Tanzania Bara vs Kenya - Live

Dakika ya 24,

Kenya wanapiga touch nzuri, lakini ndo hivyo tena... Tanzania iko kwenye ardhi yake.
 
Nizar Khalfan anaonekana ni kijana mzuri pamoja na Danny Mrwanda.

Hawa wanaifanya defense ya Kenya ipate shida.

Dakika ya 26 inakwenda
 
GOOOOAAAAAAAL!

Nizar Khalfan anaipatia Tanzania bao la kwanza dakika ya 18 baada ya wachezaji wa Kenya kuunawa mkono.
Asavali maana nilifatilia tangu unaanza kuandika nikawa naomba niskikutane na maandishi "harambee Stars wanaandika bao la kwanza".Tunafatilia
 
Hahaha,

Nakumbushwa Tanzania ilishinda Big Brother na imeshinda kumweka Tenga kama Rais wa CECAFA hivyo leo itaanza mashindano haya kwa mori mkubwa ikitaka kuendeleza wimbi la Ushindi.

Ngoja tuangalie hatma yetu. Dakika ya 29 inakwenda hiyo.

Tanzania 1 - Kenya 0
 
Mtu,

Kwenye soka lolote linawezekana. Lakini uchezaji wa Stars usipobadilika basi uwezekano wa kushinda mechi hii ni mkubwa.

Mashambulizi yanafanyika ila udhaifu wa defense yetu ndiyo hatari inayotukabili.

Uwanja mpya wa taifa unaonekana kwa mbali na unapendeza kwelikweli. Natamani mechi hii ingechezewa uwanja huu!
 
Kumbe upo Robot? nilitaka kutoka nikajua mpira umekwisha naona offline......Vipi morali ya mashabiki ipo kama siku ile ya Mozambiki?
 
Ajabu nyingine ni kuwa wachezaji wetu wanaonekana kuwa wafupi kila timu wanayokumbana nayo. Hivi watanzania ni wafupi?

Dakika ya 34 inakwenda hiyo.
 
Mtu mechi hii nitakuleteeni yote hadi iishe kwakuwa nimesikia Tv za nyumbani Tz hazioneshi.

Dakika ya 36 inaenda mambo bado ni Tanzania 1 - Kenya 0
 
POA walau leo tunaweza kupata jambo la kucheka baada ya muda mrefu wa kulilia mafisadi.
Ripoti ya REDET yaweza kuwa historia leo/kwamba hayo ni mafanikio ya CCM vipofu na wapinzani hawaoni.
 
Danny Mrwanda akiwa katika kujiandaa kuipa Taifa Stars goli la pili anawekewa 'kubwa' na sasa anabebwa kwa machela kwenda nje.

Dakika ya 41 inakwenda hiyo
 
Uzuri mmoja ni kuwa si wote tuna akili fupi. Mtu, hata vidole havilingani. La wachezaji kuwa wafupi linanishangaza.

Kona kwa upande wa Kenya kuelekea Tanzania. Dakika ya 42
 
Kenya hawapati mipira sana (umiliki) lakini wakibahatika kupata wanacheza 'touch' nzuri sana.

Hata wenzangu nilio nao hapa wanadai wachezaji wa Stars 'wa enzi hizi' wengi wafupi.

Dakika ya 44 inakwenda, bado Tanzania 1 - Kenya 0
 
Habari za kusikitisha!

Dakika ya 47 Kenya wanasawazisha kwa njia ya Penalti na mpira ni mapumziko.


 
Back
Top Bottom