Tanzania awards $500 mln oil supply deal to Swiss firm Augusta; GVT hope will lower prices...

Kalalee. Hatuwezi kusovu matatizo ya EWURA kwa post katika JF saa 9 hizi za usiku!

Inauma Mkuu ukizingatia maisha yamekuwa magumu if you go down deep sometimes someone was supposed be hanged up kwa kutusababishia ugumu wa maisha bila sababu ya msingi.Maisha magumu madakatari wanagoma kwa kuwa maisha yamepanda nao wanaitaji kipatao zaidi,watu wanapoteza maisha kisa watu walishindwa kutimiza wajibu wao kwa muda sahihi na wakati sahihi.
 
Mkandara,

uko sahihi, lakini unadhani JK akienda nje kutengeneza masoko, kwa bidhaa zipi? kwa ubora gani? kwa mazingira gani ya production ilhali umeme hakuna? Je, si bora tunge concentrate kuinua viwanda vyetu kwanza, kwa kuhimiza uzalishaji competitive ili bidhaa hizi ziweze kushindana na masoko ya nje?

Chukulia mfano cement tu hapa...production yake inaathiriwa sana na suala la umeme, udhaifu wa shilingi na transport system, kiasi kwamba ikipambana na cement toka nchi za COMESA (hata itoke Egypt) hii yetu inapoteza soko kwa kuwa production costs ni juu.

Ninakubaliana na wewe kila kitu hapo, lakini kuna basic things ilikuwa tuanze navyo then tuvutie wawekezaji au hata kutafuta masoko ya nje. Mimi ninafuatilia sana foreign reserves, ambazo kwa kiwango kikubwa inakuwa boosted na what we export. Mathalan, wakati Mkapa anaondoka 2005, FR ilifikia ya kutosha imports za miezi 8.5, lakini kuna wakati ilishuka hadi miezi 3, why?
Mkuu wangu kama huna cha Kuuza hbasi huna sababu ya kwenda nje kuomba misaada..Na kiongozi mwenye kuelewa siasa lazima angeenda nje kuomba msingi au niseme mtaji hivyo akijua atawekeza kwenye Umeme na Maji ambao ndio utamwezesha kuzalisha.

Unajua sisi tuna Mila chafu sana na umaskini wetu unatokana na mila za maskini wenyewe ndio maana hatuendelei. Ile tabia ya mtu kukufuata akakuomba fedha ya chakula au nyumbani hatuna chakula ukapewa halafu kesho unaingia tena barabarani kuomba hela ya Chakula (Zamani tukisema ana bomu) ndivyo tunavyoendesha maisha yetu hata Kitaifa. Maadam JK anakwenda nje kuomba isaada ilitakiwa misaada hiyo iambatane na malengo ambayo sisi tutaahgidi kuzalisha nini ili kesho tusirudi tena kuomba.. Sawa na mtu ama nduguyo aliyekuomba mtaji aanzishe biashara. Hivyo unampa mtaji ukijua kesho atarudisha mkopo wako ama umempa lakini kesho hatarudi tena kuomba mssaada maana umemwanzishia maisha..

Sasa Ukitazama hulka ya Mtanzania kiasili na umaskini wetu tumejaliwa kamba na utapeli sana ..yaani kudanganya hali ni kwa maisha yetu wenyewe. Mtu atakuja kukuomba hela ya chakula ukimpa atasema ahsante lakini atamfuata mwingine na kumwomba pia, Usipoomfuatilia atakwenda kunywa pombe hivyo bora umpeleke Restaurant moja kwa moja nako pia hutakuwa hujamsaidia isipokuwa mlo wa siku moja, kesho matatizo yako pale pale..
Na
mwingine utakaye mpa Mtaji vile vie atakwenda kulewa pombe ama kutafuta mabinti au kuwekeza robo ya mtaji ambao hautamweshesha kudumu (sustainability) hivyo miezi miwili tu atarudi chini na kuomba tena. Siku hizi imeingia Tabia ya Wabongo anapokuomba mtaji anakupigia mahesabu wewe mwenyewe na fedha zako yaani ukikaa vibaya hata hizo zako atakunyonga.. Haya ndio maisha ya maskini na fikra na Mtanzania toka chini kwa mwananchi hadi kitaifa kwa rais wetu..Ni utapeli na kuendeleza umaskini..

