya “kukuza na kupigania” i. (i) imani au kundi lolote la dini; (ii) kundi lolote la kikabila pahala watu watokeapo, rangi au jinsia.
Kama kweli watawala wetu ambao wanapigiwa saluti na kuhutubia kwa mbwembwe kuwa “Tanzania ni nchi ya utawala wa sheria” wanaamini kuwa walikula kiapo hatuna budi kuwauliza imekuwaje kuwe na Chama cha Wachagga ambacho kimeruhusiwa kushiriki uchaguzi na kushinda vizuri na kupata wabunge na madiwani wengi na kumsimamisha mgombea wa Urais ambaye alilindwa na vyombo vya dola wakati chama hicho ni cha kidini na cha kikabila?
Swali hili wanahitaji kuulizwa watetezi wa CCM na wapiga panda wake ambao hukesha kutuambia kuwa CHADEMA ni chama cha kikabila na kidini wamechukua hatua gani kukifuta chama hicho?
Nakumbuka Tendwa alitishia kuifuta CHADEMA si kwa sababu ya ukabila au udini wake bali kwa sababu ilikuwa imeing’ang’ania CCM kwa kuhoji matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Tunajiuliza huyu Tendwa kwanini hajawahi kusimama na kuliambia taifa kuwa CHADEMA ni kweli chama cha Wachagga na kinavunja sheria na Katiba na hivyo kinafutwa?
Kwanini hatujawaona wale wenye kuamini kuwa CHADEMA ni chama cha Wakristu na Wachagga hajawasimama na kuandamana kutaka sheria ifuate mkondo ili chama hicho kifutwe mara moja na mimi nitawaunga mkono!
Jibu pekee ambalo tutapatiwa ni kuwa “kauli hizo zinatolewa na wanasiasa”. Kwamba maneno ya kada mmoja wa CCM kuwa asingeweza kujiunga na CHADEMA kama ilivyodaiwa kwa sababu ni “Chama cha Wachagga” ni ya kisiasa na hayana uzito wowote.
Kwamba sumu inayoenezwa kwenye vyombo vya habari na radio maarufu nchini na kwenye hotuba mbalimbali za viongozi kadhaa kidini na kisiasa ni “uhuru wa maoni” basi tunalazimika kuhoji uwezo wa watawala wetu kuongoza.
Katika suala la uhuru wa maoni kuna kanuni moja ambayo pale Marekani huwa wanaitumia sana kuzuia maoni yenye kuhatarisha usalama wa watu. Kwamba “huwezi kupiga kelele za ‘Moto Moto’ kwenye ukumbi uliojaa watu” wakati hakuna moto wowote na ukiulizwa useme ati “nilikuwa natumia haki yangu ya maoni”. Wale wanaotuambia “ukabila ukabila, udini na udini” kama hawamaanishi hicho na kama hakuna ushahidi wanachezea mchezo wa “moto moto”.
Kuwaendekeza hawa ni kuliandaa taifa kwa majanga kwani chuki dhidi ya Wachagga ambayo imepandikizwa kwa muda mrefu katika jamii fulani ya watu inazidi kukua na sasa kuna ushahidi imepitishwa kwenda kizazi cha pili.
Tunakumbuka sisi wengine kuwa chuki hii ilikuwepo wakati wa Mwalimu hadi tume ya Mang’enya ikaundwa kufuatilia na sasa hivi wameibuka watu wengine ambao wanalindwa na watawala walioko madarakani kwa ajili ya kujipatia manufaa ya kisiasa wakiendeleza chuki dhidi ya Wachagga.
Watanzania ni lazima waanze kuwakataa viongozi hawa na wakati umefika kiongozi wa kisiasa yeyote atakayetoa kauli hizi na kushindwa kuthibitisha au kuchukua hatua kushughulikia wale wenye “ukabila” na “udini” ni lazima awajibishwe mara moja na hata ikibidi kuandamana kuwapinga.
Ninaamini sasa CHADEMA wasivumilie tena tuhuma hizi ambazo wamezitolea ufafanuzi miaka nenda rudi lakini zinaendelea. Akijitokeza tena kiongozi yeyote wa serikali ambaye atadai CHADEMA ni cha Wachagga, CHADEMA iitishe maandamano ya kumuondoa mtu huyo madarakani kwani hatuwezi kuendelea tena kuchezea tunu zetu za taifa ambazo nilizigusia katika toleo lililopita. Wakati umefika kuwakataa viongozi wa aina hiyo. Na nina uhakika ukitaka kujua ni jinsi gani wana chuki dhidi ya Wachagga waulizeni mnataka CHADEMA iwafanye nini hao Wachagga walioko ndani yake? Mtashangaa watakavyojiuma meno kutafuta majibu. Hili nalo waulizwe wale wenye kudai kuwa CCM ni chama cha Waislamu.
 