hakuna nchi inayonunua mafuta ya Usd 2.5 billioni kila mwaka pasipo kuhakikisha watabadilishana vipi maana sio swala la uwezo wa kununua kwa cash money hata kidogo ila wewe pia utaweza vipi kuuza mali zako kwa uhitaji wako wa mafuta yale. Nchi zote duniani zinahitaji mafuta na zinafanya deals za mauzo na kubadilishana. Nimekwambia mfano Canada inawauzia Marekani mafuta nao Marekani wanatuuzia mali zao.. Japan wanaleta magari yao kuuza huku sio kwa sababu kuna soko huru laa hadsha ni baada ya wao pia kukubali kununua bidhaa za Canada..Kama wakikata manunuzi canada na Canada nayo itakata manunuzi ya mali zao. Yaani trade baina ya nchi i kama balozi ukimnwondoa wangu nami nitamfukuza wako, hakuna cha free trade hata kidogo kaa tunavyofikiria bali ni free kwako wewe mnunuzi/ muuzaji kuchagua utamuuzia au kununua kwa nani ambaye pia atakuwa customer wako..
 
Ninaelewa concern yako mkuu. Kinachomiss siku hizi ni kwamba:
1. Viongozi wetu hawatilii maanani tena nchi kuuza bidhaa zake nje
2. Hata pale inapowezekana, hatuna willingess ya kuwa na bilateral trade relations mfano Japan, UK Canada nk ambako wao sisi wanafaidi kama soko
3. Nadhani yote haya hayawezi kufanikiwa ikiwa economic structure ni mbovu, siyo sustainable. Ndiyo maana hadi leo tunashindwa hata kujilisha wenyewe licha
ya mito na mabonde tuliyonayo.
Nilipata aibu sana nilipokuwa na wenzangu wa Israel, ambao niliwahakikishia kuwa wanaweza kutuuzia teknolojia ya kilimo...tulipokuja Tanzania hakuna watu wa maana walioenda kwenye mikutano ya kujadili hilo. Why
 
Kwa mawazo yako Mkandara, miaka 20 baada ya ubinafsishaji, je ulikuwa uamuzi wa maana? Na utekelrzaji wake ni wa maana? Nini social welfare ya wafanya kazi na wakulima kwenye ubinafsishaji? Umewanufaisha?
 
Kwa mawazo yako Mkandara, miaka 20 baada ya ubinafsishaji, je ulikuwa uamuzi wa maana? Na utekelrzaji wake ni wa maana? Nini social welfare ya wafanya kazi na wakulima kwenye ubinafsishaji? Umewanufaisha?
Neno uamuzi linachukua maana ndefu zaidi na nitakueleza kwa nini. Aamuzi wa kuingia Ubepari ulikuwa wa maana kwa sababu uchumi wa nchi unatakiwa kuendeshwa na watu binafsi sio serikali isipokuwa huduma za kijamii ambazo serikali inaweka mikataba ya makubaliano na mashirika binafsi ktk utekelezaji wake -Tender.

Kama nilivyosema hapo juukwamba sisi hatukubinafsisha japokuwa wazo la kubinafsisha lilikuwa zuri isipokuwa tulichofanya ni ku liquidate mali na mashrika ya Umma aidha kwa makusudi ama kutoelewa mfumo mzima wa Ubepari unafanya kazi vipi. Kwa hiyo ni Uamuzi wa maana, lakini utekelezaji wake haukuwa wa maana hata kidogo (ufisadi mtupu). Na ndio maana Mh. Zitto ktk kutembelea mashamba ya Mkonge na Korosho amesisitiza mashirika ambayo yameshindwa kutimiza wajibu wake yataifishwe tena..

Pengine this time tutaweza kufanya inavyotakiwa, mimi ningeshauri hata viwanda na mashirika yaliyotaifishwa ambayo yameshindwa kufanya kazi yataifishwe tena na safari hii wapewe watu wenye nia na uwezo wa kufanya kazi.. Kama mwananchi anaweza kunyang'anywa shamba au kiwanja kwa sababu kashiundwa kujenga inakuwaje vigumu kwa serikali kuwanyang'anya wenye mashamba,viwanda na mashirika yaliyo binafsishwa ambao wameshindwa kuyaendeleza kwa zaidi ya miaka 10..