Mkuu MKJJ Bravo hii vita ya Ukombozi unaipigana, tupo na wewe tunaelewa na kujali sana mchango wako kwa ustawi wa Taifa hili.

Ni katika nchni ya wapumbavu pekee ndio inayoweza kuacha kutumia rasilimali yake kiasi hiki, Tanzania inapata hasa kubwa sana kutoka na kushindwa kupanga na kuwekeza katika rasilimali watu! Mwakijiji ni rasilimali ambayo kutokana na upofu wa viongozi wetu haitumiki barabara, yamkini labda rasilimali kama hizi zipo nyingi zinapotea wakati serikali yetu haina watu kabisa.

Mungu akuongezee nguvu na maisha marefu Tanzania inakuhitaji.
 
{Viongozi wengine, wakuu wa taasisi za umma ambao wakiona jina la Kichagga wanafikiria ni jinsi gani hawatompa mtu huyo nafasi.
Kuna mifano ambayo siku moja ikiitwa wazi tutaona haya kwani baadhi ya watu wanaotukuzwa kwa "uongozi bora wa mashirika ya umma" ni wabaguzi wa kikabila waliokubuhu ambao wanastahili tuzo mbovu ya ufisadi wa kidini! }

Najua hapo amemsema mtu anayechezea mafao yetu kule kwenye akiba ya kustaafu. Nimeona article mahali , ikabidi nigune tu kwa kumsifia yule jamaa.....
 
Waislam ambao mnajinasibisha na Chadema mmemsikia Rais wa Jf???????????????????????? kaamua kuweka wazi Waislam amtakiwi Chadema :A S 103:

NANI RAIS WA jf?? ULIMCHAGUA LINI? RUDIA TENA KUSOMA MAKALA YAKE UTAJUA KILICHOMO
 
Halafu unakuwa na majitu maprofesa, madokta, malawyer wamejazana kwenye CCM , na hawaioni hatari hii.
Hivi Pinda, Mwandosya, Mwakyembe, Magufuli, Pius Msekwa, na wengine wengi ndani ya CCM ambao sio Waislam kwanini wamekaa kimya wakati sumu hii hata wao haitawaacha salama?
Ni uvumi wa wazi unaelekezwa kwa makabila ya Wanyakyusa, Wachaga, Wasukuma na Wahaya , kwamba ni wakabila na hawafai kupewa uongozi wa juu wa nchi hii. Propaganda hizi zinapigwa huku ndani ya CCM hiyo hiyo wamo viongozi wanaotoka makabila hayo. Kwa nini wananyamza? Wanategemea nini? Eti Pinda "mtoto wa Mkulima" huoni hayo yote? Au na wewe umeingia kwenye lindi la kashfa za kifisadi ndo maana umbung'aa tu huku ukiangalia nchi inayumbishwa na majitu yaliyochoka akili na wewe upo kama Wazirti Mkuu. Ni ajabu sana sijui ametokea wapi huyu Pinda , maana haya mambo hayastahili kuendelea kuzungumzwa kama vile yeye hasikii. Anabaki kulia lia tu kwa kutetea unga wake! Wakati umefika kwa watu wanaotoka haya makabila waanza kujitetea kwa kuandika makala kama hii ya Mwanakijiji, kwani kuendelea kukaa kimya kunafanya watu wote waamini upupu huu wa viongozi wa CCM.
 
Hivi wakristo wote na wachagga wakiamua kwenda CHADEMA CCM itabaki na nini??
 
Mbona mwalimu JKN, ALISHASEMA CHADEMA SAFI!! Je JKN alikuwa mkabila? Acheni uzushi ccm, Baba yenu aiishasema CHADEMA safi nyinyi mnasema ni chama cha kikabila. Hii imekaa kilaana laana, ndiyo maana mna hali mbaya, rudini kwenye kaburi mkatambike kama kawaida yenu.
Je mmekosa adabu hata kupinga fikra za mwenyekiti,mnasau nahau, nyimbo zenu zilizotukuka? Capt. Komba ebu wakumbushe.
 
M.M Mwanakijiji kachemka vibaya na hiyo hoja yake regerege, uwezi kafananisha Dini na kabila, Uislam ni zaidi ya uchaga, sababu kasema Rais wa Jf inaonekana hoja ya msingi, Mwanakijiji vipi Waislam ambao wapo Chadema unawaweka wapi?

Je Wachagga waliopo cc-J samahani M, wabadili kabila! Kichwabuta we!!
 
M.M MWANAKIJIJI nakuombea na nitazidi kukuombea mungu akuzidishie Hekima,Busara na uwezo wa kupambanua mambo.najua wasiopenda maendeleo watakuchukia, pia na wale wanaopenda kuona watanganyika tukiendela kuwa mbumbumbu. makala zako zinaleta awareness kwa raia katika harakati za kutafuta UHURU WA KWELI, Ambao waTanganyika walio wengi wanajua utaletwa CHADEMA.:A S 103:
 
CCM ni chama cha Kitaifa na kimataifa..kisera na hata kiuongozi (mpangilio nk)

Chadema ni chama cha kidini (ukristo) na kichagga kisera na hata kiuongozi (mpangilio nk)

Utaratibu wa kupata viongozi wa juu unaratibiwa na kanisa..kwahiyo waislamu watawekwawekwa tena wachumia tumbo e.g. Prof. Safari, Yule makamu wa darasa saba (kama vile wamekosa educated muslims) wanafanya kiini macho....

Chadema ki-utaratibu kinahakikisha maslahi ya kifedha yanafaidisha wachaga..tafuta watunza fedha na watumiaji fedha wengi wanatokea huko..wengine mtachujwa na kuzushiwa kashfa mpaka muondoke...

Waislamu wenye uwezo wamebinywa kwa maelekezo ya kanisa katoliki (hidden) mfano Zitto will go no where??, jambo hili linaratibiwa katika jumuia za kanisa katoliki mitaani....

Wanaweza kujivua gamba wakidhamiria kweli..lakini wanakoelekea wataimba sana kupata nchi kwakuwa ni wabaguzi wengi wa washabiki wao ni "christian fundamentlist"

Nembo ya chama ni msalaba (mistari meusi) wakipata nchi wanakamisha...

wamejificha lakini wanaonekana wazi kwa tabia, nyendo zao...

Topical,
Kinachonishangaza unapotoa hoja zako mara nyingi naona kama uko pekee
yako na siku zote hoja hujadiliwa na watu wakachangia na kuonekana upande
mmoja umeshinda,Lakini wewe mara zote nikiangalia hoja unazopinga naona
wazi umeegemea upande mmoja kama vile unafaidi zaidi matunda ya uhuru wa
Tanzania bila kuona huruma ya watanzania walio wengi.
Labda nikufahamishe kuwa CCM ni chama cha mapinduzi ya amani kati ya
vyama vya TANU(TAA) na ASP
CCM ni sehemu ya maisha ya watanzania,
ccm ni msingi wa siasa za Tanzania,kila mtanzania unayemuona leo ktk Siasa
ukiondoa wachache sana wametokea CCM,
Mimi ni mwanachama wa ccm kwa miaka 25 (Believe it NOT)
Tofauti iliyopo kati ya CHADEMA na CCM ni kuwa CHADEMA kwa miaka michache
sana tangu kuanza siasa za vyama vingi imeweza kuwa mshindani wa karibu sana
na CCM.Hizi ni jitihada za hali ya juu sana kwenye ulingo wa siasa za ushindani.
Kwa mantiki hii utaona wazi kuwa CCM imeshazeeka na inahitaji damu changa ili kiende na wakati
Sasa bahati hiyo tayari imeshapotea na badala yake imeshikwa na CHADEMA na kwa taarifa yako
CCM inaelekea UPINZANI.Huu ndio ukweli na wenyewe wameshakiri wamepoteza umaarufu na mvuto.
sasa ccm wameshaanza siasa za majitaka...oh chadema ni wachaga,mara ...oh chadema ni wakristo..
.oh chadema wanapoka demokrasia
Watanzania wameshajua nani mtetezi wa kweli hapa...ccm au chadema....niambie mwenyewe Topical.
Naomba uniambie sababu mbili (2) tu za kushindwa kwa ccm.
Sbabu (2) za CHADEMA kupanda chati.
 
Back
Top Bottom