Na kuhusu social walfare ya WAKULIMA na WAFANYAKAZI nadhani sote tumeona jinsi wasivyothaminika leo na haya yote ni matokeo ya kufilishisa mashirika ya Umma ambayo ndio kiungo cha nguvu zao ktk uthamini wa kazi na uzalishaji. Kama nilvyosema hapo awali, huwezi kutegemea mkulima kuendelea kulima Korosho ikiwa hawezi kuziuza kiwandani, na mwenye kiwanda hawezi kuendelea kununua korosho ikiwa soko lake limefungwa isipokuwa kwa kupitia mawakala wa nje (walanguzi) Hivyo basi utaona tatizo lipo kimfumo zaidi, sisi tumewekewa vikwazo vya kupitia walanguzi wa nje kuuza mali zetu na sasa tunapitia tena walanguzi hata kununua mafuta toka nje

Huu utaratibu wa Tender kuuza mali zetu ama kununua kwa WALANGUZI tukiepa majukumu ya kiutawala ni njia ya mkato sana ambayo inatugharimu aidha mali zetu kununuliwa kwa bei ya njugu lakini zikiuzwa sokoni ama nje kwa bei kubwa (Korosho kuuzwa India) ama sisi wenyewe kununua mali zao kwa bei ghali zaidi (mafuta ya Agusta Energy). Mkulima ataendelea kuwa mkulima maskini na sii mkulima mfanyabiashara kwa sababu tunamyima fursa yeye mwenyewe kulima na kuuza mali zake kiwandani..Na mfanyakazi pia tunawadumaza tumeondoa value of function ndio maana Mbunge anapokea mshahara mkubwa kuliko daktari bingwa.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
mimi ningeshauri hata viwanda na mashirika yaliyotaifishwa ambayo yameshindwa kufanya kazi yataifishwe tena na safari hii wapewe watu wenye nia na uwezo wa kufanya kazi...

Hivyo basi utaona tatizo lipo kimfumo zaidi, sisi tumewekewa vikwazo vya kupitia walanguzi wa nje kuuza mali zetu na sasa tunapitia tena walanguzi hata kununua mafuta toka nje

Mkuu, nakubaliana nawe juu ya kuwa na matatizo ya kimfumo, na kila mara nimekuwa nikitoa angalizo kuwa remedy yake haiwezi kuwa marekebisho ya juu juu tu. Ni pale tutakapopata uongozi thabiti utaodhamiria kuusuka upya mfumo wetu wa kiuchumi, ndipo tutapoiweka nchi kwenye njia sahihi, badala ya sasa tunavyoziba viraka.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Haya Wakuu Mkandara na AK48 Mafuta yamepanda ni Petrol,Diezel na Mafuta ya Taa.Mbalamwezi na utetezi wake EWURA na Project mpya ndio kusema kuwa Jawabu lao imekula kwetu!!!!Maisha ya watu wazima !!!!!!!!!!!!!!!!
 
Haya Wakuu Mkandara na AK48 Mafuta yamepanda ni Petrol,Diezel na Mafuta ya Taa.Mbalamwezi na utetezi wake EWURA na Project mpya ndio kusema kuwa Jawabu lao imekula kwetu!!!!Maisha ya watu wazima !!!!!!!!!!!!!!!!

Sidhani kama kuna dawa ya kufanya bei ya mafuta ishuke ikiwa kwenye source itapanda. Sidhani. Labda nieleweshwe inawezekanaje. Ngoja nitatafuta tangazo lao nione wameeleza nini, pamoja na vyanzo vingine. Na kuni brand kuwa mtetezi wao nadhani si vema. Kila mara tunajadili hoja kwa hoja, na nimeshakuonya kuwa branding ya namna hiyo impeds one's thinking, kwa kuwa hutanisikiliza kwa sababu tu ni wa namna fulani. Umeshafika mahali ukaniuliza hata umri wangu, sijui utaridhika, au ndo utauliza na kabila, rangi, na urefu?

Pls lets keep sensible discussion. Learn from the two brothers AK48 na Mkandara. Sote tunahitaji kujifunza kutokwa kwa kila mtu, kwa utaratibu wa kusikiliza hoja za mtu kwa kadiri anavyowasilisha na kuzipima kwa namna ambayo tunaweza.
 
"Petroli imeongezeka kwa Sh 87/lita sawa na asilimia 4.06; Dizeli imeongezeka kwa Sh 3/lita sawa na asilimia 0.14; na Mafuta ya taa yameongezeka kwa Sh 12/lita sawa na asilimia 0.59. Mabadiliko haya ya bei za mafuta hapa nchini yametokana na mabadiliko ya bei katika soko la dunia ambapo bei ya mafuta ya petroli imeongezeka kwa wastani wa dola za marekani 95.7 kwa tani sawa na asilimia 9.09, mafuta ya dizeli yameongezeka kwa wastani wa dola za marekani 27.1 kwa tani sawa na asilimia 2.76, na mafuta ya taa kwa dola za marekani 34.04 kwa tani sawa na asilimia 3.28."

Niliahidi kukutafutia, haya, endelea.
 
Sasa tumeona mafuta hayatoshi ni makusudi ya kuongeza bei hakuna vita wala nini sasa ni kwanini mafuta hakuna!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom